Magufuli unafaa, hatuhitaji Baraza la Mawaziri

chagga land

JF-Expert Member
Jul 24, 2015
394
95
watendaji wa kila wizara wapo wengi sana cha msingi ni kufuatilia tu utendaji wao.hakuna haja ya kuwa na baraza la mawaziri maana watakuharibia tu
 
Mimi ninavyoona mawaziri wawepo ila manaibu mawaziri ndio wasiwepo na wizara zipunguzwe sana.
 
Kila nyanja inawadau wanaohitaji kushirikishwa ktk maswala mbalimbali ambayo yanayowahusu.
Kwa kifupi mwisho wa siku patahitajika uwepo wa mijadala ya kisiasa katika kushughullikia changamoto zinazojitokeza katika maeneo hayo.

Mtu pekee anayeweza kushughulika na uwanja huo ni mwanasiasa ambaye sisi tunamwita waziri, makatibu wa wizara wanabaki kuwa watendaji zaidi kuliko wanasiasa, basi.

Ingawa wizara zinaweza kupunguzwa hadi kubaki 15 ktk zama hizi HKT inawezekana kabisa ili kazi nyingine waachiwe wataalamu katika wizara
 
Sahihi kabisa panya wengi hawachimbi shimo likaenda, lakini pia miluzi mingi inampoteza mbwa
 
watendaji wa kila wizara wapo wengi sana cha msingi ni kufuatilia tu utendaji wao.hakuna haja ya kuwa na baraza la mawaziri maana watakuharibia tu

Mfano ukitokea mgogoro wa serikali na madakitari, katibu wa wizara anaweza kuongea nao?
Wanasiasa waliochaguliwa na watu ambao siku zote wanaonekana kwenye majukwaa wakitea haki za raia na wafanyakazi ndio wenye nafasi nzuri ya kutekeleza wajibu kama huo.
Ni kama mchezo wa mpira, lazima awepo refa, ndio mawaziri ati.
chagga land hapo upo?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kasi hii hakuna haja ya mawaziri, ni matumizi mbaya ya pesa za umma
 
Kama wataalamu(watendaji) wa wizara ni makatibu wakuu sasa waziri kama cheo cha kisiasa ana umuhimu gani katika wizara. Bora kuundwe muundo mpya mkuu wa wizara awe mtaalamu ambaye ni katibu mkuu
 
Kwa kasi hii hakuna haja ya mawaziri, ni matumizi mbaya ya pesa za umma

Wenzako tunangojea shavu la uwaziri wewe unasema hatutakiwi? Hata hiyo, waziri ni buffer zone ya maamuzi ya serikali ambayo ni controversial. Tunahitajika ili 'kuinusuru serikali isianguke'.
 
Wenzako tunangojea shavu la uwaziri wewe unasema hatutakiwi? Hata hiyo, waziri ni buffer zone ya maamuzi ya serikali ambayo ni controversial. Tunahitajika ili 'kuinusuru serikali isianguke'.

Hahaaaaaaaa haya bana
 
Wawepo mawaziri but manaibu watolewe.makatibu pia ni wa muhimu

Yah na nahisi kuna mda naye atahitaji kuchoka na kupumzika ..ni vizuri lakini tusimchoshe sana. Aweke mawaziri tu na makatibu, full stop.
 
watendaji wa kila wizara wapo wengi sana cha msingi ni kufuatilia tu utendaji wao.hakuna haja ya kuwa na baraza la mawaziri maana watakuharibia tu

Aseee!!!! yani huyu dingi ananikosha sana kwakweli the way anavopiga kazi. hivi miaka yooote alikuwa wapi? now tungekuwa mbaaaaali sana kimaendeleo. Yani pekee yale tuu tosha sana. Mungu amlinde Rais wetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom