Magufuli: Watanzania wamekata tamaa

Apr 27, 2006
26,588
10,375
John Magufuli, amesema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta mabadiliko ya kweli. Amesema pamoja na hali hiyo, anatambua namna wananchi walivyokata tamaa ikiwamo kushindwa kubadili maisha yao, kutokana na ubinafsi wa watu wachache ambao wameamua kujimilikisha rasilimali za nchi.


"Ninajua Watanzania wanataka mabadiliko ambayo ni M4C yaani ‘Magufuli for Change' na kwa lugha ya kawaida ni Magufuli kwa mabadiliko tena ya kweli," alisema Dk. Magufuli.

Akizungumza namna atakavyoubadili mji wa Iringa, alisema anajua changamoto zilizopo katika mkoa huo, ikiwamo kero ya barabara hasa za ndani.
"Ninawashangaa watu wanasema eti CCM haijafanya kitu na wengine ni hapa hapa Iringa mjini tena mchungaji wa kondoo wa Mungu ambaye anazijua amri kumi za Mungu ikiwemo ya kutosema uongo.

"Tena amekuwa akitukana ovyo ndani na nje ya Bunge nataka kuwaambia mawaziri nao ni binadamu wana nyongo…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM," alisema.

Alisema anahitaji ushindi wa asilimia 99 ili wapinzani waisome namba kupitia masanduku ya kura.

Mchagueni Magufuli haya yote ana weza
 
aishie zake.... kisa kutukanwa na mbunge wa upinzan hauwez kutoa hela ya maendeleo kwa wananch wake.... hapo anazid kujionyesha mbabe... wana mabadiliko hatumtaki
 
yaani miaka hiyo yote mpaka kupelekea wananchi kukata tamaa serikali ya watanzania ilikuwa inaongozwa na wapinzani? wananchi wa sasa hawadanganyiki labda wa Chalinze
 
Kitengo cha it Masaki kimeshindwa kazi kwa kweli naona umekuja babu kuokoa jahazi lililozama
teh teh

Le mabadilikoz
 
Na kweli tumekata tamaa, yeye ndio anajua leo.......chini ya utawala wa CCM alitegemea nini kama sio wananchi kukatishwa tamaa, maisha magumu, elimu duni, afya duni, maji safi shida, lishe bora shida.......kila kitu hovyo, namshukuru kwa kulitambua hilo na pia akubali tu kura tumpe LOWASA na yeye tumuombee nafasi ya UWAZIRI wa michezo maana naona hiyo sehemu anaiweza, japo push up zenyewe za kichovu.
 
Mambo anayosema yanapaswa kusemwa na Wapinzani, yeye anapaswa kusema tumefanya hivi........tuongeza hivi.......tulifanya hivi, tukapata changamoto hiii...........nitaanzia ........na kuendelea. Mabadiliko sio Sera ya CCM.

Umenichekesha!!Mungu ibariki Tanzania
 
“…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM,” alisema.
Mfumo wetu unamatatizo makubwa sana. Na Magufuli ana mpango wa kuulea.

Watu wanapenda wa nyenyekewe kama Zitto alivyo kuwa ana mnyenyea Kikwete wakati ni kodi yetu.
 
Mambo anayosema yanapaswa kusemwa na Wapinzani, yeye anapaswa kusema tumefanya hivi........tuongeza hivi.......tulifanya hivi, tukapata changamoto hiii...........nitaanzia ........na kuendelea. Mabadiliko sio Sera ya CCM.

Majina nayo pia yanamaana kubwa katika maisha yetu! Kwa mfano ukiitwa Delila ujue yatakukuta ta Delila! Ukiitwa Shida/matatizo ujue napo maisha yako yatakuwa hivyo hivyo! sasa huyu anaitwa Pombe na hata akiwa waziri mambo yake yako hivyo hivyo tu!

Aliwahi mwamasisha Kikwete aendelee kwenda Ulaya Kukopa!! Sasa huyu ndio Rais Mtarajiwa!
 
mabadiliko ya kweli yatatokana na katiba ya wanachi iliyochakachuliwa magufuli sijamsikia akigusia katiba kabisa hayo mabadiliko yatakuja vipi
 
Hivi katika vitu vyote tunavyohitaji Watanzania huyu Magufuli kwake anaona number 1 ni Mabarabara kwa vile kapatia umaarufu kupitia barabara basi kila mahali lazima atoe ahadi a za barabara na kuzungumzia issues around barabara.

Tanzanians need more than that the guy seems that he does not know some people do not even have food to eat. People are hungry not a JOKE!! He should rather focus on real issues; education, food production, sanitation and health!! Tumechoka kusikia kilometer za mabarabara na number ya madaraja makubwa na madogo yaliyojengwa kipindi cha Kikwete. Hayo mafanikio ya Kikwete twambie watanzania walau utatufanyia nini zaidi!!
 
Mapadlock binafsi hana shida! shida inakuja tu pale atakapochaguliwa hatakuwa rais wa watanzania coz yeye ni TV tu remote anayo JK na Mr.Ben. Yeye kama yeye hawezi kufanya lolote juu ya mustakabali wa taifa. Sasa kwenye hali kama hiyo tumpigie kura huyu!! wakati tunajua wazi atakuwa rais wa watu wachache na familia zao!!!?
Kama kuna domo lake hapa jf mwambieni kuwa sisi atuna matatizo naye bali ni hilo lichama lake na hiyo mifumo yake ya kinyonyaji.
 
Kwa miaka 20 (10 ya mkapa 10 ya huyu bongo movie)tumesota!!! Halafu unatushawishi kweli tumchague mtu anayefungana na haya madude yalituchosha hivi!???
Tunataka taifa limpate kiongozi ambaye anajiamini,hatofungamana na mifumo kandamizi na aliyeonyesha nia ya kutaka kuwa kiongozi wetu!
Kwa taarifa yako magufuli hakuwahi kuutaka uraisi wa nchi hii!! Kwa maana hiyo hajajiandaa kuwa kiongozi wa taifa hili lilopigwa mikasi kila penye tundu.
 
Back
Top Bottom