Magufuli/"tz Tajiri": KATANI (WHITE GOLD) ilichangia 65% ya uchumi, TZ ni ya pili duniani,

CHENGU MANURE

JF-Expert Member
May 26, 2015
914
566
Ukweli Kuhusu katani na umaskini wa kujitakia wa wetu.

1.KATANI ILIINGIAJE NCHINI
715px-StateLibQld_1_234584_South_Sea_Islander_workers_on_the_Lower_Herbert.jpg

sisal4.jpg

(maktaba)

Mwaka 1893 mkulima wa kijerumani alitoka Mexico na miche 1000 kwa bahati mbaya au nzuri zilikubali kuota miche 63 tu. Hizi ndio zimekufanya kuona mashamba makubwa tanzania na afrika kwa ujumla. Kustawi kwake kuliifanya tanzania kupanda thamani kwa kazi sana machoni mwa mkoloni, Ndio miongoni mwa sababu ya kujengwa kwa reli unazotaka kuziboresha reli ya kati na tanga. Zao hili linapatikana mabara matatu tu duniani. Miaka ya 60 zao hili lilichangia hadi 65% ya uchumi wa taifa.


2. MATUMIZI YAKE NA MANUFAA KWA TAIFA,

Elimu Bure: grade ya chini inatumika kutengeneza makaratasi, mbao spesho za kufundishia etc.
Viwandani:Inamatumizi makubwa sana viwandani hasa viwanda vya nguo. pia inatumika katika hatua mbalimbali za utengenezaji wa magali, boti, carpets n.k,
y1873e0u.jpg
JECM46_FEATURE_uniroma_The-Mercedes-E-Class-fig2_composites.jpg

Kilimo: Mbolea, baadhi ya mabaki huboreshwa na kuwa chakula cha mifugo, kamba n.k

Mabaki yake: yanatengeneza BIOGAS (umeme usioharibu mazingira), Madawa ya hospitalini(juice), kwa stage fulani yanatumika katika viwanda vya saruji kutengeneza saruji za bei ya chini ili kusaidia makazi wa watu wa kipato cha chini.
arusha-jun14-promotion-of-renewable-energy-technologies-in-tanzania-11-638.jpg

NYUZi - za katani ni zaidi ya lulu duniani kwa sasa na zinategemewa kwa kiwango kikubwa.
sisal-runner-sydney-terra.jpg
sisal_desk.jpg

kwa ufupi katani hutumika katika engineering, ujenzi, kuetngeneza karatasi na plastic.

TAKWIMU ZA AJABU
sisal7.jpg


Tanzania ni ya pili duniani kwa kuzalisha katani. Ya kwanza ni Brazil, na ukitoka Tanzania inafuata China baadae kenya. (wikipedia 2007)
Lakini kwa takwimu za FAO, export brazil inaexport100,000Tonnes, Kenya 20,000 tones na Tanzania 15,000.

NINI KIFANYIKE,
Inabidi kama serikali na kupitia bodi za katani pia. Kwa sababu Moshi wa ukombozi unafuka kwa mbali tangu magufuli aSHIKE USUKANI. Mapinduzi ya lazima na haraka katika kilimo yafanyike na Dhahabu hii nyeupe izalishwa kwa wingi, malaki ya maekali yaliyolala yaamshwe ni wakati wa kuiinua Tanzania. Mazao na faida ya hii product zianzie hapa hapa kwetu pia.

ALIIONA HII FURSA WAKATI IKIWA HAINA THAMANI leo BILLIONEA Mtanzania
hqdefault.jpg
DSC_0262.jpg


Uvumbuzi wa nyuzi za plastic/synthetic fibers za bei rahisi zilishusha kabisa soko la katani, makampuni mengi yaliteteleka, Mo Dewji ni miongoni mwa wachache walioamini kuwa hali itakuja kuwa nzuri, Leo hii ameajiri maelfu ya watanzania, amewajengea mahapa pa kulala mashambani, sehemu za afya, anasafirisha 1/3 ya katani yote ya tz na anakili ni biashara nzuri. Ni mfano mzuri wa kuigwa sana.


Mwisho:
Naiona tanzania kama tajiri aliyelala na badala ya kuamswa amekuwa akibembelezwa aendelee kulala huku anafirisiwa. Leo umetokea Magufuli unaonyesha hali ya kumuamsha Tanzania. Watanzania wako pamoja kufanya kazi na wewe, Uchaguzi umepita, UKAWA watafanya kwa nafasi yao kusaidia kuiamsha tanzania, wananchi watafanya sehemu yao na wanaCCM wabadilike na kukuunga mkono waache mambo ya "ccm ni ile ile". Kila mtanzania atimize wajibu wake.

Pia Trend ya Dunia katika kilimo inaonyesha, miaka michache ijayo Dunia nzima afrika itakuwa Mzalishaji tegemewa wa chakula cha dunia. Tanznia imejaa ardhi Bikra kila kona. Hivyo basi kilimo ni Ajira ambayo mkataba ni commitment. Naungana na Billionea wa zimbabwe aliyewekeza katika Mawasiliano/telecom Strive Masiyiwa, "Nikiambiwa nianze upya biashara leo, niachagua kilimo".
Napendekeza kila kijana mjini na vijijini wamiliki angalau Hekari Moja.


unakaribishwa kwa maoni chanya.
 
[h=1]Sisal: The most useful plant you've never heard of[/h]http://edition.cnn.com/2015/11/10/africa/sisal-tanzania/index.html
 
"POVERTY IS UNJUSTFIABLE BURDEN" Jewish view of poverty

Haiwezekani mtu atoke Ghuba ya Yucatan mexico (sio kwao yeye ni mjerumani Dr Richard Hindorf), 1892,Asafiri na miche 1000 tena kinyume na sheria zao miezi kadhaa, akafika ujerumani Humburg miche 800 yote imekufa imebaki 200. Hakukata tamaa akasafiri nazo Miezi mingi tu hadi bandari ya tanga zikafa 138 zikabaki 62. Kapanda mwenyewe kwa mikono yake zote kijiji cha Kihongwe na baadae bushiri.
Leo Miche 62 imesambaa nchi nzima na afrika nzima kwa ujumla. Thamani ya zao hili sio ya kuelezeka lakini bado tunalalamikia umaskini huuhuu toka enzi hizo. Kijana mtanzania wa leo bado anaogopa kwenda hata kijiji cha karibu na dsm Ruvu kulima.
 
"POVERTY IS UNJUSTFIABLE BURDEN" Jewish view of poverty

Haiwezekani mtu atoke Ghuba ya Yucatan mexico (sio kwao yeye ni mjerumani Dr Richard Hindorf), 1892,Asafiri na miche 1000 tena kinyume na sheria zao miezi kadhaa, akafika ujerumani Humburg miche 800 yote imekufa imebaki 200. Hakukata tamaa akasafiri nazo Miezi mingi tu hadi bandari ya tanga zikafa 138 zikabaki 62. Kapanda mwenyewe kwa mikono yake zote kijiji cha Kihongwe na baadae bushiri.
Leo Miche 62 imesambaa nchi nzima na afrika nzima kwa ujumla. Thamani ya zao hili sio ya kuelezeka lakini bado tunalalamikia umaskini huuhuu toka enzi hizo. Kijana mtanzania wa leo bado anaogopa kwenda hata kijiji cha karibu na dsm Ruvu kulima.

Thank you
 
Ni kweli mkuu...binafsi nyumbani ni Tanga,Mo Dewji ana mashamba mengi sana ya katani...kuanzia korogwe mpaka mazinde..ni estates..na ameajiri wengi kupitia haya mashamba..

Siku hizi katani ni inshu..ukiweka oda kiwandani labda tani moja ya kamba itabidi uwe mvumilivu..wana oda nyingi sana...na bei inapanda kila siku..
 
Zitto alikuja na mswada kule bungeni mwaka 2012
Wabunge wa tanga wakapinga bila sababu za msingi kisa itampa umaarufu kisiasa.
Tungeanza kufufua ule mwaka,mwaka huu tungeanza kuvuna.

Wanasiasa wanaua uchumi wa nchi hii
 
Miche yake inapatikana wapi na kwa bei gani? Na soko likoje? Mnunuzi ananunua kwa kilo au kwa tani? Msaada tafadhari.
 
Zitto alikuja na mswada kule bungeni mwaka 2012
Wabunge wa tanga wakapinga bila sababu za msingi kisa itampa umaarufu kisiasa.
Tungeanza kufufua ule mwaka,mwaka huu tungeanza kuvuna.

Wanasiasa wanaua uchumi wa nchi hii

Ndio shida yetu watanzania, tunaendekeza sana itikadi za siasa.
Mtu yupo tayari kuua mradi kisa utampa umaarufu mpinzani
 
"POVERTY IS UNJUSTFIABLE BURDEN" Jewish view of poverty

Haiwezekani mtu atoke Ghuba ya Yucatan mexico (sio kwao yeye ni mjerumani Dr Richard Hindorf), 1892,Asafiri na miche 1000 tena kinyume na sheria zao miezi kadhaa, akafika ujerumani Humburg miche 800 yote imekufa imebaki 200. Hakukata tamaa akasafiri nazo Miezi mingi tu hadi bandari ya tanga zikafa 138 zikabaki 62. Kapanda mwenyewe kwa mikono yake zote kijiji chawss w w Kihongwe na baadae bushiri.
Leo Miche 62 imesambaa nczzhi nzima na afrika nzima kwa ujumla. Thamani ya zao hili sio ya kuelezeka lakini bado tunalalamikia umaskini huuhuu toka enzi hizo. Kijana mtanzania wa leo bado awnaogopa kwenda hata kijiji cha karibu na dsm Ruvu kulima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom