Magufuli washugulikie hao buda

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
Buda ina maana ya watu wabishi wasiopenda mamba hata yawe mazuri!!!!
Tanzania imekuwa na buda wengi wasiopenda ukweli na wasiopenda kufanya kazi!!!

Simaanishi ni wote no ila karibu 85% hawatimizi majukumu yako!
Ndo maana Watanzania wanaoishi nje ya Nchi wakirudi wanawashangaa watanzania wengi wanaopenda kukaa vibalazani muda wa kazi na kupiga story!!

Watanzania wanaoishi nje wamekumbana na changamoto nyingi ndo maana hata wakirudi nyumbani wanakuwa very smart!!
Niko na mfano wa mjomba wangu alienda UK miaka ya 1990 kusoma uko Manchester alisoma lakini baada ya kumaliza alikuwa akipambana na changamoto za uko!!!

Mfano baada ya kumaliza masomo alianza kazi kama secretary katika office moja mjini Manchester,ambapo alikuwa akilipa kodi lafiki zake wakamwambia uwezi fanikiwa UK kwa kazi moja no tafuta kazi nyingine
Akatafuta kazi ndani ya uwanja wa Manchester city (Etiad stadium) ya kulipwa kwa masaa alipewa kazi ya kufanya usafi uwanjani baada ya mechi

Lakini ujue wenzetu ambavyo hawana mchezo kwenye kodi walimkata hiyo pesa kodi ingawa alilipwa kwa masaa!!
Akuishia hapo alipata kazi ya tatu kwenye kampuni ya shoeshine kwenye air port ya Manchester kila siku asubuhi kabla aende ofisini alikuwa akishafisha vitu vya wateja wanaopanda ndege na alilipwa kwa masaa na pesa yake ilikatwa kodi !!!

Hivyo alikuwa na kazi tatu
Hivi hapa kwetu Tanzania kwanini tunazarau kazi??
Kazi ni kazi!!
Aliweza Fanya kazi UK kwa miaka 10 na amerudi nyumbani sasa anamiliki Chuo uko kigamboni!!
Amefanikiwa kimaisha kwa sababu ya mapambano!!
Ndo maana mnaiona UK inapendeza swala ni kodi hawana mchezo kwenye kodi !

Na watanzania wengi wanaoishi nje wakirudi wanakuwa very different hawana mzaha hata kidogo!!
So hakuna nchi iliyopata maendeleo bila kukisanya kodi!!!
Kodi lazima ipatikane kwa garama yeyote !!!

Watu wafanye kazi watimize wajibu wao kama amuwezi Fanya kazi tokeni nje ya nchi muone watu wanavyofanya kazi sio kukaa alafu unalalamika!!
Ndo maana namwambia magufuli wakamue hao buda""
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,021
2,000
Yaani hapo umenigusa. Mimi nakupia masaa 14-15 kwa siku Monday to Friday. On Saturday 10 hrs. Sundays niko free maamae. Kodi nayokatwa ni 36%. Inahitaj kweli uwe discipline na mvumiliv. Ila salary slip inapokuja unasahau uchov wote
 
Mkuu tafuta oungezee ili tukusanye kodi !!!
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
Hakuna asiyependa kulipa kodi kama zinatumiwa ipasavyo.

Tatizo wenye mamlaka wanazitumia vibaya. Sidhani kama kuna mtu atafurahia kulipakodi wakati zinaliwa na wajanja wachache.
Haaa mkuu lipa kwanza ndo utilize zimetumikaje!!! Kuoji bila kulipa uoni unakosea??
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,884
2,000
Ni kweli kabisa mtoa mada uko 100%.
Mimi pia ni mdau wa Diaspora na napiga kazi zaidi ya tatu kwa wiki na zote zinalipa kodi.

Ughaibuni Taxman na Manispaa wana uwezo w kisheria wa kuangalia akaunti yako kama una fedha zisizo halali na kama unaanza kuwazingua.
Ila tatizo la Tanzania ni mfumo wa ajira bado haujakaa sawa na hii ndio changamoto kubwa kwa JPM.

Chukulia mfano michezo ya Ndondo Cup, kama mimi nataka kuujenga vizuri uwanja wa Bandari na kuuweka kuwa wa kisasa.

Hivyo unaingia mkataba na Bandari halafu mnakula pamoja mapato.

Kisha najenga maduka mbalimbali na migahawa kuuzunguka huo uwanja, halafu naweka viingilio kwa watazamaji wa mechi za Ndondo Cup kulingana na uwezo wao.

Hivyo hio ndondo Cup inatengeneza ajira na kuboresha maisha ya wasela wa huko.

Hili suala la kula pamoja lipo hata Ulaya na ndio ajira nyingi ndogondogo zinaponea humo.

Ndio maana naunga sana hoja ya mheshimiwa Hapi ya kujaribu kuligeuza eneo la Uwanja wa Fisi kuwa la kisasa.

Idadi ya watu wasio na kazi Tanzania ni kubwa sana na nguvu kazi ipo ya vijana wengi wa Uwanja wa fisi, Tandale na Tandika mabatini.

Idadi hii ikiingia kwenye mfumo wa ajira Tanzania haitakuwa kama huko Ulaya lakini kutakuwa na afueni ya maisha kwa kila mtu

Ingawa kuna gharama- je vijana wangapi wamesoma angalau kozi za VETA?

Kama hawajasoma utawasaidia kusoma VETA, kwani watasoma wakiwa kazini hivyo wanaua ndege wawili kwa jiwe moja.

Watu hawawaelewi Makonda na mwenzie Hapi lakini hawa ndio vichwa vya kuaminiwa kubadilisha kasumba mbovu iliyopo ya kukaa na kungoja kulishwa kila kitu.
 
Asante changamoto ni nyingi sana huko Africa ila tatzo lipo pia kwa wajasiliamali kutozigeuza kazi zao wenyewe ziwe na mwonekana wa kueleweka yaani company hivi uzifanya kazi zao kutokopesheka!!!
Hivyo kupoteza furusa za kiuchumi kiukweli ulaya maisha ni magumu ila nirahisi sana!!!!
 
Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,142
2,000
Kwamfano Tamko la Makonda, ya namna ya kujua watu wa Jiji la Dar na shughuli wafanyazo ni jambo jema kwa mikakati ya maendeleo.
Lakini wanatokea wanasiasa na matamko ya kukatisha tamaa juhudi hizi, kwa kuwaambia Raia wagome ni hatari sana kwa ustawi nchi.

Kwani unapofahamu shughuli kuu za wananchi ni rahisi kuzirasimisha ili ziweze kuingia kwenye mfumo rasmi wa kulipa kodi eventually taifa kuongeza mapato na hivyo upatikanaji wa huduma za jamii kuwa wa uhakika.
Namalizia kwa kusema mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe.
 
Asante mkuu !! Nimelisema hilo swala kuwa hatawezi kupata mafanikio kama nchi hivi hivi lazima to sacrifice kwa muda
 
mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,450
2,000
Sawa. Ila kiswahili kinakupiga chenga kwelikweli! Mbona watu wanapiga kaxi ssna hapa bongo! Zunguka miji yote watu wamejaa msbarsbarani wanajitafutia riziki. Mamantile, bodaboda, machinga,. Huwaoni? Wabongo wanajitahidi sema uchumi mdogo hivyo wanachokipsta ni kidogo mno. Huwezi kulinganisha upatiksnaji ws kazi ns kipato hspa bongo na uk. Kule kazi yoyote inakulipa sio hapa bongo. Si kweli eti wabongo hawapendi kazi. Ishu ni uchumi ni mdogo hivyo uwezo wa uchumi wetu kuzalisha ajira ndogo na kubwa rasmi na zisizo rasmi. Purchasing power ni ndogo!
 
Change you're mind run to search success
 
Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,761
2,000
Kuna kipindi tunaandika mambo kwa mihemko sana. na hili ni tatizo. moja ya tatizo kubwa kwa sisi tulioko huku tunajiita diaspora tunadhan kuwa tayari tuna akili ya tofauti. wengi tunajisahaulisha maisha ya tanzania yalivyo. kwa umbumbumbu,ujinga au upuuzi. unazungumzia uk unakoweza kufanya kazi zaidi ya 2 kwa masaa. hivi unajua mazingira ya dar yalivyo? unaweza kufanya kazi 3 kweli kwa siku ukafanya kwa ufanisi?

haina haja ya kujitekenya na kucheka mwenyewe mpaka unakaa chini ukishikilia mbavu na kutokwa machozi. kuna tofauti kubwa ya mifumo ya kodi ya kwa wenzetu na huku. kule wnafanya kazi na kulipwa kwa masaa. huku ukiingia saa 1:30 asubuh ni mpaka saa 11:00 au 11:30 jioni ukitoka ukahangaika na kupata usafiri kama huna usafiri unafika nyumbani saa 1 au 2 na wakati mwingine 3 usiku. hapa unasema huyu mtu ni mvivu angefanya kazi sehemu nyingine? wewe unatumia ubongo kweli au??????????????

kesho mwananchi huyu anaamka saa 10 au 11 alfajir akamate barabara na daladala kuwah kazini. hiyo kodi anayokatwa na serikali wanakula watoto wa wakubwa na wakubwa flan ambao wanakuja kusema escrow si pesa ya serikali.... wanakula watu flan kwa mikataba hewa, na miradi hewa au bubu ya wazalendo.wanalipana posho na safari,vikao visivyo na msingi huku wabunge wakilipwa mamilioni ya pesa kwa kwenda kulala na kutalii dodoma. haya ninyi hamyasomi? mbona mi naishi nje lakini sikosi jambo hata moja Tanzania? na kila mwaka lazima mara 3 nifike Tanzania nchi yangu?

ukishaa kule ni rahisi kwa msomi wa kitanzania ku brush viatu airport but mwambie huyo uncle wako aje a brush viatu hapa JKN au Kilimanjaro au Songwe airport. inawezekana? acheni kuwaza kipuuzi.
unaweza ukawa mwokora matunda au mfagiaji barabara wa uk na usa but hebu jaribu kazi hiyo hapa dar. jaman ukiishi nje ina maana unasahau kabisa kutumia akili yako kwa manufaa? ni lazima ilinuonekane umekaa kaa nje basi utukane na kudharau waliopo tanzania? tusifike huko na kuishia kuwa wajivuni sababu ya ujinga uliokubuhu.

nimeshasema, kama utanichukia basi na iwe hiyvo.
 
Mkuu sio ugonvi lakini nimesema vizuri tunatakiwa kuzifanya kazi zetu ziwe known branding ili kuweza kuzifanya zisajiriwe kuwa kampuni ili zikopesheke na ziajiri watu zaidi kwa mfumo lasimi!!!
 
Malick M. Malick

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
647
500
Hakuna asiyependa kulipa kodi kama zinatumiwa ipasavyo.
Tatizo wenye mamlaka wanazitumia vibaya. Sidhani kama kuna mtu atafurahia kulipakodi wakati zinaliwa na wajanja wachache.
Sio kwa serikali hii ya JPM.. Fedha zitatumika vizuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom