Magunia ya kukusanyia korosho yamekwisha?

Comet

Member
Jul 26, 2019
94
92
Leo nilikuwa natazama moja ya channel pendwa za luninga hapa nchini, msoma habari alisema wakulima wa korosho katika moja ya mikoa inayozalisha zao hilo hapa nchini wamesimama kukusanya zao hilo kutokana na ukosefu wa magunia.

Nilishangaa sana, inawezekanaje magunia yakosekane ilihali msimu wa korosho unajulikana unaanza lini. Vyama vya ushirika vimefanya kazi hizi kwa miaka mingi, je, hawakujuwa ni kiasi gani cha magunia kingehitajika?


Kwa nini mlipomaliza kugawa magunia ya mwanzo hamkuagiza "stock" ya akiba? Ona sasa wakulima wanasimama kukusanya korosho kutokana na uhaba wa magunia, na msimu wa mvua umekaribia. Jamani tuwe makini kwenye kazi zetu!
 
Jiulize izo gunia zinazalishwa na serikal au mtu binafsi? Na anayezizalisha kakubwa na kasymba gani?
 
Back
Top Bottom