Magufuli: Walioanza kulalamika hakuna pesa mifukoni ni wale waliozoea kupata pesa za burebure

Huu ndio ukweli basi Malisa ,Zitto na mtatiro anadaeni makala Rais kaongea na kawapa topic
 
Kweli Mungu katupatia Rais wa aina hii? Dah!! Maana yake ki ukweli rais hajui hali halisi ya huku mtaani? Inabidi tujihurumie sana... Kampuni nyingi zinafunga zina quit Tanzania market. Rais anachekelea.. Au ndio ushetani aliokuwa anautaka? Daah!!!
Kweli watu watamuombea ? Au wateuliwa kina pole pole ndio watamuombea tu wenyewe..
Kwa namna ambayo enzi za Kikwete uchumi wa nchi ulivyokuwa ukiendeshwa makampuni mengi ya ma-crooks yaliingia hapa nchini, kujisajili na kuanza kufanya biashara au uzalishaji hivyo kukidhi malengo yao ya kujinufaisha pasipokujali maslahi ya nchi. Kuna makampuni yamejifilisi na kufunga ofisi ili kukwepa kudaiwa kodi ambazo awali walikuwa hawalipi. Kwa sasa Tanzania inaweza kutegemea kupokea wawekezaji na wafanyabiashara genuine tutakaoshirikiana nao, hivyo wao na nchi kunufaika sawia (mutual beneficiation).
 
Uzuri ni kwamba wale wapambe wa kushangilia kila lifanywalo na Rais na CCM ndiyo jua linawapiga utosini hasa, namba wanaisoma hasa kuliko wengi wetu ambao tunafahamu kuwa maisha ya binadamu hupatikana kwa ubunifu, kufanya kazi na kutumia akili na siyo kushinda unaimba nyimbo za kumsifu mtu au chama hata kama unakupelekwa machinjioni.

Tena ni vema hali iongozeke mara tano ya hapa, labda wale waimbaji wa sifa watapata akili ya kutafakari kwa kila jambo linalowazunguka.
 
Mimi binafsi ni mchuuzi nina vi grocery 2, mambo yangu yalikuwa yanaenda vizuri hadi mwezi mmoja baada ya uchaguzi. Hivi sasa imekuwa ngumu hadi kulipa wafanyakazi. Hii imeadhiri kipato changu na ajira za watu kama 4
 
Kila mtu anapenda kazi ili apate pesa

Sasa kazi zipo kwa wachache...

Serikali iangalie namna ya kutengeneza Ajira

Kipimo kikubwa kwa serikali yeyote makini duniani ni kuongeza ajira...create jobs

Obama wakati aliingia madarakani aliahidi ajira na kweli Obama akaweza....

Sarkosy wa Ufaransa alishindwa kutengeneza ajira, akawa one term president....

Faida za kutengeneza ajira ni kubwa mno

1- Kutumia nguvu kazi ya vijana kuzalisha mali na kuinua uchumi

2 - Hizo ajira, lazima walipe PAYE Na kodi ya VAT kwa sababu watanunua bidhaa

Namna gani kutengeneza Ajira

1 - Tenga maeneo maalumu (Land bank/ardhi maalum), karibisha vijana Wa Kitanzania na Watanzania wengine

Kila Mwaka watalipa Kodi kwa serikali

Sasa hivi Kijana yeyote au Mtanzania akitaka kuanzisha Kilimo, atakwama....hajui aanzie kwa Lukuvi au aanzie wizara ya kilimo au sijui wapi...Darkness

Kilimo ndo kitazalisha Mali ghafi za Tanzania ya Viwanda....

Kuna fursa nyingi za Kilimo na masoko

----Kilimo cha Miwa (Sukari)
---Kilimo cha Mawese (Palm oil)
-Alizeti (sunflower)
-Sesami (ufuta)
-Maize



2 - Tourism improvement..

Fanya marketing promotion za kutosha kupata watalii

Hizo hapo juu ndo Road Map ya kwenda kwenye Tanzania ya Viwanda
 
Kweli Mungu katupatia Rais wa aina hii? Dah!! Maana yake ki ukweli rais hajui hali halisi ya huku mtaani? Inabidi tujihurumie sana... Kampuni nyingi zinafunga zina quit Tanzania market. Rais anachekelea.. Au ndio ushetani aliokuwa anautaka? Daah!!!
Kweli watu watamuombea ? Au wateuliwa kina pole pole ndio watamuombea tu wenyewe..
Ukiona kampuni inafunga huduma zake na kuhama ujue ILIKUWA INAKWEPA KODI, full stop.
 
Back
Top Bottom