Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,495
- 51,089
Tukisoma historia, utaona kuwa nchi yetu imepita katika vipindi kadhaa vya uongozi baada ya uhuru
1. Kuna Serikali huru chini ya waziri mkuu Nyerere iliyodumu kwa miezi mitatu baada ya kupata uhuru
2.Kuna serikali iliyofuata baada ya Nyerere kujiuzulu kwenda kuimarisha TANU iliyoongozwa na Rashid Mfaume Kawawa kama Waziri mkuu
3. Kisha kuna serikali ya Nyerere kama rais sasa baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri iliyoongozwa na Nyerere tena kutoka 1962 hadi 1964
4. Kisha kuna serikali ya Muungano iliyoongozwa na Nyerere kutoka 1964 hadi 1985
5. Kuna Serikali ya Mwinyi ya 1985 hadi 1995
6. Kuna Serikali ya Hayati Benjamin Mkapa kutoka 1995 hadi 2005
7. Inafuatiwa na serikali ya Jakaya Kikwete ya kuanzia 2005 hadi 2015
8. Na sasa tuna serikali ya John Magufuli iliyoko madarakani kuanzia 2015 hadi leo 2020
Sasa sisi tunadai kuwa hii ni serikali ya awamu ya Tano, Mimi napinga hili kwa nguvu zote, kwa sababu tunadhani kuwa Uongozi Kizalendo wa nchi hii ulianza mwaka 1964 chini ya Nyerere na Tunajifanya hatuoni Serikali za kuanzia mwaka 1961 hadi 1964. Yaani awamu hii tunaifuta kabisa utadhani haipo!
Mimi naomba hizi awamu tatu za Nyerere na Kawawa kisha Nyerere tena kama viongozi wakuu wa nchi hii zitambuliwe kama awamu rasmi za uongozi.
Pamoja na kwamba zilikuwa ni awamu za Tanganyika, hilo haliondoi ukweli kuwa hoyo ni Tanganyika huru, pande la nchi yetu, ni serikali za kizalendo na Zibapaswa ziheshimiwe kama awamu za kitawala!
Sisi tunamuondoa Kawawa kama kiongozi aliyewahi kuwa Mkuu wa awamu inayojitegemea kabisa ya utawala wa nchi!
Kwa hiyo Usahihi ni kuwa Magufuli ni rais wa Awamu ya Nane siyo awamu ya Tano!