Magufuli wa Mwaka 2019 ni Yuleyule wa 2020 Katika Miradi ya Maendeleo

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Kasambula Theonest, Kigoma

Tanzania leo inaungana na mataifa mengine duniani kuuaga mwaka 2019. Kuna mengi mazuri ya kuusemea huu mwaka lakini makala hii inaongelea kazi nzuri aliyofanya Rais John Magufuli wa Tanzania katika mwaka huu wa 2019 na inayoendelea mwaka 2020.

Kwanza nikiri kwanza kwamba Rais Magufuli amefanya mengi katika mwaka 2019 katika kuwaletea watanzania maendeleo. Kwa wingi huu naomba nikiri kuwa siwezi kuandika yote maana komputa mpakato itavunjika. Nitaandika machache kwa leo mengine nitayandika siku za usoni kwani kazi ndo imeanza.

Ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika Afrika Mashariki na la nne kwa ukubwa Afrika ( Mwalimu Nyerere Hydropower Project)
Katika mwaka 2019, Rais Magufuli ameweza kusimamia wazo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere la kujenga bwawa kubwa la umeme litakalozalisha megawati 2,115 litakalo kamilika mwaka 2022 katika mto Rufiji.

Haikuwa kazi rahisi kwa sababu ya kelele za wapinga maendeleo wa ndani na nje ya nchi waliotaka kukwamisha kazi hii lakini Rais alisimama kidete na kuhakikisha mradi unatekelezwa.

Mradi huu unaojengwa kwa kodi za wananchi kwa zaidi ya shilingi tirioni sita za kitanzania ukikamilika utaweza kuifanya Tanzania kuwa msambazaji mkubwa wa umeme katika nchi za Afrika mashariki na kati.

Usafiri wa Anga
Ni vigumu kuamini lakini ndo ukweli kuwa tunamaliza mwaka 2019 Rais Magufuli akiwa amenunua ndege nane katika 11 ambapo tatu zinatarajiwa mwakani. Shirika la ndege lilishafirisiwa na mafisadi na kulikuwa na ndege moja tu wakati Magufuli anaingia madarakani. Sasa Magufuli amerudisha heshima ya Tanzania.

Ukiwa Afrika Kusini, Zambia, Malawi, DRC, Mumbai- India na muda si mrefu Guangzhou utaona twiga wetu akikuambia Tanzania tupo laivu kazini. Tunaambiwa baada ya ndege za abiria sasa madege ya mizigo yanafuata. Huyo ndo Magufuli Rais wa Watanzania, mchapa kazi na asiyependa nchi kuitwa maskini wakati ina rasilimali nyingi.

Umeme Vijijini
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tangu tupate uhuru, Rais Magufuli anaifanya nchi kuingia katika mwaka mpya wa 2020 huku vijiji 9000 kati ya 12,000 vikiwa vimeunganishwa na umeme. Asante sana Rais Magufuli kwa kuona shida za watanzania wanyonge na kuwaunganisha na gridi ya Taifa ili wapate maendeleo.
Ikumbukwe pia kuwa bila umeme hamna maendeleo.

Huyo ndo Rais Magufuli ambaye ameamua pia kila mwaka bilioni 200 za kitanzania zitolewe kupitia mradi wa umeme vijijini ( REA) ili kujenga mifumo ya umeme vijijini na kununua miundo mbinu yake. Naweza Kusema hongera wana vijiji wa kitanzania hayo ndo matunda mliyochuma mlipomchagua Maguguli kuwa rais wenu mwaka 2015.
Upatikanaji wa maji safi na salama vijijini.

Katika moto uleule wa kuwajali watu maskini na watanzania kwa ujumla, Rais Mafuguli anaifanya Tanzania kuingia mwaka 2020 huku asilimia 67 za wananchi wanaoishi vijijini wakiwa wameunganishiwa maji safi na salama kutokana na miradi 1600 iliyoanzisha na serikali ya awamu ya tano.

Raisi Magufuli anatuambia kuwa mpaka mwaka 2025 kila kijiji kitakuwa kimeunganishiwa maji. Kwa wale tunaoishi tunaona kuwa upatikanaji wa maji umeongezekeza.

Takwimu zinasema zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaoishi mjini wameunganushiwa maji na yanatoka kila siku. Haya ndo matunda ya uhuru, tuendelee kumuunga mkono jemedali wetu Rais Magufuli.

Sekta ya utalii
Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru, Rais Magufuli ameongoza jitihada za kungeza watalii ili kuinua pato la Taifa ambapo sekta ya utalii ni ya pili katika kuchangia pato la Taifa.

Pamoja na kelele za mabeberu na wanasiasa wa upinzani kuizushia Tanzania kuwa ina ebola ili watalii wasitemebelee nchi mwaka 2019, nchi imeendelea kupata watalii zaidi ya 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwamo ulaya, Asia, Israel, Mashariki ya kati, Nchi za Amerika na nyingine duniani.

Takimu zinasema katika kipindi cha mwaka jana sekta ya utalii imelingizia Taifa zaidi ya tirioni tano za kitanzania ukilinagnisha na tirioni nne za kitanzania zilizoingia mwaka 2016. Huu ni ushindi mkubwa kwa taifa letu tuendelee kumuunga mkono Rais Magufuli ili aendelee kuibadilisha nchi ili watanzania wafaidi matunda ya uhuru wao.

Reli ya Kisasa ( SGR)
Sio ndoto za alinacha wala hadithi za alfu ulela ulela bali ni ukweli usiokuwa na chenga kwamba muda si mrefu Rais Magufuli ataongoza watanzania kufungua reli ya kasi na ya kisasa katika kipande cha kwanza kutoka kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro. Kipande hiki cha kwanza kimejengwa kwa kodi ya watanzania kwa kiasi cha zaidi ya tirioni mbili za kitanzania ( US1billion)
Huu ni mwanzo tu mradi huu umegawanyika katika awamu nne.

Awamu inayofuata ni kuanzia Makutopola – Tabora (Km294), Tabora- Isaka (Km 133 km) and Isaka- Mwanza (Km248)
Kukamilika kwa mradi huu utakaokuwa na kilometa za mraba 2,561 na kutumia zaidi ya tirioni 28 ( US$ 14.2) za Kitanzania kutaiunganisha Tanzania na nchi zisizokuwa na bahari au maziwa mfano DRC, Rwanda, Burundi na Uganda.

Huu ndo utakuwa mwanzo kwa kukuza uchumi wa nchi. VIVA Magufuli, 2020 kazi iendelee.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom