Magufuli, unayajua ya Hazina na Msajili wake mpya?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Kaka yangu ndugu Rais Magufuli pole sana na kazi ngumu uliyo ianza . Mimi leo nimeona nikuulize tu tokea mbali huku maana siwezi kukusogolea karibu sijui ni hofu au kitu gani sijui ila nimeoma nikuulize tu . Wako walio karibu nawe watakufikishia .

Ndugu Magufuli hivi unayajua madudu ya Hazina na namna walivyo mpata Msajili wa Hazina ? Nikisema msahjili wa hazina wa Treasury Registrar mpya wewe utamjua tu maana ndiye pekee anaye husika hata na mambo ya viwanda kama sijakosea.

Magufuli ilitokea hivi

Katibu Mkuu wa Fedha alitangaza nafasi za kazi . Wakaomba watu na baadaye wakaitwa watu 3 yaani ndugu Mbajo , ndugu Msemwa na ndugu Mafuru .

Mchakato ukawa mzito kwa Msajili wa sasa . Kwa taarifa toka maeneo yaleee zinasema ndugu Mbajo alikuwa kinara akafuatiwa na ndugu Msemwa na mwisho akawa ndugu Mafuru. Ikafanyika vetting bado kwa vigezo na uwezo kinara akawa ndugu Mbajo . Kwa katibu Mkuu wa hazina majina yakaenda 3 na kwa Katibu mkuu Kiongozi nako majina yakaenda kama yalivyo lakini yakiwa na maelezo ya kina ya kila mmoja .

Naambiwa kwamba kufika kwa Katibu mkuu kabisa mchakato ukaanza kusua sua na mwishowe ukawa kimya . Wakato huo msajili alikuwa akifanya kazi kule FBME , baadaye washikaji wake wengine toka NHC wakampigia kifua kwa influency yao akapata kazi BRN .

Ndugu Magufuli ghafla baada ya kingi mwaka jana Dec 2014 Msajili wa sasa akatangazwa kuchukua nafasi hiyo .

Huvi ndugu Rais unaijua elimu ya msajili wa sasa ? Ulizia watu wako watauelezea vyema utashangaa hata CV yake . Lakini mbaya zaidi msajili wa sasa alikuwa anafanya kazi NBC . Unataka kujua habari zake toka huko ? Fika NMB ambako aliomba kazi ile ile ya NBC watu kusikia anataka kwenda hapo na matatizo yake ya NBC wafanyakazi wakatoa taarifa kwa uongozi na wa Dutch wakamtosa .

Huyu ana kashfa za NBC , nadhani pia alidanganya juu ya elimu yake , leo kaka Magufuli unapambana na kufufua viwanda na una watu wameingia kwa nguvu za watu utaweza ?

Kaka yangu Magufuli ndugu Rais najua unaweza ukiamua hebu jaribu kuitisha file lake na uulizie mchakato mzima ulikwaje hadi msajili akatangazwa . Utashangaa sana . Kubwa zaidi kwa sasa ni namna anavyo pangua wataalam wazoefu eneo lile , Nadhani kuna undugu na kujuana kwa kuwa anaweza wanao mtii .

Nasema nasikia na ndiyo maaa ndugu Rais nakuuliza kwamba mesha wahi kusikia juu ya madudu ya hazina na Msajili wake ? Kama bado basi fanya bidii mapema usije kusema mbona hamkusema hata kama mlikuwa mbali .

Waulize watu wako wa suti nyeusi watakueleza . Wako walio shiriki kwenye vetting ila wakapatwa na mshituko wa ajabu kuona wanayo yajua siyo wala waliyo shauri kama watalaam na watu wa utawala bora .

Kaka natoka sasa hapa ughaibuni baridi kali na salaam sana toa huku mbali .
 
Kweli kabisa, huyu jamaa bwana elimu yake kuunga kwa sana!sidhan kama atakidhi hazima ya kaka Magufuli!
 
Mafuru mi nilishangaa sana nilipo sikia eti ndo msajili wa hazina watu wa NBC walistushwa na habari hizo
 
Waulize watu wako wa suti nyeusi watakueleza . Wako walio shiriki kwenye vetting ila wakapatwa na mshituko wa ajabu kuona wanayo yajua siyo wala waliyo shauri kama watalaam na watu wa utawala bora .

Hapo napo-unawezakuta mitihani tu!. Unaweza kuta wengine walikuwa sehemu ya michakato!.Lakini naona kama vile umerahisisha kazi hata suti nyeusi ikifanya kazi ikapeleka ripoti Mhe.JP atakuwa amekuwa pre-informed na ni rahisi kung'amua kitu!

Jf-kwa maendeleo ya Nchi.
 
Elimu ya kuunga ni ipi..naomba kujua jamani

Au waliojiendeleza ndio elimu ya kuunga au

mfano Mimi
shule ya msingi 1993-99
secondary O-level 2000-2003
A-level -2004-2006
University -2006-09

Naomba mnijuze elimu ya kuunga hipo kama hii
 
watu sasa mnazidi,ukiwa na chuki tu na mtu unakuja huku jf kuandika,mambo hayapelekwi hivyo!...sio kila kitu kuchafua watu,kisa chuki binafsi na wivu
 
Nini kilichomtoa huyu jamaa NBC kwanza ndio tufuate hayo mengine isije kuwa majungu na kumtesa tu Rais wetu

rais anashughulikia mambo ya msingi ya nchi,hizi figisu figisu za watu huku mitandaoni hana muda nazo
 
rais anashughulikia mambo ya msingi ya nchi,hizi figisu figisu za watu huku mitandaoni hana muda nazo


Kopites ukweli kuhusu hizi unazo ziita Figisu ni upi ? Mimi nimemuomba rais apitie mchakato mzima hadi kupatikana Msajili .Pia nimemuomba rais aambiwe kule NBC kwa nini aliwekwa pembeni kabisa na hatimaye kutemwa . Sasa wewe una majibu ya figisu zangu mwambie ndugu Magufuli ukweli wa hili . Anzia na NBC , alivyo ingia BRN, muulize yule jamaa NHC na nguvu zake juu ya huu mkuu Msajili, then pata kujua kwa nini watu wa NBC walishitushwa mno na habari ya Msajili mpya kutinga hazina .

Toa hoja mzee tuanzie hapo
 
Kwenye ukweli jamani tuseme tu, jamaa elimu ni shida.

Wakati wa matatizo yake NBC nilifuatilia sana, yamemwayo yapo...

Kama mchakato uliingiliwa na walafi, amwagwe tu...
 
dah..is there any fact au chuki binafsi?elimu sijaiona?mchakato kuwa mbovu sijaona ufafanuzi wake?Kashfa za NBC alizozibeba nazo sijaona,naambiwa tukaulize NMB?

Mleta post,yaonesha ulikatwa wewe kwa kosa vigezo sasa unajaribu kafanya fitina,watanzania bhana..kasome na wewe
 
Back
Top Bottom