Jesusie
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 1,367
- 720
Hakika mahaba ya Rais Samia kwa watu wa Kaskazini usipime, ametoa TZS 520BL za maji Arusha ikiwa ni zaidi ya 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka.
" Hakuna kama Samia "
Hakika kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan haikamatiki,Rais ametoa Jumla ya Tshs 520BL zaidi ya 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa kwaajili ya kuzika kabisa tatizo sugu la maji la nenda urudi uje,tatizo lililowashinda wabunge wote wa NCCR, TLP na CHADEMA katika nyakati na muda tofauti tofauti ukanda huo hatimaye Rais Samia amelimaliza kirahisi tu na hii ndio raha ya kuwa na Rais Mzalendo kama Mama Samia Suluhu,
Bajeti nzima ya maji ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2021|22 ni karibu 589BL hii ni kwa mujibu wa bajeti kuu ya Serikali, Rais Samia Suluhu kwa mahaba yake na watu wa Kaskazini kama ilivyo kwa maeneo mengine nchini ameamua kufanya reallocation ya pesa ili Arusha na viunga vyake wapate kiasi hicho cha fedha na hapa nainyooshea kidole CHADEMA kwa kuwachelewesha watu wa Arusha kwa kiasi hiki na kwahakika hawapashwi kuchaguliwa tena,
Kwamsiofahamu,Mradi huu mkubwa wa kihistoria wa Mama Samia unategemewa kutoa Jumla ya Lita 200Milioni kwa siku huku mahitaji halisi ikiwa ni Lita 109Milioni tu kwa siku na hivyo kuwa na ziada ya karibu lita 91Milioni kwa siku ziada ambayo itapelekwa maeneo ya Arumeru na maeneo mengine mengi,
Wakati huohuo Mhe Rais akiwa katika mradi huo wa maji alimmwagia pongezi za dhati Mhe Juma Aweso Waziri wa Maji kwa kile alichokiita uwajibikaji wa kutiliwa mfano ndani ya baraza Lake la Mawaziri,Hongera Aweso kazi zako ni awesome kila Mtanzania atakubaliana na Mhe Rais unastahili songa mbele,
RAIS SAMIA MZALENDO WA VITENDO