Magufuri haya ya Kivuko cha Kigamboni hayakubaliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuri haya ya Kivuko cha Kigamboni hayakubaliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwalufunamba, Sep 26, 2012.

 1. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna "madudu" mengi yanayofanywa na wafanyakazi wa vivuko vya M.V. KIGAMBONI na M.V. MAGOGONI kama haitoshi hata wale wakatisha tiketi ambao wamepata ajira kwa misingi ya ujuani.

  Nalotaka kukazia kwasasa ni hili, pamoja na wakala wako/yako kukusanya mamilioni ya shilingi kwa siku bado hamtujali wananchi na kutufanya tukae kwenye giza.

  Haikubaliki jumba la kupumzika abiria wa miguu lenye holder za fluorescent tube light 28, zinazowaka ni 5; hii ni upande wa Magogoni. Ukienda upande wa Kigamboni kuna holder 16 zinawaka 3. Huu ni upuuzi wa hali ya juu hata tunapovumilia mwataka kutuona wajinga.

  Kwani nayo mtasema milioni moja itakwisha katika manunuzi ya taa tu?

  Toka ofisi uje kuona ni kilichopo usiishie kubakia kusema mia mbili wamekubali na ubavu wa kupiga mbizi hawana.
   
 2. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ukiachilia mbali suala hlo pia kuna muda mwingine unafika kivukoni unaweza kukaa zaidi ya nusu saa hujavuka na sababu wanazo wao wananch hatuzijui.hii inaboa sana hasa pale km una mambo muhimu yanakufanya utake kuwahi.jirekebisheni mia mbili co ndogo hizo.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mwenzako ashakuambia kama vipi piga mbizi maana hutakuwa na sababu ya kulipia pale getini tz govt is already dead..
   
 4. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Labda daraja litapunguza kero hizo.
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  NSSF ishafirisika haiwezi kujenga daraja.solution ni kung'oa uongozi mzima wa Kivuko
   
 6. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Utamu wa ngoma ingia ucheze, kama vyeti vinaruhusu nipatie vyeti nikupe ajira kisha nitakupanga kwenye hicho kitengo chenye mapungufu tuone utafanya nini,
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Nadhani umefilisika (siyo firisika) wewe usiyejua ni kitu gani kinaendelea nchini hapa.

  Pole sana.
   
 8. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Thanks for the point of correction hahahaha na kiswahili nacho ni wito ndugu yangu
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du mTZ hata hilo daraja la Kigamboni likipaika au akijisaidia mtu atatafutwa Maguduli
  Jamani ku-repair taa tu Serikalini siku hizi mpaka kila Supply anunue kitabu cha Electricity & Maintanance ktk Tender Board na sio chini ya 50,000 ktk kitengo cha Procurement & Supply huko Bohari Kuu ya Serikali sasa leo wasafiri au Raia wameiba au kuungua na idadi imeisha store Magufuli hahusiki.
  Kwenye Halmashauri tu ukihamsha Road fund Magfuli akisikia Out
  Imefikia kipindi sasa tulunde wenyewe au tuchomane
   
 10. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ukwaju, kama hakuna mzabuni wa kupeleka taa, wanaruhusiwa kununua vitu kwa fedha taslimu.
  Tatizo hilo lipo zaidi ya miezi miwili, mzabuni gani huyu anayeshindwa kununua taa kwa muda wote huo?
   
Loading...