Magufuli: Saddam alikuwa rais wa Kuwait!!

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
652
562
Nimenukuu ukurasa wa 22 wa Gazeti la mwananchi la leo 16/09/2015
para ya Kwanza; naomba ninukuu" Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. walimwondoa madarakani rais Saddam , hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait"

"Magufuli , na Lowassa nani atatufaa kwa Siasa za nje" ni kichwa cha habari cha article yenyewe.

Magufuli huyu anayejua kila barabara ya nchi hii ameshindwa kujua vitu vya darasa la nne vinavyotokea nje ya mipaka ya Tanzania sembuse siasa za kimataifa atazijulia wapi. Kuna uwezekano akashindwa kujua hata majina ya nchi tulizopakana nazo, au kushindwa kujua Marekani, india Uk nk zipo mabara gani. Kama ni hivyo je atajuaje trouble makers na marafiki wa kweli anaoweza kushirikiana nao katika siasa za dunia. Au ushindi kwanza mengine yatajipa?. Ukiona rais hajui kinachoendelea upande mwingine wa dunia ujue kazi tunayo hivyo tusifanye makosa katika uchaguzi wa mwaka huu la sivyo watanzania woote tutaonekana mambumbumbu.
 
Magufuli hajui lugha, hata huko UN ataweza ongea Kisukuma yule....
Hata hiyo Doctorate itakuwa alisoma kwa kiswahili
 
Magufuri ni mtu wa kukariri,sio kuelewa, mtu anaekariri muda flani husahau, hata sasa ukimshtukiza barabwra ya bagamoyo mwenge atakwambia ina kilomita 1000.

Mawaziri wa kikwete ni mzigo,vihiyo. Mulugo alisema Tanzania inatokana na zimbabwe na zanzibar. Pia akasema mbeya ina ukubwa wa kilomita 29 za mraba.

Saddam alikua rais wa kuwait?
 
Huyu jamaa ni sawa na Idd Amin-if so to speak...kilichomuokoa ni kaelimu tu
 
Magufuri ni mtu wa kukariri,sio kuelewa, mtu anaekariri muda flani husahau, hata sasa ukimshtukiza barabwra ya bagamoyo mwenge atakwambia ina kilomita 1000.

Mawaziri wa kikwete ni mzigo,vihiyo. Mulugo alisema Tanzania inatokana na zimbabwe na zanzibar. Pia akasema mbeya ina ukubwa wa kilomita 29 za mraba.

Saddam alikua rais wa kuwait?
Teh,teh,teh we jamaa wewe daa!!hii nimeipenda.
 
Dr.Magufuli unataka umlinganishe na huyo mwenye shahada ya sanaa za maigizo?ebu tuache mizaa kwenye mambo muhimu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom