"Magufulifications" of Africa

Ni rais gani wa africa ambaye aliwahi kuheshimu!? Any way tuachane na Africa, Tanzania, ni rais gani ambaye aliheshimu sheria na jee! Tulimuunga mkono vya kutosha? Nakumbuka Kikwete aliitwa dhaifu kutokana na kila aliposhinikizwa kushughulikia watu alikuwa akisisitiza sheria ziheshimiwe na kuepuka kuingilia mamlaka nyingine. Sasa kama wale wale waliomlaumu kikwete kwa mfano, ndio hao hao wanaomlaumu Magufuli, hapo unaweza kusema nini?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno

..mimi naomba unishawishi kwanini in 21st century Afrika nzima inahitaji Maraisi wasioheshimu katiba na sheria.

..kwa maoni yangu ni hatari sana kwa mataifa yetu kuwa na watawala wasioheshimu sheria, wasiotenda haki, wenye double standards, wasioheshimu wengine haswa wenye mawazo mbadala.
 
Ni MAZWAZWA tu Mkuu ndiyo ambao wanaweza kuwa na mtazamo huo wa kutaka Africa iwe na madikteta uchwara kama bwana yule.

..kwa mtizamo wangu, hotuba za Prof.Lumumba ziko kizamani-zamani mno.

..Magufuli haheshimu katiba na sheria za nchi hii, sasa Prof.Lumumba anataka Afrika nzima iwe na maraisi wa aina hiyo?
 
"Africa should be Magufulified"

Mmoja wa wasomi wa kubwa na wanaotambulika kama wazalendo na wanaopigania mabadiliko Africa kwa zama hizi, ni Prof. P.L.O lumumba.

Binafsi, Prof. Lumumba ameanza kunii inspire tangu nikiwa chuo kikuu cha Dar es salaam miaka ya 2010 kutokana na hotuba zake za kusisimua ambazo wakati wote zimekuwa zikilenga kuwakosoa viongozi wa kiafrka kutokana na ufisadi, udikteta, uhujumu uchumi, uhujumu wa demokrasia, kutokufikiri sawa sawa n.k. Kwa wale ambao tumekuwa tukimfuatilia Prof. Tunaweza kukubaliana kuwa falsafa ya Lumumba ni kwamba umasikini na matatizo ya Afrika kwa kiwango kikubwa yameletwa na viongozi wasio na maono.

Sasa Prof. Baada ya kumfuatilia Rais Magufuli: kwenye hotuba zake nyingi anasisitiza "Africa should be Magufulified".

Prof.Lumumba si mtanzania, na anayasema haya. Nafikiri ni vyema tukatafakari kwamba ni kwa nini baada ya kuwaponda viongozi wa afrika kwa kipindi kirefu sasa anayasema haya kipindi hiki. Inawezekana kuna kitu muhimu na kizuri kinaonekana ila walioko ndani hawakioni.

Ujue mtu akiwa na neema anaweza asijijue isipokuwa walio pembeni ndio wakaiona, yule aliyenayo atakuja kubaini kuwa alikuwa nayo ikishaondoka.Mahitaji ya binadamu ni very complicated na wakati mwingine yana confuse sana. Mfano mtu anaweza kulaani joto kali la dar ila akisafiri kwenda mbeya akalaani baridi la kule.

Ninawaza tu hapa! ? Pengine ingekuwa ni kushauri, ningeshauri tumuangalie Rais Magufuli kwa jicho positive na tutaona fursa nyingi ambazo tunaweza kuzitumia na kuboresha hali yetu ya maisha.Tujaribu kuangalia mambo kwa jicho positive ili tuweze kusonga mbele kulingana na hali zetu na changamoto mbali mbali tulizo nazo.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno

Ushauri mzuri, isipokuwa lile Neno "Nabii hakosi kupata heshima isipokuwa kwao", gumu sana. Inasemekana wanakijiji wa Butiama walitambua kuwa Mwalimu alikuwa mtu mkubwa sana duniani siku alipozikwa kijijini hapo. Hawakuamini macho yao ule ugeni uliofika pale na kuendelea kufika kwa muda mrefu kuhani msiba wa mwanakijiji mwenzao.
 
Afrika bado tuko vitani, huwezi kuwa vitani tukawa tunajiuliza hivi hapa tunafuata haki za kibinadamu au la. Afrika hatujafikia muda wa kupumzika na kufuata mstari. Hata nchi zilizoendelea zilikuwa na crazy time walizopitia mpaka wakafika hapo walipofika.

..ukiniambia hiki kinachoendelea ni "transition" period kwamba eventually tutafika mahali pazuri unanipa matumaini kidogo.

..naweza nikakupa the benefit of doubt.

..lakini mtoa mada anasema kitu tofauti. Anapendekeza tutawaliwe kikatili, kidikteta.
 
..mimi naomba unishawishi kwanini in 21st century Afrika nzima inahitaji Maraisi wasioheshimu katiba na sheria.

..kwa maoni yangu ni hatari sana kwa mataifa yetu kuwa na watawala wasioheshimu sheria, wasiotenda haki, wenye double standards, wasioheshimu wengine haswa wenye mawazo mbadala.
Kwa sababu bado kuna idadi kubwa ya watu wasiojitambua na wanafiki, ambao ukikaa watakulaumu, ukisimaa watapiga yowe, ukitembea watalia, ukilala watakutukana na kukukanyaga.

By the way sisemi katiba inatakiwa ivunjwe lakini ninachozungumzia ni ama ukali au upole.

Kwa mfano isgu ya makinikia, imekuwepo toka kitambo ila Rais Magufuli kaishughulikia kwa namna ya kipekee, unaweza kusema nini kuhusu hilo?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Mkuu betlehem, hebu rudisha ile avatar yako ambayo macho yamekutoka kama fundi saa, maana nilizoea kuwatania watu huku mtaani "utatoa macho kama betlehem wa JF" huo utani sasa hivi unakuwa ni irrelevant.
 
Only time will tell. Mugabe started very well. Look where Zimbabwe is now.

Too early to be judging Magufuli. In my humble opinion, all indications are pointing to an intolerant leader. Very bad for democracy. We need to build institutions and not personalities.

Again, Prof. Lumumba may come to regret his words in five to ten years!

I wish I will be proved wrong.
 
Ni MAZWAZWA tu Mkuu ndiyo ambao wanaweza kuwa na mtazamo huo wa kutaka Africa iwe na madikteta uchwara kama bwana yule.
Ila mkuu chadema ambao walikuea wanamponda sana kikwete, ndio waliokuwa wametuambia na kutusisitiza kuwa tanzania ilikofikia inahitaji rais dikteta.Sasa ikiwa Magufuli ni dikteta kweli, huoni hatimae maombi na ushauri wao utakuwa umekubaliwa! Au unataka kutuambia chadema walikuwa mazwazwa kama unavyodai?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
..ukiniambia hiki kinachoendelea ni "transition" period kwamba eventually tutafika mahali pazuri unanipa matumaini kidogo.

..naweza nikakupa the benefit of doubt.

..lakini mtoa mada anasema kitu tofauti. Anapendekeza tutawaliwe kikatili, kidikteta.
Mkuu, unanibambikizia maneno, sijasema unayosema nimesema.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Only time will tell. Mugabe started very well. Look where Zimbabwe is now.

Too early to be judging Magufuli. In my humble opinion, all indications are pointing to an intolerant leader. Very bad for democracy. We need to build institutions and not personalities.

Again, Prof. Lumumba may come to regret his words in five to ten years!

I wish I will be proved wrong.
Lakini unaposema istitutions, tayari tunazo mbona, au unataka tufanye je tena, au institution gani ambayo hatuna?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Alaaniwe yoyote anayedumaza demokrasia, nasema hivyo kwakuwa katika watu wanaotekeleza demokrasia kwa vitendo ni wewe bwana Betlehem. Leo hii unatuambia tena kwa kumtumia msomi Nguli Prof. Lumumba kwamba ameona kitu cha maana sana hapa nchini mwetu lakini sisi ndio hatuoni. Ila nikikumbuka kwa jinsi ulivyokuwa unamtetea rais wa awamu aliyopita na huku ukitushangaa sisi tusiomuelewa ilikuwa inaleta raha kidogo. Leo hii kaingia rais wa awamu ya tano na wewe unacheza mziki huo huo wa kwamba hajawahi kutokea kama huyu na unashangaa kwanini bado watu wanalalamika au kukosoa. Sasa kama huyu anasema nchi hii ilikuwa imeoza na majizi yalikuwa mengi, iweje wakati ule ulikuwa huoni na kutushangaa kwamba hatujui ubora wa rais wa awamu ile.

Tuje kwenye hii unayoita Magulification kama unavyosema kutoka kwa msomi nguli Prof. Lumumba. Ili kiongozi awe bora kwanza ni kupima faida wanazozipata wananchi wake kiuchumi au kwa maneno marahisi ubora wa maisha yao na wala sio hofu waliyo nayo kwa kiongozi wao. Ukiangalia kwa sasa tofauti kubwa sana ya maisha ya wananchi kwenye nchi hii sio ubora wa maisha yao ulioletwa na kiongozi huyu bali ni hofu waliyo nayo wananchi dhidi yake. Kwa hiyo wewwe na prof Lumumba mnafurahia hofu waliyonayo wananchi wake kwa kiongozi wao na sio maisha bora waliyo nayo wananchi wa nchi hii. Labda nijikite kwenye wananchi walio wengi kama sio kwa takwimu za kupima wengi ni wakulima. Unaweza kutaja mabadiliko ya dhahiri ama nikipeda kutumia neno mapinduzi ya kilimo uliyoona mpaka sasa? Ukiniambia msukumo halisi katika kundi hili kubwa na wananchi naweza kuelewa hicho unachosifia. Vinginevyo yeye ni wa kawaida sana lakini sasa ndio muda wake wa kutamba na nyie mnatafuta nyimbo za wakati wake tu. Halafu kama ulivyosema kila mtu ana uimara na udhaifu wake, hivyo usiogope kuna watu watatokea watasifia uimara wake kama nyie, na wengine kama sisi tutatokea tutakosoaudhaifu wake. Kamwe haitatokea wote wasifie kila kitu, wala haitatokea wote tukosoe kila kitu.
 
Lakini unaposema istitutions, tayari tunazo mbona, au unataka tufanye je tena, au institution gani ambayo hatuna?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Sasa Kuna katabia ka kuwa juu ya Institutions. Tumeanza kuwasikiliza zaidi viongozi ambao hawazipi sana nafasi taasisi kufanya kazi zake.
Wengine waliotumbuliwa wamerudishwa kimya kimya au bado wanavuta mishahara bila kazi. Tunaokoa pesa au tunafuja?
 
Hata mie wakati fulani baada ya kuangalia jinsi vile tulivyo, nashawishika kukubaliana na wewe

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Mkuu, ukifuatili historia za nchi ambazo leo tunazionea wivu, utakuta kuna wakati walipitia maamuzi magumu. Marekani kuna kipindi walipambana sana na mafisadi na ma mafia ambo walikuwa wanaficha hela na hawataki kulipa kodi. Ilikuwa vita vya risasi na kuuwana kati ya ma-mafia na viongozi wa kodi na FBI. Urusi hivyo hivyo wakati wa Lenin, kuna watu walipoteza maisha lakini ndio wakati urusi ilingia kwenye uchumi wa viwanda. Ufaransa nao walipambana Napoleon war. Uingereza na vita ya kutawala dunia kiviwanda na kibiashara. kwingine kote South Africa, Egypt, China nk. Kifupi wakati unaleta ajenda ya maendelo lazima utawakwaza watu fulani (ambao wako tayari kutoa roho ya mtu) ili mitandao yao iendele. Sisemi kama maendelo yanaletwa na mtu mmoja, au mtu huyo mmoja ni malaika, lakini sisi kama wananchi inabidi tujuwe kipi ni maendelo na kipi ni bla bla.
 
..kwa mtizamo wangu, hotuba za Prof.Lumumba ziko kizamani-zamani mno.

..Magufuli haheshimu katiba na sheria za nchi hii, sasa Prof.Lumumba anataka Afrika nzima iwe na maraisi wa aina hiyo?
Acha uongo wewe mtu
 
Back
Top Bottom