Magunia 58 na hekari 31 za bangi vyateketezwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Polisi Mkoani Arusha kwa kushirikiana na tume ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya, limeendesha oparesheni siku mbili kijiji cha Kisimiri Juu na Engalaon, Wilayani Arumeru na kukamata magunia 58 ya bangi, kilo 210 bangi na hekari 31.

Akizungumza leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema, magunia hayo na mbegu hizo, zilikamatwa katika oparesheni iliyofanyika kwa siku mbili Januari 10 na 12 mwaka huu, katika kijiji cha Kisimiri Juu, Wilayani Arumeru.

Amesema Januari 10 walivyofanya oparesheni hiyo saa 11:00 alfajiri katika kijiji hicho, Kata ya Uwiro, Tarafa ya King’ori walifanikiwa kukamata magunia hayo 31 ya bangi, mbegu kilo 210 na hekari 19 zilizooteshwa miche ya bangi ambavyo vyote vimeteketezwa kwa moto.

Mkumbo amesema Oparesheni hiyo iliendelea Januari 12 mwaka huu, kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 7:00 mchana katika maeneo ya kijiji cha Engalaon Kata ya Mwandet Tarafa ya Muklati, ambapo magunia 27 ya bangi yalipatikana na hekari 12 zilizooteshwa mimea ya bangi viliteketezwa.

Amesema jeshi hilo litaendelea kufanya oparesheni ya mara kwa mara na kuharibu mimea hiyo na hasa katika kipindi hiki cha mvua, ili kudhibiti kilimo hicho.

Aidha ameonya viongozi wa maeneo yanayohusika na kilimo cha bangi, kuacha mara moja na watu wasiunge mkono ulimaji wa zao hilo na vema watu wakatambua kila mmoja ana wajibu wa kushirikiana na jeshi hilo kutokomeza zao hilo ambalo linaleta madhara makubwa kwa jamii.

Chanzo: EATV
 
Mbona madawa ya kulevya yakikamatwa huwa hayachomwi moto ..huwa yanapekekwa wapi??

Maana nyavu,bangi zikikamatwa huchomwa moto watu tukishuhudia

Ila madawa hayachomwi na hatutangaziwi kama yanachomwa

Natamani kujua huwa yanahifadhiwa wapi
 
Hizi nguvu wakizielekeza kwenye unga nitawaona wa maana zaidi
 
Tanzania bwana ukikutwa na bangi shambani kwako kosa unafungwa na kufungwa dhahabu ikipatikana shambani kwako Mali ya serikali
 
Back
Top Bottom