Magufuli vs. CCM-Asilia. Nani atakuwa wa kwanza kupepesa macho?

Najiuliza tu:
Je katika hizi sarakasi zinazoendelea WATAFUKUZANA?
Je kwanini "kunao waliokuwa wakisema na kujisifia sana sasa wako kimya?"
Je kwanini kuna wengine wamekuwa na tuhuma muda mrefu hawaguswi ina maana chamani mwao bado kuna WASIOGUSIKA?

Utajua hili suala ni zito kwa jinsi kila upande unavyocheza mchezo kwa umakini. Hii ingekuwa 2016 au 2017 Magufuli angekuwa ameshafukuza watu zamani.

Niliwahi kuleta uzi nikigusia jinsi style ya zamani ya Magufuli ilikuwa inamuweka kwenye hatari zaidi.

https://www.jamiiforums.com/threads/is-this-chess-or-checkers.1235252/

Naona sasa kwa kiasi kikubwa amebadilisha style yake kwa kuwatumia watu kama kina Musiba na wengine huku yeye akikaa pembeni. Hiyo kidogo inampa room ya kucheza mchezo kwa uhuru zaidi.
 
Wanasiasa wanajuana vizuri
Wako wanapigania maslahi yao tunawatazama kwa makini.
Ingekua Hawa wazee wanazungumza tukiguswa watanzania ingekua sawa Ila wanazungumza wakiguswa wao tu.
 
Nadhani tathmini yangu haikuwa mbali na ukweli ukizingatia yale yaliyokuja kutokea.
 
Back
Top Bottom