MAGUFULISM: Falsafa ya Magufuli kwenye Siasa, Uchumi N.k

Sitaki kuwa MNAFIKI, kwangu Mimi Hayati Magufuli alikuwa na Sifa zifuatazo;

1. Mtu aliye nyang'anya TUNU ya UHAI ambayo Mwanadamu alipewa na MUNGU.

2. Mtu aliyekuwa na Kiburi na Jeuri.

3. Mtu mwenye UPEO Mdogo wa Kudadavua mambo, hasa ya Dunia ya Sasa.

4. Mtu mwenye wivu na husda na maendeleo ya MTU/WATU.

5. Mtu aliyetakiwa kuongoza zaidi ya Miaka 100 iliyopita hususani kwenye mambo ya Haki na Uhuru.

Samahani kwa wale ambao watakwazwa na mtazamo wangu.
Hizi ni sifa za mbowe
 
Isome vizuri historia ya dunia ilipotoka na ilipofika, jitahidi pia kutembea na kujionea maendeleo ya dunia sehemu mbalimbali..

Mzee wetu hakuwa na jipya, aliwaza kizamani karne ya 21 na hapo ndio tatizo lilipoanzia na kutofutiana na watu.....Alikuwa anajaribu kulazimisha watu na dunia iishi anavyofikiri yeye akiamini ana akili nyingi sana kumbe wenzie wanamuona ana fikra za kizamani....
 
Umeandika kitu ambacho niliwahi kuandika hapa pia. Shujaa alikuwa na NIA NJEMA kabisa ya kutaka Tanzania ipige hatua mbele, ila tatizo hakuwa KIONGOZI mwenye MAONO na alipo pata MAONO hakuwa na namna nzuri ya kuyafikia maono yake.

Sehemu alivyo-fail Shujaa ni 'how to execute' mipango ili kutimiza maono! Aliamini katika 'YEYE' kuliko katika 'SISI', aliona wengine wote hawana uwezo wa kutimiza mambo isipokuwa yeye tu na ndiyo maana alikuwa mtoa AMRI wa kufanyika jambo siyo mtu wa MSHAURIANO.

Shujaa alipaswa kuwa MTEKELEZAJI wa maelekezo ya KIONGOZI siyo MTOA MAELEKEZO ya kutekeleza.
 
Magufulism ni falsafa inayoamini kuminya vyombo vya habari,vyama vya siasa na asasi za kiraia ikiamini kufanya hayo ni kushinda uchaguzi.

Inapojikuta ni total mess n failure Magufulism inabadilika sasa na kuelekeza wizi wa kura wazi wazi.
 
Magufuli na Elimu...
Magufuli na Afya...hapa amejenga Vituo vya huduma za afya zaidi ya 400
Hospitali ya Uhuru
Kujenga vituo vya afya 400 bila kupeleka dawa na wataalamu ni matumizi mabaya ya fedha.
 
MAGUFULISM
Hii ni aina mpya ya Falsafa iliyoanzishwa katika Karne ya 21 haswa mwaka 2021 kutokana na falsafa za aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliyeishi kati ya 1959-2021. Katika Falsafa ya Magufulism tutaangazia mitizamo ya mwanafalsafa huyu katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii, Kidini, Kiutamaduni, Kielimu na Kisayansi. Falsafa hii imeandikwa na kubuniwa na Josias Charles, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika Elimu ya Saikolojia ya Watoto na mbobezi katika Historia kwa Ujumla.

MAGUFULIST
Hawa ni watu wote wanaoamini , wanaoishi na kuenenda katika falsafa ya Magufulism. Magufulist siku zote wanaamini kuwa maendeleo ya Taifa ama mtu binafsi yanatokana na kulinda raslimali tulizo nazo kwa nguvu zote na Kufanya kazi kwa uadilifu bila kutegemea misaada kutoka nje.

Hapa chini tutaichanganua falsafa ya MAGUFULISM katika nyanja mbalimbali ambapo tutaangalia Dr. John Pombe Magufuli alikuwa na mitizamo na falsafa gani kuhusu mambo mbalimbali:

MAGUFULI NA UCHUMI:
Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliamini uchumi imara hutengenezwa kwa kutumia raslimali zilizotuzunguka kwa uaminfu na uadilifu. Dr, Magufuli aliamini pia kuwa endapo kila mmoja akitimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi kwa uaminifu basi uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ungeimalika sana. Dr. Magufuli alipinga uwekezaji wenye masharti ya Unyonyaji kutoka kwa mataifa ya Nje hususani katika Sekta ya Madini, Bandari nk.

