Magufuli: Vijana wengi hawapendi rushwa kama wazee, ntaongeza vijana zaidi kwenye serikali yangu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Rais Magufuli amesema anafikiria kuongeza vijana zaidi kwenye serikali yake kwa kuwa hawapendi rushwa kama wazee, Amesema hayo huku akimtolea mfano Paul Makonda

Amesema wanashangaa sana kwa sababu hawajayazoea haya, na walifikiri atakuwa mmoja wao lakini 'never' na atawashughulikia kwelikweli hata kama ni kutumbua kila siku yeye atatumbua tu.

Na Tanzania ikipelekwa kikwata kwata ndio itabadilika.Ameongezea Tanzania ilikuwa imechakazwa na rushwa huku akitolea takwimu za wafanyakazi hewa na fedha zilizopotea kwenye miradi hewa na wanafunzi waliopata division four kupelekwa chuo na kupata mikopo.

Pia amezungumzia meli nyingi zilizokuwa zinafika na makontena mengi lakini makontena yalikuwa hayaonekani, na amesema atapambana nao hata kama itamaanisha kujitoa sadaka kimwili.
 
Rais Magufuli amesema anafikiria kuongeza vijana zaidi kwenye serikali yake kwa kuwa hawapendi rushwa kama wazee, Amesema hayo huku akimtolea mfano Paul Makonda

Lakini Rais wangu mpendwa usisahau pia wapo wazee waadilifu sana ambao yakupasa kuwaa nishani. pia nilazima ukumbuke wazee ndio tunu yetu kuwapata vijana wazuri.
 
Vijana taifa la leo halafu wazee taifa la kesho safi sana tukihitaji ushauri wenu tutakuja ila naamini kabisa hata nyie wazee mlikuwa vijana hebu kaeni pembeni mpishe damu changa tuendane na kasi ya mheshimiwa kwa sababu inaonekana hamna jipya tena tangu 1971 mko kwenye mchakato na upembuzi yakinifu hapana imetosha
 
Back
Top Bottom