Mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar wadaiwa kumlawiti mwenzao hadi kufa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,136
Mahabusu adaiwa kufa baada ya kulawitiwa Segerea
Na James Magai

MAHABUSU katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kumlawiti mwenzao hadi kufa.

Habari zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita zilisema mahabusu huyo Hasara Omar anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 20 alifanyiwa kitendo hicho Jumatano iliyopita.

Alipoulizwa na Mwananchi jana kuhusiana na tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Mtiga Omari, alikiri kupata taarifa za kifo cha mahabusu huyo.

Hata hivyo ACP Omari alisema taarifa anazozifahamu ni kwamba mahabusu huyo anadaiwa kupigwa na mahabusu wenzake na kwamba alifia hospitalini.

Lakini habari zilizopatikana kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu(SMS) kutoka kwa mtu ambaye hata hivyo hakujitambulisha zilisema mahabusu huyo alifikishwa gerezani hapo siku ya Mei 27 na kufanyiwa vitendo hivyo usiku hali iliyosababisha kifo chake.

Katika SMS hiyo ambayo hata hivyo haikuwa na ufafanuzi wa kina kuhusiana na tukio hilo, mtumaji ambaye alionekana kutuma ujumbe huo kwa hofu huku akiliita tukio hilo kifo cha kinyama, aliomba msaada wa vyombo vya habari pamoja na vyombo vya kisheria kuingilia kati katika tukio hilo ili wahusika waweze kuchukukliwa hatua.

ACP Omar alisema mahabusu huyo alifikishwa gerezani hapo Mei 27 na kwamba inadaiwa alipigwa na mahabusu wenzake usiku, na alitolewa gerezani hapo Mei 28 na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Licha ya kuwa na taarifa hizo za mahabusu huyo kupigwa na mahabusu wenzake, ACP Omar alisema kuhusu chanzo cha kifo cha mahabusu huyo bado wanasubiri taarifa ya uchunguzi wa chanzo hicho (Postmortem Report) kutoka hospitalini hapo.

“Ninachofahamu mimi ni kwamba Segerea kuna mahabusu alifariki dunia, na alifariki akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, taratibu zetu za kisheria ni kwamba ‘cause of death’(Sababu ya kifo) ni baada ya kufanyika postmortem(uchunguzi),” alisema ACP Omar.

Alipoulizwa sababu ya mahabusu hao kumpiga mahabusu mwenzao, ACP Omar alisema kwa sasa bado wanafanya uchunguzi juu ya sababu ya mahabusu hao kuchukua hatua hiyo.

Aliongeza kuwa watakaogundulika kuhusika na tukio hilo watachukulia hatua za kisheria.

“Kama unavyojua kumuua mtu ni kosa la jinai, kwa hiyo bado tunasubiri kujua taarifa ya kifo, waliompiga watafikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka,” alisisitiza ACP Omari.
 
Si kuna mkubwa mmoja wa jeshi la magereza alisema haya mambo hayafanyiki katika magereza/mahabusu yetu? Mpaka hapo tutakapoweza kukiri uovu unaotendeka katika jamii yetu bila kuoneana haya, tutaendelea kuzikana.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.

Amandla......
 
Bongo wallah usiombe kupelekwa lupango,ni nusu kifo maana ukitoka hai shukuru mola wako.Till when lakini?
 
Hivi upuuzi huu ni kweli hauwezi kudhibitiwa?? maana hizi habari za vitendo vya ulawiti magerezani nimezikia siku nyingi sana! Nchi hii bwana, na hii eti kwa wakubwa siyo kashfa.
 
Jeshi la Magereza lazima liwajibike kwa hilo...mbona huyu kamishna mpya anakutana na matukio yasiyo kawaida au sababu ya utandawazi.....ndiio habari zimavuja????tunahitaji majibu yanayoridhisha toka kwa wahusika.......
 
Haya mambo yanatendeka kwa kasi sana huko kwenye magereza. Wengine huko wanakuwa na partners kabisa na kuwa huyo huwa hachangiwi. Kuna ambao pia wanafanya kwa ridhaa pia kwa ujira wa sigara, sabuni, bhangi, n.k. Ukimwi kule ni kama kawa!!! Condom zipo ila supply ni ndogo sana kuliko demand hivyo, tegemea masuala ya pekupeku ni makubwa.
 
Jamani hivi askari magereza usiku hawana zamu au inakuwaje?? na hadi mtu anapigwa au analawitiwa hadi inampelekea kifo - wao wanakuwa wapi?? Inabidi waliokuwa zamu siku hiyo wawajibishwe pamoja na hao viongozi wao - thats is too bad - hata kama mtu ni mhalifu lakini hupaswi kufanyiwa hivyo na wahalifu wenzako. Pole kwa ndugu na jamaa za marehemu
 
Ukitilia maanani kwamba si kila apelekwae mahabusu ni mharifu na maafisa wa magereza wanalijua hilo,maana yake ni kuwa wao walitakiwa wawe makini na wale wote wanaopelekwa huko waishi kwa staha zao za kibinadamu,wasilawitiwe wala kupigwa kwa kisingizio chochote,2me that is a full brown murder for which those responsible deserve a death penalty nothing more nothing less...
 
Haya matukio yanafahamika na yanaachwa yaendelee ili kujenga hofu kwa watu waweze kutoa rushwa kubwa sana ili wasiingizwe mahabusu na wao askari kunufaika.
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita nililazimika kutoa rushwa kubwa tu ili jamaa yangu aweze kuangaliwa vizuri akiwa mahabusu.
Nilisikia pia kuna wengine hutoa rushwa kubwa kiasi kwamba huruhusiwa kwenda kulala majumbani kwao na kurudi gerezani kabla ya kuhitajika mahakamani,hii nchi we acha tu!
 
Haya matukio yanafahamika na yanaachwa yaendelee ili kujenga hofu kwa watu waweze kutoa rushwa kubwa sana ili wasiingizwe mahabusu na wao askari kunufaika.
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita nililazimika kutoa rushwa kubwa tu ili jamaa yangu aweze kuangaliwa vizuri akiwa mahabusu.
Nilisikia pia kuna wengine hutoa rushwa kubwa kiasi kwamba huruhusiwa kwenda kulala majumbani kwao na kurudi gerezani kabla ya kuhitajika mahakamani,hii nchi we acha tu!

Unanikumbusha marehemu Mapunda aliyekua anakwenda bar maeneo ya keko wakati ni mahabusu
 
Hapo tumeshahitimisha kuwa kweli kifo kimesababushwa na kulawitiwa....inawezekana kabsa hakulawitiwa isipokuwa alifight asilawitie...akazidiwa nguv akauwawa....tusubiri taarifa rasmi
 
Inaonekana uume sasa ni silaha kama bunduki inayoweza kuleta maafa kwa wengine. Ipo haja ya kuwanyang'anya silaha hiyo watu wote wanaoingia gerezani.
 
Naomba mnisaidie kisheria... Hivi mfungwa akimuua mfungwa mwenzake huchukuliwa hatua gani.? Ameshahukumiwa je atarudishwa tena mahakamani au ataendelea na kifungo chake.?
 
Ni jambo la aibu kubwa mno. Uchunguzi ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria
 
Back
Top Bottom