Elections 2015 Magufuli: Safari za Kikwete nje ya nchi zina manufaa makubwa

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,031
1,603
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John Magufuli, amewashangaa watu wanaokejeli safari za nje za Rais Jakaya Kikwete, akisema manufaa ya ziara hizo ni makubwa kuliko wanavyofikiri.

Amesema kupitia safari hizo, Rais Kikwete amefanikiwa kuwashawishi wafadhili kutoa misaada ya miradi mbalimbali nchini.

Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Mvumi Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana.

Dk. Magufuli alitoa mfano wa Sh. bilioni 992 zilizotolewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mfuko wa MCC kwa ajili ya miradi ya umeme kama sehemu ya matunda ya safari za Rais Kikwete nchi za nje.

"Mabilioni yaliyotolewa na MCC, yatasaidia kusambaza umeme katika mikoa na vijiji vingi nchini na tayari mipango imekamilika ya kuwafikishia wananchi nishati hiyo," alisema.

Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na wafuasi wa Ukawa kuvamia ofisi za chama hicho mkoani Tanga na kufanya mashambulizi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, January Makamba, shambulio hilo lilifanywa juzi kabla na baada ya Ukawa kumaliza mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano kwa kurusha chupa zenye haja ndogo.

Aidha, alidai kuwa tukio hilo lilifuatiwa na la mgombea wao wa urais, Dk. John Magufuli, la kusimamishwa njiani na vijana wa Ukawa pamoja na kupiga kelele kwenye mkutano wake wa hadhara mkoani Mbeya kuwafanya wananchi wasimsikilize


CHANZO: NIPASHE
 
huyu ajitambui anamponda alafu anamsifia, nayeye akiingia ataanza safari za ulaya akajifunze english hadi ajue miaka mitano imeisha!
 
OVYOOOOOOOO!!!!!!!!!! Mr Push-up ana roho ileile ya ombaomba na kutembeza bakuli ya Mr Dhaifu, ndiyo maana tunamtaka Lowassa mwenye maono ya jinsi ya kutumia raslimali nyingi tulizo nazo, katika kutukwamua katika lindi la umaskini!
 
OVYOOOOOOOO!!!!!!!!!! Mr Push-up ana roho ileile ya ombaomba na kutembeza bakuli ya Mr Dhaifu, ndiyo maana tunamtaka Lowassa mwenye maono ya jinsi ya kutumia raslimali nyingi tulizo nazo, katika kutukwamua katika lindi la umaskini!

Ma foreigner wanagwaya sana opposition. Hii inaonyesha kuwa ni wanufaika wakubwa sana wa mfumo uliopo.

Nilikuwa naongea na mmoja, nikamweleza why we need changes, ikiwemo sababu ya kuchoshwa na wizi wa rasirimali zetu kunakofanywa na mataifa yao ya ulaya.

Eti akaleta story na mifano ya Libya na Iraq, hovyo kabisa.
 
Duh...ameamua kuendeleza sera ya 'kutembeza bakuli' Ulaya!!
 
Nahisi huyu jamaa akifanikiwa atasafiri hadi mwezini kama na yeye anaona safari zilikuwa na manufaa!!!!
 
huyu ajitambui anamponda alafu anamsifia, nayeye akiingia ataanza safari za ulaya akajifunze english hadi ajue miaka mitano imeisha!

Atakuwa anatembea na mkalimani ................... wenzako wanakwambia lugha siyo tatizo!!
 
Back
Top Bottom