Uchaguzi 2020 Magufuli: Tulikuwa tumekosa 'connection', hamkuwa na msemaji na ni makosa ya kuchagua kwa jazba

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Kampeni zinaendelea nchini na sasa Magufuli yuko Mbalizi amesimama kusalimia wananchi waliokusanyika barabarani akielekea Songwe. Baada ya kuongelea mengi pia ameongelea hali ya sekta ya maji Mbalizi na kusema kuna kipindi alipita eneo husika na alikuta tatizo la maji na wakaamua bilioni tatu zitolewe na ameambiwa mradi ni wa mserereko na maji yameanza kuja na kilichobaki ni kuyasambaza. Akaendele...

MAGUFULI: Lakini lazima niwaambie niwaambie ndugu zangu wa Mbalizi, tulikuwa tumekosa connection, hamkuwa na msemaji na haya ndio makosa ya kuchagua kwa jazba. Mliniletea madiwani wa vyama vingine hapa, nasema uongo? Haya ndio huwa ni malipo yake na mimi wana-Mbalizi lazima niwaambie ukweli.

Kufanya kosa ni kosa, kurudia kosa? Nawaomba mwaka huu mfanye mabadiliko makubwa.

Hapa napajua, ni mahali pa biashara, watu wana vision nzuri, watu wana muelekeo mzuri lakini mnajichelewesha saa nyingine ndugu zangu na ndio maana suala la maji hakuna mtu aliyekuja kuniambia mpaka siku nilipopita hapa, sasa mwaka huu mniletee madiwani wa CCM kwa sababu maendeleo hayana chama.

Tunachowaomba ndugu zangu wa Mbalizi, maendeleo hayana chama ingawaje maendeleo ya kweli yatatokana na chama kinachojua maana ya maendeleo ni nini na chama hicho ni chama cha mapinduzi ambapo tumeyanakili yote yanayotakiwa kufanywa katika kitabu hiki cha ilani ya uchaguzi.

Hakuna chama chochote katika wagombeaji mtakaowakuta mambo yao wameyapanga katika kurasa 303 watakayoyatekeleza, wakipita hapa waonyesheni muwaombe, tuonyeshe ilani ya uchaguzi yao ina kurasa ngapi, sisi ni kurasa 303 maana yake yale tuliyafanya katika miaka mitano tumeongeza mara mbili zaidi ili Tanzania hii ibadilike.

Ninafahamu mna changamoto, moja ya changamoto ni ombi la barabara ya Mbalizi-Shigamba kilomita 52, hii barabara nimeshaipitia mimi. Mtampa kura lakini kweli huyu mbunge? mtawapa na madiwani? Kweli watu wa Mbalizi mtafanya hivyo? Au mnanizungumzia hapa nitoke nimefurahi alafu baadae mnafanya mambo yenu?

Wangapi watampa mbunge kwanza tukubaliane na Mungu anawaomna mmenyoosha mikono na wangapi watawapa madiwani pamoja na diwani wa hapa? Mnafanya mabadiliko? (Wananchi: Ndiooo)

Haya wasaidizi wangu naomba muandike hii, hii barabara ya Mbalizi-Sigamba kilomita 52 baada ya uchaguzi tukishamaliza, kipindi kinachokuja, mimi naji-commit mwenyewe mbele ya wananchi wa Mbalizi, tutaitengeneza kwa kiwango cha lami.

Kule Dar es Salaam nilipowaambia tutajenga maflyover mengi hata zaidi ya matano hawakuamini, hakuna aliemini kwamba unaweza ukapitisha gari ghorofa la tatu, mita zaidi ya 15 lakini leo ni mashahidi, tumeibadilisha Dar es Salaam, tumeweka pale zaidi ya bilioni 660. Hakuna cha msongamano au mtoto wa msongamono utatokea tena.

Ukweli unabaki kuwa ukweli, mahali ambapo hawajakuchagua haina tofauti na ukawa na watoto. Huwezi ukashibisha kwanza watoto wa nje kabla hujashibisha watoto wako wa kuzaa na watoto wangu wa kuzaa ni CCM.
 
Kampeni zinaendelea nchini na sasa Magufuli yuko Mbalizi amesimama kusalimia wananchi waliokusanyika barabarani akielekea Songwe. Baada ya kuongelea mengi pia ameongelea hali ya sekta ya maji Mbalizi na kusema kuna kipindi alipita eneo husika na alikuta tatizo la maji na wakaamua bilioni tatu zitolewe na ameambiwa mradi ni wa mserereko na maji yameanza kuja na kilichobaki ni kuyasambaza. Akaendele...

MAGUFULI: Lakini lazima niwaambie niwaambie ndugu zangu wa Mbalizi, tulikuwa tumekosa connection, hamkuwa na msemaji na haya ndio makosa ya kuchagua kwa jazba. Mliniletea madiwani wa vyama vingine hapa, nasema uongo? Haya ndio huwa ni malipo yake na mimi wana-Mbalizi lazima niwaambie ukweli.

Kufanya kosa ni kosa, kurudia kosa? Nawaomba mwaka huu mfanye mabadiliko makubwa.

Duh, kwahiyo watu wa mbalizi walinyimwa maji kwasababu ya kuchagua kiongozi wa upinzani?

Bado safari ni ndefu
Ukisikia connection juwa ni rushwa aka 10% wata Pelekaje pesa huko ambazo CCM hawapati pesa hko aka connection
 
  • Thanks
Reactions: Paa
hii nchi sijawah kuilewa kiukweli kama ndo hvo mbona anakusanya kodi hadi uko mbalizi. Huu ujinga sana maana huyu kichaa anataka kuona hii chi ni ya babaake na mamaake shubaamit
Ina huzunisha sana kuwa na Rais kama huyu
 
Chato , buseresere, katoro hakuna maji hawana connection? Huyu baba ni muongo muogopeni Kama ukoma.
Mbunge wa Mbeya vijijini ni wa Ccm lakini anawasimanga wananchi kwa hao madiwani wachache wa upinzani,amesahau jana kawasimanga Mbeya mjini kwa ajili ya kuwa na mbunge wa upinzani akasahau kuwa madiwani wa Ccm walikuwa wengi zaidi baada ya wale wa upinzani kuunga juhudi.
 
Back
Top Bottom