Magufuli-Sipaswi kulaumiwa kwa bomoabomoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli-Sipaswi kulaumiwa kwa bomoabomoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jul 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Ujenzi, John Magufuli


  Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, amesema hapaswi kulaumiwa katika suala bomoboa kwa watu waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara kwani sheria zimetungwa na wabunge na kupitishwa na wao wenyewe.

  Alisema hayo jana bungeni wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya Makadirio na Matumizi ya wizara yake.

  Alisema Sheria inasema mtu asijenge ndani ya mita 30 kutoka barabara kuu hivyo sheria hiyo lazima ifuatwe.

  Akitoa mfano alisema hata jengo la Shirika la Umeme (Tanesco) lilipo Ubungo jijini Dar es Salaam, lipo ndani ya hifadhi ya barabara hivyo litabomolewa.

  Alisema pamoja na watu kupinga kuhusu kubomolewa kwa jengo hilo lakini kwa mujibu wa sheria lazima litabomolewa.

  “Hata kama halitabomolewa leo, lazima libomolewe tu kwa sababu limo ndani ya hifadhi ya barabara, hata akija mtu mwingine, litabomolewa tu,” alisisitiza.

  Magufuli alisema hata yeye jimboni kwake alibomoa nyumba 157 na alijua kabisa kwa hatua hiyo hatapigiwa kura katika uchaguzi wa wabunge, lakini wanaume na wake zao, walimpa kura na kupita bila kupingwa.

  Aliongeza kuwa kuna Watanzania wanaoelewa sheria na wanapenda maendeleo ndio maana hata zoezi hilo linapowakuta huwa tayari kulipokea.

  Kuhusu suala la kiasi gani serikali inadaiwa na wakandarasi wa barabara mpaka sasa, lililouliwa na Andrew Chenge, Magufuli alisema mpaka kufikia mwaka 2011 kulikuwa na deni la Sh. bilioni 320.

  Alifafanua kuwa wiki iliyopita serikali ilikuwa imeshalipa Sh bilioni 300 na fedha iliyobaki haizidi Sh bilioni 50 ambazo wanatarajia kulipa ifikapo mwisho wa mwezi huu.

  Aliwashauri makandarasi wanaoidai serikali kupeleka vyetu vyao kwa wataalamu kwa uhakiki ili waweze kulipwa haraka.

  Aliwataka wapeleke vyeti hivyo kwa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad), wizarani na Hazina.

  Bunge liliidhinisha bajeti hiyo ya Sh. 693,948,272,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo
  .  CHANZO: NIPASHE

   
Loading...