Magufuli ndiye Rais pekee anayefata misingi ya Katiba, siasa na matakwa ya wananchi

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,369
17,051
******Ndugu zangu wana jf ningependa kila mmoja kabla ya kuchangia kichwa cha habari ASOME MPAKA MWISHO KABLA HAJASEMA CHOCHOTE******

Kwanza kabisa namshukuru mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu rehema kubwa na kati ya zile zilizo ndogo pasina kujali kabila,Dini na utaifa wetu.

Pili nipende kuwashukuru wote watakaosoma huu uzi au kuchangia;

Kulingana na katiba ya Tanzania sehemu ya tatu ya katiba kuanzia ibara ya 18 mpaka ibara ya 21 inazungumzia haki ya uhuru wa mawazo nita,kabla ya kuanza naomba ninukuu ibara ya 18 ibara ndogo ya 1 ya katiba yetu “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”

Kwa kunukuu ibara hiyo naomba moja kwa moja nianze kuelezea mawazo yangu

Kwanza kabisa J.P.M ni rais pekee ambaye amekuja Tanzania kukiwa tayari kuna revolution ya technologia kubwa kuliko marais wote,pili nchi ikiwa inakadiriwa kuwa na wasomi wengi kuliko miaka yote ya nyuma; kulingana na taarifa ya ripoti ya UNDP kabla ya mwaka 2010 tanzania ilikuwa na 20% ya jumla ya wasomi wote but mnamo mwaka 2015 wasomi waliongezeka kutoka 20% mpaka 49.7% hivyo ni sawa na onezeko la 29.7% ni idadi kubwa sana ambayo sio constant ,means inaendelea,Hivypo hiyo pia ni moja ya changamoto za SIASA Tanzania ambazo inabidi kutafuta mbinu mbadala kuziovertake..

Kwanini naema anafata misingi yakikatiba…katiba ya sasa ya Tanzania inampa madaraka makubwa sana rais kuliko mtu mwingne serekarini au kuliko mihimili yote serikalini hvyo inamfanya kuwa juu ya mahakama na Bunge

Kwani anao uwezo wa kulivunja bunge endapo halitapitisha vitu flani flani…nanukuu kauli ya mwalimu nyerere “KATIBA HI IMENIPA MADARAKA, MAKUBWA SANA, IPO SIKU ATAKUJA MTU ATAITUMIA ATAKAVYO NA ATAKUWA KAMA MUNGU” Mwl J.K Nyerere February 23 1983

Kulingana na kauli hiyo ya hayati baba wa taifa tunapata jibu kwamba katiba haiku sawa na mtu akiitumia vizuri kama sasa anaonekana yupo kinyume..

Cha pili ni mwana siasa kwani tumeshuhudia matamko mengi sana ambayo mengi hayajatimia yakiwemo AJIRA, MAKINIKIA UBORESHWAJI WA MIKATABA BUNGENI ,kuongezwa kwa mishahara kwa watumishi wa umma hayo ni baadhi tu ila kuna protocol za kisiasa kazifuata kama DIVIDE THEM AND RULE (kaifanya kuwatenganisha act na vyama vingne-kwa kuwateua viongozi wa ACT kuwa viongozi waandamizi serikalini hyo inavunja nguvu ya ACT kuihoji serikali wala kuunga mkono wapinzani wenzao…kingne kwenye siasa tunakita MAKE ENEMY OF MINE TO BE ENEMY OF OURS hii njiailitumiwa sana na waingereza walipotaka kumtoa mjerumani Tanzania walitufanya tuone kuwa mjerumani ni adui yetu mkubwa ili tusaidiane nao kumtoa na kuwakaribisha wao ..ndicho anacho kifanya kuwafanya watanzania waone kuwa wapinzania wanzavunjasheria kwa kuwaweka mara nyingi ndani kupoteza uaminifu na wananchi..kingne ni kutokuwapa nafasi wapinzani kusema chochote iwe bungeni au mtaani..

Rais wetu anapendwa sana na watu kwa kuligundua hilo anatumia njia moja inaitwa kutumia hisia zao kuwa mihemko anajaribu kufanya matukio mengi amabyo yatawafurahisha wananchikuendelea kupataimani yake ..

NARUDIA TENA IBARA ibara ya 18 ibara ndogo ya 1 ya katiba yetu “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”
 
Back
Top Bottom