Magufuli utaua mawaziri waliopita kwa njaa, hawana cha kufanya

The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
9,395
20,630
Mh. Magufuli kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyoifanya mpaka sasa, japo sijutii kura yangu niliyompa mamvi na wala sitakaa nijutie, tulikuwa tunataka mabadiliko na sasa ninayo furaha ya dhati kabisa kuyaona haya mabadiliko kupitia kwako

Pili Mh. Nilichofurahi zaidi ni kupunguza gharama kubwa za kuhudumia wizara na mawaziri wake 60 wa awamu iliyopita hakika wewe ni mzalendo, na samia pia najua aliupata uzalendo zaidi katika kipindi za kampeni kijiji kwa kijiji nilimshuhudia akimwaga chozi kwa shida za wananchi alizokumbana nazo huko vijijini hakuamini na alituahidi na wasanii wakiwepo(mashahidi) mtaipitia mikataba yote ya madini

Mh. Magu chukua hii kama New year special, ulivyowatimua wastaafu mawaziri kwenye nyumba za serikali wengine hawana pa kukaaa, hakya Mungu tena ninaapa, hawakuona umuhimu wa kujenga kwa maana walijua nyumba za serikali ni zao

so sad , kuna mmoja anakaa kwa shemeji yake, (kaka wa mke wake) amechoka vibaya, sasa mbaya zaidi kaja na kuku wake kila siku wanatifua bustani za majirani maana humo ndani hamna banda wanafugia nje inaleta usumbufu mno, na hataki kuondoka mpaka ahakikishe kwamba hata ukuu wa wilaya amekosa ndio atarudi mwanzaaaa

Ninachokuomba Mh. harakisha hizo teuzi usifanye kwa nukta nukta utaua watu na njaa, hawana pa kuishi, hawana kazi, ubunge wamekosa, january hii watoto adaa mheshimiwa ujue hawasomi shule za kata, soon watakosa chakula na mimi ninasema ikifika february kuku wake wakiendea kutifua bustani yangu nakula mmoja baada ya mmoja
ImageUploadedByJamiiForums1451655626.544909.jpg
 
Last edited:
hadi sasa wameshakufa wangapi, wanatakiwa kama wanakufa wafe haraka ili sisi tusichukue muda mrefu kuandaa mazishi yao, hapa tupo kwaajili ya kazi tu hatutaki kitu cha kutuchelewesha. na walivyoitafuna hii nchi majina yao hata sitaki kuyasikia masikioni mwangu. wapotee kabisat usijekuwasikia tena milele kwenye vyombo vya habari.
 
Hehebhehe Hehe hehe hii kama ni kweli basi mtihani sana kuishi kwa kutegemea siasa zikupe maisha, kwa wenye hekima uongozi huwa si wa kukimbilia huwa unateuliwa na watu wanaokuamini uwaongoze lakini kwa wao wakiokuwa mpaka wakihonga ili wapate dhamana za uongozi hao ni mufilisi kabisa na mungu awaadhibu kwa uovu walioufanya kipindi wakiongoza ncgi yetu. wasipotubu na kumrudia muumba wao wacha waisome namba tena kwa tarakimu KUBWA.
 
Kweli aisee, watu wanaisoma namba
kuna wengine wameisoma namba hadi raha, natamani nikutane nao kitaa hawana cheo wala nini, hadi ubunge wamekosa. na kwa mabadiliko ya siasa tz, ndio wasubiri tu uzee uwaishie watangulie kwa muumba wakahukumiwe kwa kuwanyanyasa watz kwa kula hela zao na kuwaibia kodi zao.
 
wengi watakufa kwa ugonjwa wa moyo muda si mrefu, visukari tayari na wengine wanakunywa arv, na uwezo wa kwenda kubadilisha damu ulaya hawana tena, mirija imezibwa.
 
Watanzania shida sana, kiongozi akiiba taabu, asipoiba taabu. Halafu jukwaa limekuwa na majungu na umbea mwingi, jf inaelekea wapi? Kuna haja ya kupima IQ za watu kabla ya kujiunga jf, mods chukueni hiyo.
 
kama ni majungu na umbea kwa mafisadi, what's wrong with that?...ulitaka tuwapake mafisadi mafuta kwa mgongo wa chupa au tuwafunge na kamba za viatu kama naniliuuuu
 
Labda hujui kusoma, mwenzio anamcheka waziri Mstaafu asiye na fedha. Mada za Facebook
 
Watanzania shida sana, kiongozi akiiba taabu, asipoiba taabu. Halafu jukwaa limekuwa na majungu na umbea mwingi, jf inaelekea wapi? Kuna haja ya kupima IQ za watu kabla ya kujiunga jf, mods chukueni hiyo.
Sasa hapo majungu yako wapi?nimeomba raisi Magufuli awahishe hizo teuzi ili waliokosa waendelee na jitihada nyingine za kimaisha kuliko kusubiri teuzi zisizo na uhakika, kuliko kukaa na kusubiri bila shughuli yoyote
 
mtaje jina huyo "WAZIRI mstaafu" mwenyeji wa Mwanza aliyehamia kwa Shemeji. Mimi nilikutana na mmojawapo anafuatilia Cheti chake OPEN UNIVERSITY anadai anataka kuomba kazi japo ya ualimu (akumbukie enzi)
 
Mkuu sitamtendea haki, nimemtumia tuu kama mfano wa ex ministers wanaosota, sijatunga kitu
 
duu
Mh. Magufuli kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyoifanya mpaka sasa, japo sijutii kura yangu niliyompa mamvi na wala sitakaa nijutie, tulikuwa tunataka mabadiliko na sasa ninayo furaha ya dhati kabisa kuyaona haya mabadiliko kupitia kwako

Pili Mh. Nilichofurahi zaidi ni kupunguza gharama kubwa za kuhudumia wizara na mawaziri wake 60 wa awamu iliyopita hakika wewe ni mzalendo, na samia pia najua aliupata uzalendo zaidi katika kipindi za kampeni kijiji kwa kijiji nilimshuhudia akimwaga chozi kwa shida za wananchi alizokumbana nazo huko vijijini hakuamini na alituahidi na wasanii wakiwepo(mashahidi) mtaipitia mikataba yote ya madini

Mh. Magu chukua hii kama New year special, ulivyowatimua wastaafu mawaziri kwenye nyumba za serikali wengine hawana pa kukaaa, hakya Mungu tena ninaapa, hawakuona umuhimu wa kujenga kwa maana walijua nyumba za serikali ni zao

so sad , kuna mmoja anakaa kwa shemeji yake, (kaka wa mke wake) amechoka vibaya, sasa mbaya zaidi kaja na kuku wake kila siku wanatifua bustani za majirani maana humo ndani hamna banda wanafugia nje inaleta usumbufu mno, na hataki kuondoka mpaka ahakikishe kwamba hata ukuu wa wilaya amekosa ndio atarudi mwanzaaaa

Ninachokuomba Mh. harakisha hizo teuzi usifanye kwa nukta nukta utaua watu na njaa, hawana pa kuishi, hawana kazi, ubunge wamekosa, january hii watoto adaa mheshimiwa ujue hawasomi shule za kata, soon watakosa chakula na mimi ninasema ikifika february kuku wake wakiendea kutifua bustani yangu nakula mmoja baada ya mmoja View attachment 314189
nimecheka sana
 
Yale mambo ya kufikiria uongozi ni kupewa hati miliki yaachwe sasa. Uongozi ni utumishi
 
Back
Top Bottom