Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

Wasomali hawana kodi kama huku dubai hawana ushuru wowote wa port.huwa wanakuja na meli zao chakavu wanapakia bidhaa kiasi wanachohitaji bila kodi aina yoyote(exempted)kisha wanaondoka!
Jamaa wana roho ngumu wale wanaweza kusafiri na MV LIEMBA hadi marekani.
 
Wasomali hawana kodi kama huku dubai hawana ushuru wowote wa port.huwa wanakuja na meli zao chakavu wanapakia bidhaa kiasi wanachohitaji bila kodi aina yoyote(exempted)kisha wanaondoka!
Jamaa wana roho ngumu wale wanaweza kusafiri na MV LIEMBA hadi marekani.
Hahahaaa,nimecheka kweli.MV LIEMBA mpaka Marekani inaweza tumia miaka 100.
 
Vijana wa Tanzania acheni kuangalia huyu ana nini yule ana nini! tumieni ubongo wenu kuwa wajasiriamali! hawa lazima walianza chini mpaka wakafika hapa!

Tanzania ni nchi ilobarikiwa na rasilimali nyingi sana tumieni rasilimali zenu mtafanikiwa!
 
Yes halafu wana ushirikiano mno. Kitu ambacho sisi hatuwezi

Ni kweli hawa jamaa wana ushirikiano mno,hata jumuia zao nchi za nje iwe marekani ama UK au South Afrika zina nguvu sana, wanapeana kampani ile mbaya,ndio maana nchi yao ni robo karne sasa wanatwangana lakini wananchi wake hawana shida kiviile kwa kuwa waliopo nje wanatuma sana pesa nchini kwao na kenya kwa kutumia utaratibu wao wanaouita Hawala,wanatuma pesa nyingi sana mpaka serikali za marekani na Uingereza wakaufungia huu mfumo kwa kudhani kama ndio mfumo unaofadhili ugaidi kumbe ni mfumo wao wamaisha kusaidiana kwa walio nje ya nchi kuwapa kampani wale waliopo nyumbani afrika.
 
Kama ilivyo Tanzania sio wote ni maskini same to Somalia,,, maskini na matajiri wapo wengine hadi wanajiuza Kampala kwa wingi,,,,, matter of fact Somaliland, puntiland wako na usalama na bandari kubwa za 350000+ containers per year,,, Somalia-mogadishu ndio wanakiamsha.
Hivyo, hao jamaa wana kila sababu ya kutajirika
 
Wasomali wanapiga kazi balaa, kuna mama bilioner wa kisomali kawekeza Kenya shida tupu, sasa hivi anajenga kiwanda cha sukari uganda analima miwa kijiji hapo uganda kwa ajili ya kiwanda chake..

Vijana wa bongo wanapo nikasirisha ni kujifariji kwa maneno ya kipumbavu, watakwambia hao vijana walikuwa mapirates,

Hakuna mwekezaji anae kuja nchini kwako na hela kwenye mabegi hela zote wanazichukua kwenye mabenk yenu ya ndani...

Vijana waache wasubirie ajira za magufuli na kushinda kwenye vijiwe vya siasa na magrup ya whatsapp,

Tanzania atafika siku 96% ya uchumi wa Tanzania utashikwa na raia wa kigeni
Hujui usemalo wewe,, kimada wa Museveni huyo.
Mzee, This is Africa
 
Wasomali ni Bright sana...ndio maana hata nchi yao iliharibiwa makusudi na mataifa ya Magharibi sababu walishaproject future ya Somalia wakaona ni tishio.
Wasomali ni watu wenye discpline sana ya Maisha na ndio maana ni wasomali wachache sana tulio nao kwenye Jamii yetu wanaoishi Maisha ya kubabaisha.
Wasomali ni Risk takers wa ukweli sana na wao wako tayaribwafanye lolote mara wanapotaka kitu.
Wasomali wemgi hasa vijana hawana tabia kama za sisi vijana wa Kibantu! Wenzetu wanainuana sana na hakuna dharau kati yao ndio maana wanasonga mbele, sie tunabaguana hata kumiliki simu tofauti tuu au gari tofauti( Ujinga na upumbavu wa Kibantu na Kiswahili).
Wasomali si watu wa kuendekeza Starehe za Kipuuzi!
Msomali hata awe na hela vipi hana asili ya Show Off kama sie! Na msomali haridhiki na vitu vidogovidogo na kujisahau, Kijana wa Kibongo tena graduate anakopa hela anaenda kununua Gari na simu ya kisasa..garo anapaki CCM lakjni hata kusalimia jirani inakuwa ni shida!
Mwisho, wasomali hawana tabia za ubabaishaji!
Huwajui wasomali,,, wanapenda starehe balaa,, ni malaya kuanzia wanawake hadi wanaume na maskini ni wengi... Kwa ufupi ni binadamu wengine kama sisi..
 
Warudishwe kwao wanabana nafasi za ajira
Ama kweli wewe ni hasidi na mjinga, hao ndio wanaotengeneza ajira, kila familia ya kisomali inaajiri wafanyikazi wawili wa nyumbani, kila mfanyi biashara anaajiri sio chini ya wanne, kama hawa vijana waliotajwa hapa wameajiri watu wengi kuanzi makuli hadi wahesabu na mameneja, sio kama wahindi wanaoleta wafanyakazi kutoka India ama huwaajiri wahindi wenzao waliozaliwa hapa.

Wasomali hawana ubaguzi ni waafrika wenzatu.
 
Wasomali wanapita njia zote walizopita Wahindi tofauti yao kubwa ni kuwa Wasomali wanaongea Wahindi ni wasiri sana.

Ilianza biashara vya neno ya tembo mhindi alipiga kwa miaka mingi. Msomali alipoanza dunia ilijua.


Kujilipiua ukimbizi Ulaya Mhindi aliaanza, tokea mmgawanyiko wa India na Pakistan mpaka Iddi Amin kufukuza Wahindi Uganda

Msomali alipoanza hata sisi wamatumbi wa Kyela tulijilipua Kisomali.
Ni kweli kabisa nimekutana na wadigo na wasambaa uingereza walipewa sheria ya ukimbizi na sasa ni wananchi huko, wamejipa kama wasomali.
 
Wale woote ambao wako chini ya miaka 40, mjitahidi kufanya set-up ya kibiashara ili familia baadaye ziwe na family business na sio kupiga blah blah hapa..
Ukimsikiliza jamaa anaeleza kabisa walikuwa na business Mogadishu kabla ya vita na ilikuwa furniture business na material walitoa Tanzania, hii ilikuwa family business ya baba zao au babu zao kutokea hapo ndio set-up ilifanyika..

"Tanzania is blessed"
 
Baada ya kuangalia documentary hii ya kijana huyu wa kisomalia Mahad Nur na ndugu yake Mohamed Nur, wanaomiliki City Mall , Victoria Plaza na Africa flight Service, a cargo company , nimejiuliza inakuwaje vijana wa kisomalia kama hawa wanatoka mogadishu wanakuja na kufanikiwa hapa hapa kiasi hiki lakini sisi tupo tu wala hatuzioni hizi fursa sana sana , vijana wamebaki kusubiria ajira.

Kweli hii ni changammoto kubwa sana kwa nchi yetu.

Tusaidiane mawazo




Wana backup ya ndugu zao walio ulaya na america na hao ndio wanahisa.
 
Ama kweli wewe ni hasidi na mjinga, hao ndio wanaotengeneza ajira, kila familia ya kisomali inaajiri wafanyikazi wawili wa nyumbani, kila mfanyi biashara anaajiri sio chini ya wanne, kama hawa vijana waliotajwa hapa wameajiri watu wengi kuanzi makuli hadi wahesabu na mameneja, sio kama wahindi wanaoleta wafanyakazi kutoka India ama huwaajiri wahindi wenzao waliozaliwa hapa.

Wasomali hawana ubaguzi ni waafrika wenzatu.
Huwajui wasomali we kiazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom