Magufuli, ukichukua mikoba CCM, nakuomba uondowe wasaliti kwanza tafadhali

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,954
Wanabodi JF

Ni UKWELI usiopingika sasa kwa watanzania wote, ya kwamba Taifa letu tumepata kiongozi ambaye tulimtarajia.
Ili kulirudishia Taifa letu heshima ya utanzania, ambayo ilikuwa inaporomoka kwa spidi isiyo na gavana (kifaa kitumikacho kudhibiti mwendo).

Lakini pia ni UKWELI usiopingika kwamba wananchi walio wengi wana Imani na Rais JPM, lakini hawana Imani Sawa na hiyo kwa CCM.

Ni UKWELI usiopingika kwamba JPM anapaswa kukabidhiwa CCM mapema Ili aitumbuwe na kuisafisha, ili iendane na Nia njema ya serikali yake.

Hii itamsaidia kuirudishia jamii ya watanzania Imani kwa chama tawala CCM. Na serikali yake.

Pia itamuepushia JPM, tatizo la kufanya kazi na wanafiki ndani ya serikali (jambo ambalo lilimsumbua baba wa Taifa).

Mengi yamejiri katika duru za siasa za nchi hii tangu kumalizika kwa Uchaguzi mkuu, ambao ulimuweka madarakani mheshimiwa JPM.

Tumeona akiingia ikulu na kuanza kazi kwa vitendo, bila masihara, akishambulia kila kona nyeti ya uchumi na Hazina ya nchi hii.

Kazi hii si lelemama, kwa sababu inataka uthubutu na Nia ya kweli ya kuutokomeza ufisadi uliotamalaki kwa kina nchini. (JPM ameonyesha Nia hiyo).anapambana na lidude linaloishi kila kona ya nchi hii.

Kila kitu kizuri kina gharama zake, iwe mwanamke, dhahabu, almasi, Amani, upendo, nk.. Nk. Vyote hivi vina gharama Tena UKWELI ni kwamba kadri kinavyokuwa kizuri zaidi ndivyo kinavyokuwa Na gharama kubwa zaidi.

Sisi Watanzania tuliyataka mabadiliko na ndio ilikuwa kilio kikubwa nchi nzima.
Tulitaka tupate serikali inayofuata sheria, inayojali kero za raia wake, afya za raia wake, ustawi wa raia wake na elimu bora na nafuu.

Ili haya yatokee kuna gharama zake pia, Tena kubwa, na saa nyingine chungu mno,
mifano Hai ipo sasa hivi live kila kona ya nchi.
Na hiyo ndio Gharama na thamani ya mabadiliko..

Tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika???

Ili hayo yote yatimizwe lazima serikali ifanye kazi bila upendeleo wala haya,(tayari JPM ameonyesha hilo). Bila kujali wewe nani au ndugu yake nani.... Sheria iwe msumeno wa kweli.

My take.
Kumezuka hivi karibuni kauli mbali mbali toka kwa viongozi wa sekta mbali mbali nchini, wa ndani na nje ya CCM, Tena wengine walikuwa viongozi waandamizi wa serikali ya awamu ya tano nk...

Hii ni ishara kwamba kuna kundi kubwa la watu ambao hawapendezwi na jinsi Rais anavyopambana na ufisadi na dhurma ilivyokuwa inaelekea kuangamiza utaifa wetu.

Wengi wa kundi hili ni kutoka hasa upinzani zaidi aka UKAWA hasa wakisukumwa na hasira za matumaini yao kuingia ikulu kukatizwa.
Na ndoto hiyo kuelekea kuyeyuka hasa kutokana na kukubalika kwa JPM kila uchao, ndani ya watanzania walio wengi.

Lakini pia wako kundi fulani ndani ya serikali na pia ndani ya chama cha CCM chenyewe.

Na hawatapenda kumuona akikabidhiwa uenyekiti wa CCM.(ingawa hawataweza kulizuia hilo lisitokee).

Wakati anaihama CCM, aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania ndg E. Lowassa na baadae kuwa mgombea Urais kupitia UKAWA. alinukuliwa Mara kadhaa akijinasibu kuwa na kundi kubwa la wafuasi ndani ya CCM ambao angehama nao.

Hatimae wako waliohama nae na Sina sababu ya kuwataja hapa maana ni historia sasa.

Wako wengi pia ambao walisita kumfuata kichwa kichwa, yaani walisita kwa sababu mbali mbali, kulingana na hali halisi ya wakati ule, kwani tukio na mazingira ya tukio ilikuwa ghafla na wengi hawakuwa wamejiandaa Rasmi..

Na sasa wanaweza kuwa na wasaa mzuri zaidi wa kujipanga na kujiandaa huku wakimharibia kasi Mh JPM . wakiwa ndani ya CCM bado

Hii ndio sababu ya mimi
kuomba kama mtanzania mpenda haki na mabadiliko ya kweli kutumia haki yangu kikatiba, kutoa angalizo hili.

Lakini angalizo langu kubwa kabisa ni kwamba wale team Lowassa wa mkutano mkuu wa dodoma, ni kwamba baadhi yao wako CCM kwa dhati.(na Hawa ndio wengi).

lakini baadhi yao wako CCM KIMWILI,lakini kimawazo na kivitendo wako kwa lowasa na UKAWA yake! Yaani ni wana CCM maslahi zaidi.(shame on them) time will tell and teach them a lesson.

Na Sina Shaka Hawa ndio virus zitakazomsumbua JPM kutimiza ahadi na Nia yake ya mabadiliko ya kweli.

Ni bora adui unaemuona na kumjua, kuliko adui usiemjua wala kumuona.

Chonde Chonde JPM, chukua chama mapema ukisafishe mapema kabla ngamia hajaingiza kichwa kwenye hema mara ya pili MUNGU akubariki JPM
1453487198062.jpg


MUNGU ibariki nchi yetu kipenzi cha wengi Tanzania.

Mbarikie afya njema Rais wetu Mh JPM, atuongoze vyema katika majukumu yake ya kila siku tunasema Amen
 
Ahsante kwa ushauri wa akili kubwa mkuu,ujumbe ataupata. Sina mashaka hatua sahihi atachukua,japo mamluki wanaomba siku hiyo isifike.
 
Tena wapo wengi sana na wanatumia hela walizowaibia watanzania kutaka kuvuruga CCM. Naona JK anawaogopo au ni mmoja wao kwani JPM alikwisha mwambia safisha chama lakini mpaka leo hii hakuna hata mmoja amefukuzwa.
 
Ahsante kwa ushauri wa akili kubwa mkuu,ujumbe ataupata. Sina mashaka hatua sahihi atachukua,japo mamluki wanaomba siku hiyo isifike.
Nakushukuru mkuu, tuko pamoja katika vita hii. Tatizo mafisadi na vitoto vyao humu ndani wanalazimisha, umiliki wa ufahamu wetu.
Lakini tuendelee kuna . kumuombea JPM
 
Tena wapo wengi sana na wanatumia hela walizowaibia watanzania kutaka kuvuruga CCM. Naona JK anawaogopo au ni mmoja wao kwani JPM alikwisha mwambia safisha chama lakini mpaka leo hii hakuna hata mmoja amefukuzwa.
Ghengis,
Haogopwi mtu hapa Bali ni suala la taratibu tu, lazima JPM akabidhiwe chama kwanza Ili apange safu ambayo ni Safi na yenye kuaminika kwa wananchi then ndio majipu ndani ya chama nayo ya tumbleweed.. Kama alivyoahidi JPM leo kule arusha wakati akisalimia wananchi.
 
Tena wapo wengi sana na wanatumia hela walizowaibia watanzania kutaka kuvuruga CCM. Naona JK anawaogopo au ni mmoja wao kwani JPM alikwisha mwambia safisha chama lakini mpaka leo hii hakuna hata mmoja amefukuzwa.
1453496504517.jpg

Mtu wa kazi ndani ya kazi
 
Ghengis,
Haogopwi mtu hapa Bali ni suala la taratibu tu, lazima JPM akabidhiwe chama kwanza Ili apange safu ambayo ni Safi na yenye kuaminika kwa wananchi ndio majipu ndani ya chama nayo yatumbuliwe Kama alivyoahidi JPM leo kule arusha wakati akisalimia wananchi.
1453496812643.jpg

Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Kwenye siasa hakunaga permanent enemies wala permanent friends

Mwaka 1995 Kikwete ana genge lake, Mkapa na kundi lake
mkapa akashinda.Kikwete akawa waziri wa mambo ya nje

Mwaka 2005 Team ya Kikwete ina Kingunge,Lowassa,

Nape NNauye team ya Sumaye pamoja na Mary Nagu

Magufuli sio team Kikwete .....na kadhalika

mwaka 2015.....Magufuli team ina Kikwete na Nape

Lowasa kingunge watoka CCM...

the list is long.....
 
Kwenye siasa hakunaga permanent enemies wala permanent friends

Mwaka 1995 Kikwete ana genge lake, Mkapa na kundi lake
mkapa akashinda.Kikwete akawa waziri wa mambo ya nje

Mwaka 2005 Team ya Kikwete ina Kingunge,Lowassa,

Nape NNauye team ya Sumaye pamoja na Mary Nagu

Magufuli sio team Kikwete .....na kadhalika

mwaka 2015.....Magufuli team ina Kikwete na Nape

Lowasa kingunge watoka CCM...

the list is long.....
America, yaani US... Alikuwepo Collin Powell, alihitilafiana na Rais kimtazamo,
Kilichofuatia ilibidi Rais kupangua safu yote ya waandamizi kutoka Republican na leo ni history... Remember that eeh?
 
America, yaani US... Alikuwepo Collin Powell, alihitilafiana na Rais kimtazamo,
Kilichofuatia ilibidi Rais kupangua safu yote ya waandamizi kutoka Republican na leo ni history... Remember that eeh?
Rais yupi huyo?
Powell hakuwahi fukuzwa
 
We ndo una changanya mambo
Powell ali serve term yake moja
toka mwanzo hakupanga ku serve term zaidi ya moja
Sio hakupanga, kwa sababu hata kuteuliwa hakupanga pia. Kauli yake moja tu ya kumkosoa Rais wake ndo iliyo mcost.
Na wenzetu wanafanya siasa za kweli. Kwa hiyo alijitambua na akafanya maamuzi sahihi, na siyo magumu kama tuitavyo hapa kwetu.
 
Watawafukuza vipi wakati Chenge na Ngeleja wamewapa kamati muhimu bungeni.. Na ndio vichwa vyao ndani ya chama.
 
Watawafukuza vipi wakati Chenge na Ngeleja wamewapa kamati muhimu bungeni.. Na ndio vichwa vyao ndani ya chama.
Bado hujanielewa vizuri, hata mimi nalielewa hilo, lakini wewe pia nuelewe.
Kwamba naomba akabidhiwe chama Ili afanye kazi ya kukisafisha
 
Back
Top Bottom