Magufuli ulisema mafisadi na wala rushwa wameondoka CCM kwa kukuogopa, vipi hawa wabunge uliowanadi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Mheshimiwa Rais, nakumbuka kipindi cha kampeni ulitamba kwenye majukwaa ulisema kuwa wanaCCM wote mafisadi wameshakimbia na kukihama Chama kwa kuhofia uteuzi wako kuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama hicho, lakini tangu ushinde na kukabidhiwa madaraka tuhuma za rushwa zinawaandama wanachama na viongozi wasaidizi wa Chama chako.

Wengi wao ni wale ambao ulisimama kidete kuwanadi na kuwaaminisha wananchi kuwa wakupe watu hao ukafanye kazi na wao kwa kuwa unawaamini na kuwakubali. Ona sasa tuhuma za rushwa haziishi na kila kukicha afadhali ya jana.

Kumbe CCM ina hazina ya mafisadi na hawatokaa waishe!
 
Ahahahahahaha amna hao sio wala rushwa hao ni shushushu wa bunge ili kuona nani mla rushwa sema mtego umegoma, apo walitaka kumkamata Zitto akastuka mtego akauruka.

We subiri tego lao likubali uone mpinzani ataenasa atakoma. Wanamtaka zitto sna ili kumuua kisiasa, badae chama kama kitakua kikubwa basi ndo itakua kandamizo lake kwenye kampeni..
 
Ahahahahahaha amna hao sio wala rushwa hao ni shushushu wa bunge ili kuona nani mla rushwa sema mtego umegoma apo walitaka kumkamata zitto akastuka mtego akauruka we subiri tego lao likubali uone mpinzani atae nasa atakoma wanamtaka zitto sna ili kumuua kisiasa, badae chama kama kitakua kikubwa basi ndo itakua kandamizo lake kwenye kampeni
Hii ni Tomm and Jerry chess, panya akikimbizwa na paka usiweke mtego wa panya utamnasa paka panya atahepa, ndio hii.
 
Hii ni Tomm and Jerry chess, panya akikimbizwa na paka usiweke mtego wa panya utamnasa paka panya atahepa, ndio hii.
Ahahaha panya mjanja kuliko panya duh balaa umenipa raha sna ila ndo maisha yetu haya nakumbuka mwalimu wa hesabu kapewa mtiahi aliyondunga mwenye akafeli vibaya ahahaha hii imetokea sna niliwahi kuulizwa na ndugu yang ni mwalimu wa shule ya msingi za serikali eti kama jibu la mtoto alilotoa kwenye swali alilotunga mwenyewe kama liko sahihi sasa hii ndo tuliko huko haya twende lkn
 
hivi huyu Anna Malichela hakuwa mgombea katika uchaguzi uliopita kweli?
 
CCM ndio baba lao nashangaa kumfuatafuata Lowassa kumbe CCM no kiwanda Na hazina kubwa ya wala rushes wezi wakwepa kodi Na mafisadi
 
Mheshimiwa Rais, nakumbuka kipindi cha kampeni ulitamba kwenye majukwaa ulisema kuwa wanaCCM wote mafisadi wameshakimbia na kukihama Chama kwa kuhofia uteuzi wako kuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama hicho, lakini tangu ushinde na kukabidhiwa madaraka tuhuma za rushwa zinawaandama wanachama na viongozi wasaidizi wa Chama chako.

Wengi wao ni wale ambao ulisimama kidete kuwanadi na kuwaaminisha wananchi kuwa wakupe watu hao ukafanye kazi na wao kwa kuwa unawaamini na kuwakubali. Ona sasa tuhuma za rushwa haziishi na kila kukicha afadhali ya jana.

Kumbe CCM ina hazina ya mafisadi na hawatokaa waishe!
Wamondoka mafisadi wamebaki mafisi na wabaya hasa.
 
Back
Top Bottom