Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,753
- 71,126
Mgombea wa CCM amewaahidi Walimu kuwa akichaguliwa atawapatia maisha bora kama Mapadre. Ahadi hiyo imeleta maswali mengi zaidi kwani ni Watanzania wachache wanaojua maisha hayo bora ya Mapadre kwani wao wanaishi maisha ya kitawa katika maeneo yao wanayoishi ambayo kwa kawaida huwa wanajitenga kulingana na kanuni za kazi yao.
Au huu nao ni mwendelezo wa ahadi za kukurupuka kama zile ambazo tuliziona 2010 na zimebaki kama riwaya kwenye vitabu? Jee kiongozi anaposimama na kujiropokea ahadi anazojua hazipo na haziwezi kuwepo ni dharau kwa wapiga kura au ni maagizo ya chama anachokiwakilisha?
Wapo walimu ambao kutokana na Imani zao za kidini hawawezi kuishi maisha yao kama mapadre hao amewachukuliaje?