MAGUFULI NA SIASA:
Katika upande wa Siasa Dr. Magufuli aliamini katika uwepo wa Vyama vya siasa vyenye mlengo wa kuleta ushindani wa hoja na sio vyama vinavyotumiwa na mataifa ya Kigeni kutaka kuvuruga amani na mshikamano wa Taifa. Dr Magufuli alividhibiti kwa nguvu kubwa vyama vilivyokuwa vikitumiwa na mataifa ya Kigeni kupenyeza agenda za mataifa ya kigeni. Katika Upande mwingine Dr. Magufuli aliamini kuwa Maendeleo hayana chama. Katika kuonyesha kuwa maendeleo hayana chama , Dr. Magufuli aliwateua viongozi wengi wa Vyama vya Upinzani katika nyadhifa tofauti tofauti katika Serikali yake.

MAGUFULI NA JAMII
Dr. John Pombe Magufuli aliamini katika ustawi wa jamii na kupinga aina zote za unyanyasaji toka kwa watu wenye madaraka na matajiri. Katika kipindi chake cha uongozi ndipo jina "WANYONGE" lilipata umaarufu. Wananchi walipoona Msafara wa Dr. Magufuli waliukimbilia na kuona mtetezi wao amefika, naye Dr. Magufuli aliwapa nafasi ya Kuwasikiliza.

MAGUFULI NA DINI
Dr. Magufuli aliamini kuwa tunamuamini Mungu mmoja hivyo alihimiza usawa, upendo na mshikamano kati ya watu wa madhehebu yote. Alichangisha fedha za Kujenga Misikiti katika makanisa mbalimbali, na pia pesa za kujenga Makanisa kutoka misikiti mbalimbali. Dr. John Pombe Magufuli aliamini kuwa hakuna jambo linaloshindikana mbele za Mungu. Hata katika kipindi ambacho Dunia ilikuwa ikihangaika na janga la Corona Dr Magufuli alichukua msimamo tofauti na mataifa mengine, aliwahimiza watanzania kumuomba Mungu maana yeye hashindwi na jambo lolote lile.

MAGUFULI NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA
Dr John Pombe Magufuli aliamini katika ushirikiano usio na chembe za unyonyaji kati ya Taifa lake na mataifa ya Kigeni. Dr Magufuli allikuwa tayari kusitisha uhusiano na Taifa lolote ama taasisi yoyote yenye lengo la kufanya unyonyaji kwa Taifa lake. Kwa Lugha rahisi Dr Magufuli hakuwa muumini wa Kujipendekeza kwa Taifa tajiri ama Taasisi za Kimataifa kwani aliona kuwa watu wote ni sawa hivyo hakuna sababu ya kuwanyenyekea wanyonyaji kutoka katika mataifa ya Kigeni.

MAGUFULI NA RUSHWA/UFISADI
Dr. Magufuli alichukia Rushwa na Ufisadi kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa tayari kuvunja urafiki na mtu yeyote aliyetetea ama kufanya vitendo vya rushwa. Katika Kipindi chake cha Uongozi neno "KUTUMBUA MAJIPU" lilimaanisha kuondoa viongozi wote wasio waadilifu na kuwachukulia hatua.

Hii ni sehemu ndogo kati ya Historia ndefu na ya kusisimua kuhusu Kiongozi na mwana falsafa huyu aliyeishi katika Karne ya 21.

Josias Charles
Mtazidi kuweweseka sana
 
Pole sana maana kwa sasa tupo na mama yetu Samia.
 
Sitaki kuwa MNAFIKI, kwangu Mimi Hayati Magufuli alikuwa na Sifa zifuatazo;

1. Mtu aliye nyang'anya TUNU ya UHAI ambayo Mwanadamu alipewa na MUNGU.

2. Mtu aliyekuwa na Kiburi na Jeuri.

3. Mtu mwenye UPEO Mdogo wa Kudadavua mambo, hasa ya Dunia ya Sasa.

4. Mtu mwenye wivu na husda na maendeleo ya MTU/WATU.

5. Mtu aliyetakiwa kuongoza zaidi ya Miaka 100 iliyopita hususani kwenye mambo ya Haki na Uhuru.

Samahani kwa wale ambao watakwazwa na mtazamo wangu.
Mkuu mi naunga hoja kwa kishindo
 
Back
Top Bottom