Magufuli siyo dikteta, hajawahi kuwa dikteta na hana mpango wa kuwa dikteta

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Wanajf habari za frustrations za maisha?

Kuna habari zisizo za ukweli zinamchafua Rais wa Tanzania kuwa ni dikteta, nitaweka sababu zangu za kwanini magufuli siyo Dikteta,

1.Vijana wengi wamezaliwa kipindi cha Mkapa hawaqkujitambua na wamejitambua na kujua mambo ya siasa kipindi cha Kikwete, Kwa bahati mbaya Tanzania huwa tuna Miaka kumi ya kazi na miaka kumi ya likizo, wenye akili mmenielewa, Kwa mtu aliyeongozwa na Nyerere, Aliyeongozwa na Mkapa na ambaye kaongozwa na Magufuli atajua nasema nini,

Najiuliza kwanini Moringe Sokoine au Mrema hawajawahi kuitwa madikteta wakati ukali wao ulipitiliza mpaka kwa Magufuli? Au ni kwakuwa hawakuwa marais udikteta tunaupima kwa upande wa Rais tu?

2. Watanzania wengi ni wazembe hasa kizazi cha smart phones, wanataka mziki masikioni hawataki kufanya kazi wanataka kuwa wakukaa nyumbani tu na kulishwa tu bila kutumika ipasavyo,
hivo anapotokea mtu wa kuwarudisha kwenye reli lazima mseme ni dikteta,

3.Kupuuza sheria ulikuwa ni mchezo uliozoeleka Tanzania na kupuuzaa taratibu za nchi sasa akija Chuma cha kuwanyoosha wanasema ni dikteta

4. DW ni ka media ka propaganda za kijinga sana na hawana hoja za msingi kusema magufuli ni Dikteta, si wajiulize swali je Magufuli ameshafika hata robo ya Hitler? aliyekuwa rais wao? wanawashwa nini na mambo yasiyowahusu?

KUPITIA MATENDO HAYA YA MAGUFULI NAJUA KWAMBA HUYU MZEE SI DIKTETA KAMA WANAVYOSEMA

1.Hakuna Dikteta anapendwa na watu wake kama Magufuli wanavyompenda,

2.Hakuna kiongozi ambaye ni dikteta ambaye anaweza kutamaniwa na nchi jirani kuwa kiongozi wao, ni kama mabavyo Tanzania hatukuwahi kutamani iutawaliwa na AHMED KHAZAI au Idd amini Au mobutu, lakin uko nje watu wanapigana vikumbo kumjua na kumtaka Magufulia aongoze walau siku kadhaa nchini mwao

3. Dikteta hawezi kukuacha umemuotea kufa

4.Dikteta hawezi kukuacha umekwamisha michakato ya maendeleo

5.Dikteta hawezi kuyakuta magari bandarini yanayojifanya kutokuwa na mwenyewe akayaacha lazima ayagawe bure au apeleke kijijini kwake,

6.Dikteta hawezi kubana matumizi akajenga hosteli halafu wachache wakapotosha kwamba kuna expansion joint halafu akawaacha wanazagaa huyo ni dikteta gani sasa?

7.Dikteta hasingeacha media ziendelee kuandika ukwasi juu yake au habari hasiyopenda yeye, mfano ni Rwanda au Pakistani kaulize kama kuna ujinga uo, navyokwambia kuna website hazifanyi kazi uko wala whatsap calls hakuna na hazina end to end encryption

8.Dikteta hawezi akakuuliza swali ukajibu hovyo kama yule wa Bukoba akakuacha

9.Zaidi dikteta hawezi maliza miezi 24 madarakani bila kuua mtu hadharani kuwatisha wengine

10.Dikteta hawezi husisha vyombo vingine katika maamuzi ya juu mfano Bunge na mahakama

11. Dikteta gani atavumilia meya aseme amepokea simu yake ya kumrubuni Mnyika na atamuaibisha? labda awe dikteta uchwara , narudia Magufuli si dikteta

Magufuli si dikteta ila anawanyoosha tu

Brittany
 
Enzi zote hizo hakuwahi kutokea raisi anayehubiri Watanzania kuishi kama mashetani,kkuwazodoa waliopata majanga kama lile tetemeko la Ardhi Bukoba wala raisi aliyehimiza wapinzani washughulikiwe na spika bungeni halafu yeye atawashughulikia nje ya bunge na ikatokea Mbunge akapigwa risasi mchana mweupe kwenye majengo ya serikali na wanakoishi viongozi!!!

Cha kujiuliza kwa nini Nyerere hakulalamikiwa kushinda huyo anayetajwa?! Kwa nini sio Mkapa na maneno yake ya wivu wa kike na malofa?! Kwa nini sio Kikwete?!

Ninachoamini tutaweka historia ya kuwa na kiongozi ambaye ataiacha nchi ikiwa fukara wa kutupwa kwani huwezi kukuza uchumi kwa kuua sekta binafsi na bila ya kuanzia kwenye microeconomics!!!
 
Hii yote ni madhara ya kuwa na rais uchwara a.k.a. Kikwete. Aliwabwetekea sana vijana na wananchi wasiojitambua kiakili wajihusishe na ujinga ili yeye na kundi lake ajihusishe na wizi wa rasilimali zetu.

Alipokaribia kuachia nchi akawaambia wananchi wale wale (Vijana na wasiojitambua kiakili) kuwa nimewatumia kwa kunipigia kura na sasa naondoka, mtanikumbuka.

Aliwapiga dongo la ajabu sana kiaisi kwamba hawajitambui tena na hawajuwi wapi pa kwenda wakati mshua wao yuko Mzoga anakula raha zake mwenyewe.

Kikwete aliwaharibu sana vijana kutaka washabikie ujinga wa bongo fleva na taarab mpaka sasa karibia ya vijana wengi wa Dar wanashikishwa ukuta kwa ajili yake.
 
Hii yote ni madhara ya kuwa na rais uchwara a.k.a. Kikwete. Aliwabwetekea sana vijana na wananchi wasiojitambua kiakili wajihusishe na ujinga ili yeye na kundi lake ajihusishe na wizi wa rasilimali zetu. Alipokaribia kuachia nchi akawaambia wananchi wale wale (Vijana na wasiojitambua kiakili) kuwa nimewatumia kwa kunipigia kura na sasa naondoka, mtanikumbuka. Aliwapiga dongo la hajabu sana kiaisi kwamba hawajitambui tena na hawajuwi wapi pa kwenda wakati mshua wao yuko Mzoga anakula raha zake mwenyewe. Kikwete aliwaharibu sana vijana kutaka washabikie ujinga wa bongo fleva na taarab mpaka sasa karibia ya vijana wengi wa Dar wanashikishwa ukuta kwa ajili yake.
umeona hiyo ni kweli tupu
 
Back
Top Bottom