Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
--- Kama umasikini ndio chanzo cha kupata mimba kwa wanafunzi wa kike, kwanini shule nzima wasiwe na mimba? Kama umbali wote wanatoka mbali na wanaishi katika mazingira yanayofanana.
--- Eti wanadai ni haki ya mtu kupata elimu kwa maana kuwa na elimu ndio silaha ya kwanza ya kupambana na umasikini. Hiyo ni sawa. Lakini haki ni lazima iendane na wajibu (to get your Rights you should behave responsibly)
--- Wengine wanadai eti serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa maadili mabovu kwa maana wao ndio wametufikisha hapa kwa miaka 50 ya utawala wao. Ninasema hapana. Serikali haiwezi kuja nyumbani kwako ikakwambia baba na mama flani sasa zimeni TV ili mtoto wenu aache kuangalia cartoons afanye homework yake. Huo ni mfano tu juu gani ya wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao katika maadili ya watoto.
Huku uswahilini ninapokaa sio jambo la kushangaza kukutana na mtoto wa kike darasa hata la 3 usiku wa 4 eti ametoka kwende kibanda kuangalia movie. Hivi binti kama huyu akibakwa na kupata mimba (achilia mbali magonjwa mengine) italaumiwa serikali? Let's be serious guys.
JPM stay focused. Wewe ni mzazi unayejitambua sana.
Mwenye macho na asome.
Nimemaliza.