Magufuli: Nimefurahi sana kusikia madereva wa malori wamekosa mizigo, barabara zitapona

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Habarini wakuu, sasa hivi kama mnafahamu watu tunaochukua mizigo bandarini kazi zimepungua sana na wengine wamepunguzwa kazi.

Hata sisi ambao tuna kazi mishahara huwa inachelea hadi miezi 3 kwa kuwa hatuwezi kulipwa na sababu ni mizigo ya kusafirisha hakuna

Sasa mheshimiwa rais alipoanza kuzungumzia kuhusu ukosefu wa kazi kwa wadau wa bandari, hakuzungumzia hata kwa undani ila alisema amesikia madereva wamekosa mizigo.

Badala ya kuzungumzia hiyo changamoto ambayo imetuathiri sana akasema amefurahi sisi kukosa mizigo kwa kuwa alikwisha gombana na sisi.

Hao madereva wa malori aliogombana nao pengine wengi walishaacha kazi tupo sisi wapya, sasa badala ya kuzungumzia muafaka anasema anafurahi kwa sabau aligombana na madereva kipindi cha nyuma?

 
Kuna transformation katika sector mbalimbali na victim lazima wawepo kama ilivyokuwa kwa reli n.k...Sasa kama kazi hii haiwezekani unatafuta nyingine ambayo inaendana na sera ya wakati huo...uchumi ndivyo ulivyo...bei zikishuka hasara kwa muuzaji na faida kwa mnunuzi lakini net effect unayotakiwa kuiangalia ni je society ina gain au ina loose na je hizo transfer dead weights zake ni kubwa kiasi gani... Ndivyo ilivyo

Nyakati zile za uchumi holela wakulima walikuwa ndiyo victim in expense ya wafanya biashara wa bidhaa za nje, sasa kuna shift ambapo kilimo kinaonekana kuongeza thamani yake kiujumla kwahivyo akili ni kuwa dereva wa fuso kuleta mali kutoka vijijini kwenda kwa walaji ambao wana cash na kubeba michanga yakujenga nyumba zinazojengwa, barabara na reli...

Uking'ang'ania kuendesha magari ya mizigo kwenda nje kupitia bara bara huku ukiendelea kubomoa barabara zetu kisa tu mfanya biasha aliyekuajiri aendelee kuchuma badala ya usafirishaji unaopendelewa na nchi kupitia reli basi hatuna msaada...

Tajiri wa hayo maroli kashanyang'anywa deal na kama alikuwa fisadi basi ndiyo mwisho umefika na kazi yake anapelekewa yule aliyejiunganisha na wakulima vijijini...
 
yeye kasema matajiri wa malori nyinyi mmegeuza madereva hahahaha mnachekesha sana.

Hawajui hilo..Wanailetea garama nchi kwa faida ya waajiri wao binafsi...sasa garama za barabara tulipe sote lakini faida inaelekea kwa hizo familia chache huku wakisaidia mataifa na makampuni ya nje kusambaza bidhaa zao huku wakulima wetu wakilia hakuna masoko....
 
To be fair, naona mleta mada umem quote out of context (kwa kuacha kuhusianisha kauli yake na suala la uharibifu wa barabara na ulipaji kodi). Lakini vizuri umeweka video!

Hata hivyo njia ambayo serikali ilitumia kushughulikia suala hili ilikuwa ya kukurupuka (not holistic enough) - iliondoa hata wale waliokuwa wanalipa kodi na ndio sasa tunaanza kuwabembeleza tena warudi.

Je anamwambia Kabila kuwa mizigo ya Congo ilikuwa hailipiwi kodi? Kabila analalamikia wizi/upotevu. Naona kuna misalignment kiaina.
 
wale wabandari wasubiri tutakapo anza kusafirisha mazao yetu nje kama tutafanikiwa otherwise tunaimarisha uzalishaji na soko la ndani kwanza...Tuna punguza importation na kama hakuna equivalent substitution kwenye exportation hiyo mizigo bandarini itatoka wapi? Hii ni akili yakawaida tu na zama hizi za transition kuna kukaa jangwani kidogo usitegemee leo umepungaza imports then kama huja produce qulity exports hutapata gap hapo...Ukipunguzwa kazi unaenda kulima au unakuwa mwl wa shule kule ambapo hakuna waalimu...huko vijijini hakuna waalimu, hakuna wakulima wasomi, hakuna wanaoweza hata kusaga unga wala kukoboa makande hizo ndizo option za nyakati hizi...mambo ya kukaa Dar yatakaribia mwisho sote tuende shamba tukalime...
 
Habarini wakuu, sasa hivi kama mnafahamu watu tunaochukua mizigo bandarini kazi zimepungua sana na wengine wamepunguzwa kazi
Hata sisi ambao tuna kazi mishahara huwa inachelea hadi miezi 3 kwa kuwa hatuwezi kulipwa na sababu ni mizigo ya kusafirisha hakuna

Sasa mheshimiwa rais alipoanza kuzungumzia kuhusu ukosefu wa kazi kwa wadau wa bandari, hakuzungumzia hata kwa undani ila alisema amesikia madereva wamekosa mizigo,
Badala ya kuzungumzia hiyo changamoto ambayo imetuathiri sana akasema amefurahi sisi kukosa mizigo kwa kuwa alikwisha gombana na sisi

Hao madereva wa malori aliogombana nao pengine wengi walishaacha kazi tupo sisi wapya
sasa badala ya kuzungumzia muafaka anasema anafurahi kwa sabau aligombana na madereva kipindi cha nyuma?

Tumia reli kusafirisha.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hili la meli Kupotea zaid ya sitini bila kuwa record zilileta nini Tanzania tulitisha asee .

Ukwel nchi ilioza kwa Rushwa na ndio maan maisha sasa hivi tait sabab ya mianya mingi ya rushwa na deal imefungwa.

Lazima maisha yawe magum kwa watu maan kila kona kilio tu .
 
Gud thing ni kwamba alishasema toka kwny mkutano wa kamati kuu wa Dodoma, hana uvumilivu ata kidogo na wanaokwenda nae against......
 
Ili umwelewe inabidi uwe na akili za kuelewa kama ni hizi za kupiga deal utaishia kumlaumu kila siku...siyo yeye anayekukwaza unakwaza na akili yako mwenyewe iliyofungwa na status quo
 
Kila nikikaa na kutafakari kauli za huyu mtu nakosa jibu, hivi hajui kama kuna watu tunaumia na kauli zetu,hvi huyu ni baba gani jaman asiyejali watoto wake,hivi hajui kama ss hv hali ni mbaya zaidi , vibaka wamerudia kazi yao kama zamani, mm muhanga wa vibaka last week nmeporwa kila kitu, yote hii sababu ya hali ngumu tulo nayo, lkn bado halioni hili
Mungu tu amsamehe bure huyu baba
 
Ajabu hata hili kuna watu watalitetetea...
nahisi jina la 'Pombe' limegeuka ulevi mbaya kwa kila mtu...

watu 'wamelewa' na hawataki kusikia..

Omba kueleweshwa kama huelewi... ni hivi uchumi upo mikononi mwa watanzania na siyo kwa wajanja wachache kushirikiana na wachuuzi wakimataifa...Uzuri ni kuwa amesema hizo korosho zita nyooka tu na mwisho tutatabasamu wote tutakapo ina hiyo Tanzania ambayo mioyo yenu ya giza imegoma kuiamini inakuja na macho yenu ya giza imekataa kutazama maono yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom