Magunia matano yaliyojaa pesa yagunduliwa uwanja wa ndege Nigeria

qaxemvule

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
231
120
Huyu aliosahau gunia tano za pesa hapo uwanja wa ndege huko nigeria makusudi bahati mbaya au maji mengi. dola 150,000/=

==========

_95156902_c32891cd-6020-4221-859c-6d70173e61e4.jpg

Maafisa wa serikali nchini Nigeria wanasema magunia matano yaliyokuwa na mabunda ya noti yamegunduliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.

Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege.

Fedha hizo, za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.

Msemaji wa tume ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na mabunda ya noti mpya za naira 200 na 50, ambayo yalikuwa bado hayajafunguliwa kutoka kiwandani.

Amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo.

Haki miliki ya picha EFCC
Mabunda hayo ya noti yalikuwa yamefungwa na kuwekwa utepe kuonesha yalikuwa yametoka kwa kampuni ya kufua sarafu ya Nigeria Security and Minting Plc (NSPM).

Ibrahim Bappah anayefanya kazi katika afisi ya kupambana na rushwa Kaduna alisema noti hizo mpya ziligunduliwa wakati wa ukaguzi baada ya "harufu nzuri ya kipekee" kutambuliwa.

Magunia hayo yenye pesa yalikuwa yameachwa bila mtu wa kuyatunza na hayakuwa na nembo za kumtambua mwenyewe.The bags were left unattended and without tags.

The EFCC is investigating whether it was an illegal attempt to move money.


Chanzo: BBC Swahili
 
WaNigeria bahati mbaya sana waliwekwa bara chafu...nadhani wangekua sehemu ya Finland au scotland wangekua wanasumbua sana dunia.
Mkuu unamaanisha Africa ni bara chafu.!?
Mi naipenda Africa na ninajivunia kuwa mweusi kabisa bila manung'uniko

Wewe yawezekana hujitambua
Na unaukubali weusi na kuuthamini weupe,
Kwa kweli hiyo kauli yako imenikera sana.
 
Mkuu unamaanisha Africa ni bara chafu.!?
Mi naipenda Africa na ninajivunia kuwa mweusi kabisa bila manung'uniko

Wewe yawezekana hujitambua
Na unaukubali weusi na kuuthamini weupe,
Kwa kweli hiyo kauli yako imenikera sana.
Mkiambiwa bara chafu mnakimbilia kwenye rangi kama kichaka cha kujificha na uchafu tatizo sio rangi tatizo ni fikra zetu waafrika
 
Back
Top Bottom