Magufuli vs. CCM-Asilia. Nani atakuwa wa kwanza kupepesa macho?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000
Kuna mchezo mmoja wa watoto unaitwa 'Who Will Blink First'. Katika mchezo huo watu wawili wanaangaliana na anayekuwa wa kwanza ku 'blink' au kupepesa macho anakuwa ameshindwa.

Katika sakata linaloendelea huko ndani ya CCM mchezo ambao umekuwa unachezwa ni huu nilioutaja hapo juu.

Toka audio clips zilipoanza kutoka nilisema hizi zimerekodiwa na kuachiwa na wahusika wenyewe kwa lengo maalumu (sikulitaja kwa sababu nilikuwa bado nafanya tathmini).

Team CCM-Asilia kama walivyosikika wanasema ni kwamba wanajaribu kuchochea na kuwapa ujasiri wana CCM-Asilia wengine waanze kutoa hisia zao waziwazi kuhusu mienendo ya chama na nchi.

Nimetoka kusikiliza clip ya Membe na Katibu Kata, hii clip na yenyewe imeachiwa kimkakati kabisa. Ukizungumza ngazi ya Kata unaongelea CCM wa chini huku, hii wamefanya ili isionekane kuwa hili ni suala la wazito walio juu tu.

Kwa kumalizia, kitendo cha The Gang of Five kwa mpigo kujihusisha na waraka na audio clips pia haikuwa kwa bahati mbaya. Wanajua Magufuli pamoja na jeuri yake hawezi kuwavua uanachama wote Membe, Makamba Sr na Jr, Nape, Kinana kwa mpigo. Swali linabaki, je atatoa adhabu gani huku akiwaweka hawa siyo tu 'at arms length' lakini ikiwezekana pia kuwatenganisha na wakati huo huo aweze kuproject mamlaka isiyotikisika? Hilo ndiyo zoezi kubwa linalomkabili.

Je akifukuza baadhi yao na wengine akawapa onyo kali kama alivyofanya wakati ule kwa Sophia Simba na Nchimbi, je haitaonekana amewaogopa? Ukizingatia ukubwa wa 'kosa' wanaloshutumiwa nalo hiyo italeta tafsiri gani kwa wengine wanaosikilizia upepo unaelekea wapi? Je, The Gang of Five hawataonekana mashujaa wanaostahili kuigwa?

Wasiwasi wangu ni kuwa hili jambo linaweza kabisa kwenda out of control na likatuathiri hata watazamaji. Ni dhahiri The Gang of Five hawako peke yao. Ni wazi Magufuli analijua hilo. Na yeye anapalilia vitu ili mambo yakienda ndivyo sivyo aende kama Tony Montana. Huo ndiyo wasiwasi wangu.
 
lukindo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2010
Messages
8,469
Points
2,000

lukindo

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2010
8,469 2,000
Na hapo ndipo ccm walipokosea na kama chama kikongwe huenda kikaipeleka nchi kusiko.Huwezi kuwa na chama alafu kuna wadudu wanajiita sijui asilia na wengine sijui wakuja. Chama kinataka kuleta maendeleo lakini humo huko kuna makundi ya kulinda maslahi ya watu fulani.
Hebu chukulia mfano kama cdm wasingechukua maamuzi magumu ya kuwaondoa akina Mwaigamba, ZZK na wengineo waliojidhihirisha kuwa walikuwa sio tu wasaliti bali ccm saa hivi wangekuwa wapi!?
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
6,105
Points
2,000

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
6,105 2,000
Kuna mchezo mmoja wa watoto unaitwa 'Who Will Blink First'. Katika mchezo huo watu wawili wanaangaliana na anayekuwa wa kwanza ku 'blink' au kupepesa macho anakuwa ameshindwa.

Katika sakata linaloendelea huko ndani ya CCM mchezo ambao umekuwa unachezwa ni huu nilioutaja hapo juu.

Toka audio clips zilipoanza kutoka nilisema hizi zimerekodiwa na kuachiwa na wahusika wenyewe kwa lengo maalumu (sikulitaja kwa sababu nilikuwa bado nafanya tathmini).

Team CCM-Asilia kama walivyosikika wanasema ni kwamba wanajaribu kuchochea na kuwapa ujasiri wana CCM-Asilia wengine waanze kutoa hisia zao waziwazi kuhusu mienendo ya chama na nchi.

Nimetoka kusikiliza clip ya Membe na Katibu Kata, hii clip na yenyewe imeachiwa kimkakati kabisa. Ukizungumza ngazi ya Kata unaongelea CCM wa chini huku, hii wamefanya ili isionekane kuwa hili ni suala la wazito walio juu tu.

Kwa kumalizia, kitendo cha The Gang of Five kwa mpigo kujihusisha na waraka na audio clips pia haikuwa kwa bahati mbaya. Wanajua Magufuli pamoja na jeuri yake hawezi kuwavua uanachama wote Membe, Makamba Sr na Jr, Nape, Kinana kwa mpigo. Swali linabaki, je atatoa adhabu gani huku akiwaweka hawa siyo tu 'at arms length' lakini ikiwezekana pia kuwatenganisha na wakati huo huo aweze kuproject mamlaka isiyotikisika? Hilo ndiyo zoezi kubwa linalomkabili.

Je akifukuza baadhi yao na wengine akawapa onyo kali kama alivyofanya wakati ule kwa Sophia Simba na Nchimbi, je haitaonekana amewaogopa? Ukizingatia ukubwa wa 'kosa' wanaloshutumiwa nalo hiyo italeta tafsiri gani kwa wengine wanaosikilizia upepo unaelekea wapi? Je, The Gang of Five hawataonekana mashujaa wanaostahili kuigwa?

Wasiwasi wangu ni kuwa hili jambo linaweza kabisa kwenda out of control na likatuathiri hata watazamaji. Ni dhahiri The Gang of Five hawako peke yao. Ni wazi Magufuli analijua hilo. Na yeye anapalilia vitu ili mambo yakienda ndivyo sivyo aende kama Tony Montana. Huo ndiyo wasiwasi wangu.
Inawezekana. Swali la ziada hivi kwanini Sophia Simba alipomkana Yohana hadharani hakufukuzwa chamani?
 
Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000
Inawezekana. Swali la ziada hivi kwanini Sophia Simba alipomkana Yohana hadharani hakufukuzwa chamani?
Bado alikuwa mgeni kwenye chama kwa hiyo labda alitaka kwenda nao taratibu. Pia kumbuka kuna kusalitiana, hauwezi kujua role yake kwenye lile sakata lilikuwa ni nini hasa.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
6,105
Points
2,000

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
6,105 2,000
Bado alikuwa mgeni kwenye chama kwa hiyo labda alitaka kwenda nao taratibu. Pia kumbuka kuna kusalitiana, hauwezi kujua role yake kwenye lile sakata lilikuwa ni nini hasa.
Najiuliza tu:
Je katika hizi sarakasi zinazoendelea WATAFUKUZANA?
Je kwanini "kunao waliokuwa wakisema na kujisifia sana sasa wako kimya?"
Je kwanini kuna wengine wamekuwa na tuhuma muda mrefu hawaguswi ina maana chamani mwao bado kuna WASIOGUSIKA?
 
Forum statistics

Threads 1,381,917
Members 526,218
Posts 33,814,256
Top