Magufuli; Wavuja jasho wanaopambana kulisha familia zao na kulipa kodi kwa serikali wanastahili heshima kuliko hata cheo cha Raia!

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,156
2,000
Kiburi, maringo na ubabe wa watawala wa kisiasa vinatokana na uwepo wa wafanyakazi na walipakodi. Covid_19 iliwafanya watu wengi wafunge biashara na kukaa nyumbani! Uchumi ukayumba, Watawala wakaanza kubabaika.

Ni lini wafanyakazi na walipakodi wataijua thamani yao?

Wavuja jasho wanaopambana kulisha familia zao na kulipa kodi kwa serikali - wanastahili heshima kuliko mtu yeyote katika nchi.

Bahati mbaya vyombo vya inteljensia duniani kote hupokea maagizo kutoka kwa watawala, na kupeleka taarifa za utekelezaji kwa watawala. Sheria huwekwa kuvibana vyombo hivyo.

Kwahiyo ikitokea katika nchi watawala ni wabovu - mambo huwa shaghalabaghala!

Mr mkiki.
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,142
2,000
Huo ni mpasho kwa rais magufuli au statement ya rais magufuli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom