Magwangala ya dhahabu mkoani Geita yazua tafrani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu Mkoani Geita wamekataa miamba taka maarufu kama Magwangwala waliyopewa na serikali kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita.

Wachimbaji hao wameikataa miamba taka hiyo mara baada ya kubaini kuwa hayana dhahabu bali yanafaa kwa ujenzi wa nyumba na kusema kuwa miamba hiyo siyo ambayo iliagizwa na Rais kutolewa kwa wananchi hao.

Wachimbaji hao wameongeza kuwa gharama ya kubeba mawe hayo mpaka kuyafanyia mchakato wa kupata dhahabu ni kubwa zaidi ya dhahabu itakayopatikana huku wakisema wamechelewa kutoa miamba taka hiyo ili kufanya uchakachuaji.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema kuwa sababu ya kuchelewesha kutoka kwa wakati miamba taka hiyo ni kutokana na agizo la Rais, masharti mengi yalikuwa yakihitajika kutekelezwa na serikali katika kuipata miambataka hiyo.

Chanzo: EATV
 
Lissu mbona alishasema
 
Muhahahahahahahahahahahaha ahahahahaha! Yaani ndonga jamaa wanatoa makubwa mno wadau gharama za kubeba wanaona bora kuacha Muhahahahahaha Dawa ya Jeuri ni Kusudi..

Nimekuja Kugundua vitu ambavo Mbwana Yule anaona anawakomoa watu fulani karibu vyote humgeuka... Tokea alipokuwa waziri Tumeona Samaki, Nyavu, Barabara mbovu,Elimu fake,Lugha chenga
 
Sasa hiyo miamba taka ya nini jamani...!! Kwa nini msiombe Dhahabu yenyewe...!! Kweli nchi ishaauzwa hii....

Namsubilia mzungu alietengeneza movie ya Yale mapanki ya mwanza aje atengeneze part two ya mapanki ya dhahabu;
Safari hii wabunge watashangilia badara ya kulalamika kama awali
 
Back
Top Bottom