Magufuli versus Tundu Lissu; yupi unamwamini kwenye sakata la makinikia?

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,501
2,000
Hivi TMAA, TRA etc. ni serikali? Kuna namna tunajivua nguo kama taifa bila kujua. Tukienda mahakamani tutasema TMAA na TRA walikuwa wanatudanganya?

Itakuwa muhimu sana kupata ushahidi wa namna Acacia walivyoingilia utendaji wa TMAA, TRA etc, ili kujenga hoja kuwa "walidanganya". Nje ya hapo tutapigwa tena na Mara hii mapema zaidi!
 
kg1

Senior Member
May 27, 2017
152
225
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

Unawezaje kumlinganisha mtu mwenye akili zake timamu dhidi ua mwenue akili zenye tund?
Halafu unaanzaje sasa? la sivyo wewe kwa vyovyote utakuwa na TUNDU katika akili yako!
 
S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
500
Magufuli ameongea kwa reference ya Tume ya wataalamu...lakini pia kumbuka ni mkemia mwanasayansi tofauti na ngwini Lissu.
Hata Waliosaini Mikataba ya madini tuchukue asilimia 04% tu ya mrahaba ni Watalaam....Katiba Mpya nayo ilifanyika kitalaamu na ikaja kukataliwa na wanaojua kusoma na kuandika tu.....
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
117,645
2,000
Utamwiminije mwizi wa nyumba za Serikali, mnunuzi wa kivuko uozo na aliyelidanganya Bunge kuhusu upotevu wa mabilioni ya pesa za ujenzi? Yote haya yamo kwenye ripoti za CAG.

Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

kalla

Member
May 23, 2017
18
45
Hapa naona kama tunawekwa kuja Giza amblo mwana wak unahitaj elim na sio malumban

Lakin pia naona kama rais amekuwa yuk mbele bila kutoka kujua hoja n mitaxam ya wapinzan hiki kitu kinaleta uchum na maendeleo kuwa kama yanasukumwa na kinyonga

Raisi muaminf ni yule mweny Hekima busara na upendo magufuli badilika masikin wanufaike

Viva lowassa 2020
 
dullynho

JF-Expert Member
Jul 17, 2016
350
250
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

vp mtazamo wa chenge na werema? unakinzana na nani? wengi wapewe wenye mitazamo inayofanana hao wa 2 ongeza na chenge na werema wapewe wengi
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,093
2,000
Kila mtubana haki! Ila kitu sipendi ni unafiki!

Okey lets say anafwatilia...je hiyo mikataba unadhan itavunjwa kijinga tu?? Angekataa isisahiniwe kama kweli alikua na nia njema!
Ingekuwa inavunjwa kijinga angeunda time ya sheria??
 
dullynho

JF-Expert Member
Jul 17, 2016
350
250
Hiv lissu anajua hata symbol ya GOLD ni Au, Copper ni Cu. ,iron ni Fe, au anaropoka tu?
sawa mkali wa chemistry ila kweny makontena hakuna symbol bali kuna madin yenyewe so hatupimi symbol tunapima madini na ktk chemi tunapima reaction yenyewe
 
danymTZ

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
342
500
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

Acha kulinganisha Rais wa nchi na vitu vya kijinga
 
Gauss93

Member
Mar 28, 2017
9
45
Magufuli angekuwa na akili angefuatilia hili na kujiridhisha kama hii statement ni kiki tu au ina ukweli wowote. Ila kama kawaida, hatapoteza muda kufuatilia.

Harafu kama zile kontena zimebeba deal la kufa mtu as per Prof. Mruma na team yake, Serikali izinunue basi kwa bei ACACIA aliyokuwa anakwenda kuuza then tukaelewane na wachenjuaji watuchekie kilichomo ndani na tupige faida kabla ya kurudi kujadili terms upya na ACACIA.
Rais hawezi kuwa anakaa kufatilia kuprove au kudissprove kila kitu anachosema mtu, akifata ya TL mtataka na ya Zitto afatalie, ana akili yake washauri wake na mipango yake full stop. Hata akifata ushauri wa Lissu sio lazima aseme kwamba ameufata.

Serikali kununua makontena yanayocontain mali za wizi ni upumbavu mkubwa over scale yaan sio wa dunia hii.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom