Uchaguzi 2020 Magufuli si mgombea wa Tanzania pekee bali Afrika nzima inamuhitaji

Hakuna wanakomhitaji hata bure maana atakuwa mzigo usiobebeka. Ni Chama chake ndo kinatubebesha mzigo usio na manufaa yoyote ulitakiwa utupwe mahali uchomwe Moto majivu yatupwe baharini. Hafai kuishi kati ya watu!
CCM bila Polisiccm bila Tumeccm bila mahakamaccm bila wakurugenziccm bila Msajiliccm bila uchakachuaji bila wizi wa kura ni weupe sana
 
Mchakato wa kurekebisha sheria ili mikataba ya madini inufaishe taifa, Chadema mlipinga. Mchakato wa kuzinasua ndege za ATCL kutoka kwa mabeberu, chadema mlihujumu. Mchakato wa kuzuia hila za mabeberu katika vita dhidi ya Korona, Chadema mlihujumu. Hicho ni kipimo tosha kwamba hamna nia ya dhati ns Taifa hili hivyo hamuaminiki kupewa madaraka
Tanzania ni Nchi yenye rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani ni Nchi ilipaswa iwe tajiri kuliko America kama siyo CCM mda huu Tanzania ingekuwa ni Nchi tajiri mno lakini CCM wameifirisi Nchi kwa kuchukua pesa za viwanda pesa za maendeleo zinatumika kudidimiza demokrasia kudhoofisha kuihujumu chadema hawataki maendeleo
 
Hahaaaa, mwenye akili timamu na ufahamu, atamchagua Magufuli

Makundi ya mashoga, makundi ya vyeti feki, wapiga dili, makundi ya ulaji wa mishahara hewa, makundi ya ujangili wa wanyama pori, makundi ya wezi wa madini, makundi ya vibaraka wa mabeberu. Hayo kweli, yameumizwa. Mitano tena ili ayateketeze kabisaaa
Wapiga dili wapo CCM ndiyo maana kuna wizi wa trilion 1.5 mkamtoa kafara CAG, kuna wizi ufisadi kwenye ununuzi wa Ndege ujenzi wa SGR bwawa la umeme, wapiga dili wamezidi utawala huu kuna ufisadi wa kutisha ndiyo maana wakakosa pesa za nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma pesa zote zinaibiwa na wajanja wachache ukiwemo wewe mvuta Bangi, Mbona makonda Bashite alipiga kelele juu ya ushoga ukakaa kimya na wabunge wa CCM wakiwa Bungeni wakampinga Bashite wakiongozwa na Kange lugola , CCM wanaupenda ushoga ndiyo maana wabunge hawajawahi kutunga Sheria kali dhidi ya ushoga
 
Tanzania IPO katika nchakato wa Uchaguzi Mkuu, miongoni mwa wagombea URAIS ni Mheshimiwa Daktari John Joseph Pombe Magufuli.

Rekodi alizovunja Mheshimiwa JPM nchini Tanzania, Afrika na dunia nzima, zinamfanya asiwe mgombea wa Tanzania pekee Bali tegemeo LA Afrika kama mfano wa Kiongozi bora, shupavu, jasiri, Mzalendo na Mchapakazi.

Katika nchi nyingi, RAIA na viongozi wanamtazama Magufuli kama kiongozi bora wa mfano wa kuigwa katika ulinzi wa Rasilimali na Maendeleo ya nchi.

Tungekuwa na uchaguzi wa RAIS wa Afrika, JPM angeshinda kwa kura nyingi maana Afrika inamhitaji kuliko yeye anavyoihitaji Afrika.

Hizi rekodi zake haziwezi kufikiwa na Rais mwingine yeyote wa Afrika hivyo kumpambanua kama kiongozi bora wa karne hii:
1. Kuongoza nchi ya kiafrika kwa miaka mitano bila kukanyaga Ulaya, Amerika wala Asia hivyo kupunguza gharama za uendeshaji serikalini na kuepuka mikataba ya uporaji rasilimali za nchi.
2. Kuzuia safari za nje kwa viongozi na watumishi wa umma ili viongozi wawatumikie wananchi
3. Kudhibiti biashara ya madawa ya kulevya nchini
4. Kudhibiti ujangili hivyo kulinda rasilimali za nchi na kukuza utalii
5. Kujenga ukuta ili kulinda rasilimali madini, matunda yake ni upatikanaji wa mawe makubwa ya Tanzanite kupitia mtanzania Laizer. Tanzania itaongoza kwa uuzaji wa Tanzanite tofauti na awali ambako Kenya, Afrika ya kusini na India zilijinufaisha kutuibia madini hayo. Faida ya ukuta huo ni kuongeza pato LA Taiga, ajira na kukuza uchumi.
6. Kutumia wasomi na Elimu zao kwa maendeleo ya nchi bila kujali itikadi. Mfano Prof. Kitila, Kafulila, Mtatito
7. Kufufua shirika LA ndege kwa kutumia cash money, Nchi kumiliki ndege zake ni usalama kwa nchi, na kukuza uchumi kupitia ajira na biadhara.
8. Kubadili mfumo wa mashirika ya umma kutoka kuomba ruzuku hadi kutoa gawio. Mashirika yetu sasa kama TTCL, STAMICO, TANAPA, KADCO, yanajiendesha kwa faida na gawio lake hutumika kukenga miundo mbinu na kuboresha huduma za jamii kama Elimu, maji, usafiri na afya.
9. Kusimamia uwajibikaji wa viongozi wa umma. Viongozi kwa sasa huudumia RAIA na kutatua kero zao.RAIA anaweza kuongea na mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, mkurugenzj au waziri na kutatuliwa kero yake.
10. Kuwaminya mabeberu hadi kukubali kukaa meza ya mazungumzo ili kutupatia Hisa na gawio LA mapato ya madini. Mwezi huu Oktoba, tumepata gawio LA bilioni 100 kutokana na faida ya madini.
11. Kuboresha miundo mbinu na usafiri wa anga, barabara, majini na reli. Nchi nzima imejengwa na kazi inaendelea
12. Kukomesha mgao wa umeme na kuongeza uzalishaji wa umeme. Mchezo wa kufungulia mabwawa ili kutengeneza mgawo wa umeme, umedhibitiwa. Mradi wa Stiglers Gorge ukikamilika, nchi itauza umeme nchi.
13. Kupambana na Covid-19 kidete hadi kuirejesha Tanzania katika hali ya kawaida na sasa maisha yanaendelea vyema. Nchi jirani mpaka sasa hawajafungua shule wala vyuo na uzalishaji umeshuka
14. Kuimarisha mifumo ya Uthibiti ubora wa Elimu kwa kuimarisha NACTE, NECTA, SQA, TCU n.k. Elimu inazidi kuimarika
15. Kuimarisha huduma za afya na Bima ya Afya, sasa hivi wenye bima wanapokelewa kama wafalme hospitalini, zamani tuliwekwa benchi. Hospitali zetu sasa zinapandikiza figo na kufanya upasuaji mkubwa. Hatuhitaji tena kupeleka wagonjwa India kama zamani.
16. Kuimarisha michezo na usimamizi hivyo wachezaji wananufaika na jasho lao na timu zetu zinafanya vizuri. Ndani ya miaka mitano ya JPM Tanzania imecheza AFCON, ilifuzu CHAN, simba ilifika robo fainali. Soko LA soka mpira biriani kwa afrika mashariki na kati ni Tanzania na nchi yetu ndiyo yenye ligi bora zaidi.
17. Heshima ya Tanzania kama Taifa imerejea, hakuna Nchi inayotuchezea tena. Mipaka IPO salama na tunatembea kifua mbele ndani na nje ya Afrika.
18. Kilimo kimeimarishwa hivyo nchi imeongeza uzalishaji, hakuna njaa tena nchini. Tanzania ndiyo inayouzia chakula mashirika ya umoja wa mataifa.
19. Imani ya wananchi kwa CCM imeongezeka na sasa wana CCM wanazaa sare zao hadharani tofauti na 2013-2014 ambako MTU angepita na sare ya CCM, angezomewa au ingechanwa.
20. Mheshimiwa Magufuli ni Mgombea jasiri, mzalendo na Mchapakazi, yupo kwaajili ya maslahi ya nchi na maendeleo ya Nchi. AMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUSONGE NAYE PAMOJA (2020-2025) KWA KUMPIGIA KURA ZA KUTOSHA OKTOBA 28.
Kwa sababu hizo na zinginezo, Waafrika wanatutegemea sana watanzania tumpe Ushindi wa Kishindo DR. JPM kwa ustawi wa Tanzania na Afrika nzima. CHAGUA JPM, CHAGUA MAENDELEO.
Aende huko huko wanako muhitaji atuachie nchi yetu.
 
Mchakato wa kurekebisha sheria ili mikataba ya madini inufaishe taifa, Chadema mlipinga. Mchakato wa kuzinasua ndege za ATCL kutoka kwa mabeberu, chadema mlihujumu. Mchakato wa kuzuia hila za mabeberu katika vita dhidi ya Korona, Chadema mlihujumu. Hicho ni kipimo tosha kwamba hamna nia ya dhati ns Taifa hili hivyo hamuaminiki kupewa madaraka
Mkienda kuomba omba misaada ulaya huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa upumbavu wizi ufisadi udikiteta wa CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike
 
Aende huko huko wanako muhitaji atuachie nchi yetu.
Nchi yako ipi? aende wapi? Acha kuvuta Bangi kukariri ujinga kwa cyprian Musiba kisha kuja kusumbua watu mitandaoni? Kwani bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi angefikaje huko ulaya? acha ushetani wako
 
Kwa kusema tu ni mengi ameweza ni ushahidi wa ubora wake, tukimpa miaka mingine mitano atatatua hizo changamoto. Zamani ulikuwa ukienda Hospitali kwa kadi ya bima, unawekwa kando ili wahudumiwe wenye cash kwanza. Hata ukihudumiwa ilikuwa unaandikiwa dawa ukanunue,
Saivi huduma za bima ya afya ni bambam. Waelimishe na wengine wasipotoshwe na mabeberu
Alisema tukimpa madaraka tutalimia meno.Hayo tumeona,Nakuhakikishia tukirogwa kumpa tena awamu hii tutalimia ulimi.Siwezi kushiriki dhambi hiyo.
 
Umemaliza kila kitu mkuu,huyu jamaa sioni mfano wake Afrika.Wakati ule ilikuwa ni aibu sana ukifika ughaibuni kujitambulisha kuwa unatoka Tanzania,sasa hivi unazungumza kwa herufi kubwa,"am from Tanzania",kama haelewi unamuuliza "do you know John Pombe Magufuli",utasikia "ok,now i understand,welcome sir"kiujumla we are in another level,huyu jamaa by hooks and crooks lazima tuhakikishe anapita bila kupingwa...
Wewe ni mnufaika wa kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi wapinzani kwani umejitoa fahamu kwa kiwango cha kutisha
 
Afrika nzima inamuhitaji mtu ambae hawezi hata kuendesha kikao cha SADC?Magufuli is a country bumpkin
 
Kamtendea nani ubaya?, usisikilize porojo za mtaani
Wewe ni mnufaika wa blackmail kuwabambikia kesi wafanyabiashara unapata pesa kwa njia haramu ndiyo maana unatetea udikiteta ili uendelee kujinufaisha kwa njia haramu za kishetani
 
Mchakato wa kurekebisha sheria ili mikataba ya madini inufaishe taifa, Chadema mlipinga. Mchakato wa kuzinasua ndege za ATCL kutoka kwa mabeberu, chadema mlihujumu. Mchakato wa kuzuia hila za mabeberu katika vita dhidi ya Korona, Chadema mlihujumu. Hicho ni kipimo tosha kwamba hamna nia ya dhati ns Taifa hili hivyo hamuaminiki kupewa madaraka
Watakuja kukujibu Kimhemko na jazba
Wanaotaka dola kwa maslahi binafsi ni wengi lakini wenye uzalendo ni wengi zaidi
 
Watakuja kukujibu Kimhemko na jazba
Wanaotaka dola kwa maslahi binafsi ni wengi lakini wenye uzalendo ni wengi zaidi
Wenye masilahi binafsi wamekula 10% ununuzi wa Ndege ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge wamekula trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara, bilion 12 matibabu ya Ndungai India , mihemko ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani?
 
Mchakato wa kurekebisha sheria ili mikataba ya madini inufaishe taifa, Chadema mlipinga. Mchakato wa kuzinasua ndege za ATCL kutoka kwa mabeberu, chadema mlihujumu. Mchakato wa kuzuia hila za mabeberu katika vita dhidi ya Korona, Chadema mlihujumu. Hicho ni kipimo tosha kwamba hamna nia ya dhati ns Taifa hili hivyo hamuaminiki kupewa madaraka
Mikataba mipya ya madini ni siri kubwa haina manufaa yeyote kwa Tanzania kwani hakuna ajuaye undani wake zaidi ya kuwahadaa watanzania na sinema za uongo, hapo kuna ufisadi mkubwa akiingia Rais mpya ndipo zitaibuka kashifa za kila aina
 
Niwe muwazi tu, 2015 nilimpigia...lakini this time Hapana.....katili sana JPM
MTU anyetaka Kukuua kwangu mimi hata kama mzuri vipi,, kwangu mimi hawezi kunishawishi.

Siasa sio vita...ni hoja tu.
Toa hoja yako then itetee.

Lissu kanusurika , ipo siku nyingine atapigwa Mzazi wako au mtoto wako au ndugu yako wa karibu na hatanusurika.

Mimi na familia yangu Tunamchagua LISSU potelea mbali , nature itaselect.
 
Wenye masilahi binafsi wamekula 10% ununuzi wa Ndege ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge wamekula trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara, bilion 12 matibabu ya Ndungai India , mihemko ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani?
Thibitisha
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom