Magufulism and Nationalist People Party kupambana 2025

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
Je, wajua kuwa kifo kimeshindwa kuwatenganisha watanzania na Magufuli ?

Je, wajua kuwa umagufuli ni maisha kwa wanyonge wa taifa hili?

Je, wajua nguvu ya moyo ndio huamua nani awe rais kwa taifa hili kwa idadi ya watu?

Je, wajua kuwa mawazo na maisha ya umagufuli ndio yameijenga nchi kwa kipindi kidogo na kufanya makubwa?

SIKILIZA

Watu wenye ushawishi ndani ya CCM ambao kwa sasa wanajipambanua kama wafuasi wa sera za John Pombe Magufuli wamekutana hiyo jana na kuambua kuja na chama kipya cha kupambana na CCM ya samia na kuchukua nchi kwenye Uchaguzi ujao 2025.

Kutoka ndani ya CCM, Serikali, mtaani na ndani ya taasisi nyeti ni kuwa mwamko ni mkubwa na sasa wameamua hakuna wa kuwarudisha nyuma uwezo mkubwa wa waasisi kutoka ndani na nje ya nchi kutunisha mfuko na kuasaini kujiunga sasa ni rasma chama chenye nguvu kinakuja.

Chama hiki kinakwenda kuwakomboa Watanzania juu ya kinachoitwa kutelekezwa kwa miongozo ya Serikali ya John Pombe Magufuli ambaye alikuwa pacha wa Samia

Wizi, Ufisadi, Uzembe, Madawa ya Kulevya vimerejea kwa kasi bila chama hiki nchi itapotea.

Jiandae

USSR
 
images (13).jpeg
Sasa hicho chama kwa mtu kama huyu ndio mtetezi wa wanyonge?

Anatetea nini hapo!? Wanyonge ni akina nani hebu tupe mifano halisi!
 
Heri waanzishe tu, maake huku tunakoelekea hata hakueleweki. Nchi haiwezi endeshwa kwa kubembelezana. Nchi haiwezi endeshwa kwa hisia za mitandaoni. Si kila neno tamu ujenga. Si kila malezi ya kudekeza watoto uwafanya watoto wakue kwa maadili mema.
Imefikia wakati watanzania tubadilike. Ili nchi yetu ipige hatua kimaendeleo. Na hii si kazi rahisi, inahitaji kujitoa na zaidi kuwa na uzalendo. Tunahitaji damu mpya yenye lengo la kuisimamia nchi, na hasa kujali watu wa hali ya chini kimaisha, na kuwawezesha wenye uwezo ili wasiteteleke ili kukuza uchumi wa ndani.

Kuna baadhi ya watu ndani ya CCM wanadhani wana hati miliki ya hii nchi. Wengine kwakua wazazi wao walikuwa na vyeo basi wanaona na wao wanafaa. Kwanini tuendelee kuwa wale wale tulivyokuwa miaka ya nyuma. Kwanini tusipige hatua, na kuleta vijana na wazee wenye maono mapya kwa ajili ya nchi yetu. Kwanini twendelee kuishi katika umasikini miaka yote, hadi leo tunaanza kuona nchi kama Kenya ati ni waungwana zaidi yetu.
Kwanini tusiwe na wivu wa kimaendeleo? Tanzania tukiamua tunaweza. Na tunao watu safi katika hii nchi kutufikisha tunapotaka kufika. Magufuli alionesha njia. leo hii tusivurugwe na wachache kisa kuogopa kutukanwa na kuzomewa. Tanzania inahitaji mabadiliko. Hatuchagui viongozi ili wale raha, na kutanua maisha wakati watu wa hali ya chini wakiumia. Viva Tanzania Viva! Viva maendeleo Viva!
 
Wanatamani reli, ndege, mabarabara, mahospitali wayafunge lakini haiwezekani

Magufuli aliwagaragaza akiwa Hai na atawagaragaza akiwa mauti.
sidhan kama kuna mtu anataka kuyafunga maendeleo. huyo mtu atakuwa anatatizo mahali
 
Heri waanzishe tu, maake huku tunakoelekea hata hakueleweki. Nchi haiwezi endeshwa kwa kubembelezana. Nchi haiwezi endeshwa kwa hisia za mitandaoni. Si kila neno tamu ujenga. Si kila malezi ya kudekeza watoto uwafanya watoto wakue kwa maadili mema.
Imefikia wakati watanzania tubadilike. Ili nchi yetu ipige hatua kimaendeleo. Na hii si kazi rahisi, inahitaji kujitoa na zaidi kuwa na uzalendo. Tunahitaji damu mpya yenye lengo la kuisimamia nchi, na hasa kujali watu wa hali ya chini kimaisha, na kuwawezesha wenye uwezo ili wasiteteleke ili kukuza uchumi wa ndani.

Kuna baadhi ya watu ndani ya CCM wanadhani wana hati miliki ya hii nchi. Wengine kwakua wazazi wao walikuwa na vyeo basi wanaona na wao wanafaa. Kwanini tuendelee kuwa wale wale tulivyokuwa miaka ya nyuma. Kwanini tusipige hatua, na kuleta vijana na wazee wenye maono mapya kwa ajili ya nchi yetu. Kwanini twendelee kuishi katika umasikini miaka yote, hadi leo tunaanza kuona nchi kama Kenya ati ni waungwana zaidi yetu.
Kwanini tusiwe na wivu wa kimaendeleo? Tanzania tukiamua tunaweza. Na tunao watu safi katika hii nchi kutufikisha tunapotaka kufika. Magufuli alionesha njia. leo hii tusivurugwe na wachache kisa kuogopa kutukanwa na kuzomewa. Tanzania inahitaji mabadiliko. Hatuchagui viongozi ili wale raha, na kutanua maisha wakati watu wa hali ya chini wakiumia. Viva Tanzania Viva! Viva maendeleo Viva!
Upeo wako ni mdogo. Ungekuwa na uelewa ungejua maendeleo ya nchi yetu yalidumazwa kwa kiwango gani na marehemu.

Kwa miaka 5 wastani wa pato la Mtanzania liliongezeka kwa dola 80 tu. Wakati wa Kikwete liliongezeka kwa dola 400. Wakati wa Mkapa kwa dola 380. Lakini wajinga, misukule ya marehemu wanaamini dikteta Magufuli aliupaisha uchumi wla Tanzania.

Ni aheri unyimwe vyote kuliko akili. Watu wote wanaomsifia marehemu, ukiwachunguza, ni watu wenye akili ndogo.
 
Upo sahihi mkuu, hata ukose makalio, utakalia pamba, lakini akili haina mbadala!
 
Safi sana. Sasa ndio mtaona inauma kiasi gani kukubaliwa na wananchi alafu tume inawakataa na kumtangaza mwingine.

Ujue malipo huwa hapa hapa duniani. Nitaomba sana kuwa hai siku hii kitu ikiwa kweli nishuhudie.
 
Back
Top Bottom