Magufuli ndo wa kwanza,Tanzania aipambe (Shairi)

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745

1.Hongera Johni Pombe ,kwa kazi uloianza.
Wewe umepata kombe,shindano halijaanza.
Chomoza yako mapembe,uchome walojibanza.
Magufuli ndo wa kwanza,Tanzania aipambe.
Mwiba


2. Hakuhitaji wapambe,kazi alipoianza.
Alipita kwenye pembe,benki alipoanza.
hatizami nani shombe,wote aliwauliza.
Magufuli ndo wa kwanza,Tanzania aipambe.
Mwiba

3, Sasa apita na jembe,afukuwa kwenye manza.
Walioachwa wasombe,na mali zilizo mwanza .
awapasua kwa wembe,matumbo waliojaza.
Magufuli ndo wa kwanza,Tanzania aipambe
Mwiba

Endeleza !
 
Back
Top Bottom