Magufuli: Nakerwa na vigezo vya uzoefu kuomba ajira | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli: Nakerwa na vigezo vya uzoefu kuomba ajira

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Paul Alex, Sep 29, 2015.

 1. Paul Alex

  Paul Alex JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2015
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 2,875
  Likes Received: 4,188
  Trophy Points: 280
  Wadau hebu someni hii habari halafu tujadili kama hii ni nini zaidi ya siasa za mfamaji!

  Tatizo la ajira ni kigezo cha uzoefu au ukuaji wa polepole wa sekta ya umma na sekta binafsi?

  Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira.

  Dk Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi hizo lakini wana uwezo wa kuongoza.

  Katika kampeni zake mjini Iringa leo, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

  Amesema kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo.

  ''Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa? Tena wanataka uzoefu wa miaka mitano huo uzoefu wataupata wapi, nataka kama kuna uwezekano haya mambo ya uzoefu yafutwe kabisa," Dk magufuli.

  Ameeleza kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda ili kumaliza tatizo hilo sugu kwa wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla. Amewataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.

  Poleni CCM
   
 2. MOTOCHINI

  MOTOCHINI JF-Expert Member

  #21
  Sep 29, 2015
  Joined: Jan 20, 2014
  Messages: 24,064
  Likes Received: 12,630
  Trophy Points: 280
  Huyu mnajisumbua ndie rais
   
 3. MOTOCHINI

  MOTOCHINI JF-Expert Member

  #22
  Sep 29, 2015
  Joined: Jan 20, 2014
  Messages: 24,064
  Likes Received: 12,630
  Trophy Points: 280
  Ulitaka akerwa kipindi gani
   
 4. M

  Magnify JF-Expert Member

  #23
  Sep 29, 2015
  Joined: Nov 16, 2014
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeanza kukerwa lini hata bungeni kutoa hiyo hoja hujawahi?
   
 5. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #24
  Sep 29, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,891
  Likes Received: 24,284
  Trophy Points: 280
  Kweli Watanzania mmeamka hadi raha.
   
 6. DE FULE

  DE FULE JF-Expert Member

  #25
  Sep 29, 2015
  Joined: Jan 10, 2013
  Messages: 1,122
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Muulize EL ndo anachukia leo umaskini...?
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #26
  Sep 29, 2015
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,309
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Asilete siasa kwenye kila jambo. Kwenye Utumishi kuna kitu kinaitwa scheme of service au miundo ya utumishi...Mtu asiye na uzoefu wa kazi anaajiriwa kwenye vyeo vya kuingilia au entry point. Vyeo vya juu ya hapo vinataka mtu awe amefanya kazi kwa angalau miaka mitatu. Kuna vyeo ambavyo unaajiri mtu anayejua kazi sio anayeenda kujifunza. Kama anataka kufuat huo utaratibu awe mkweli kwamba haitachukua mwaka mmoja kwa sababu utatakiwa kubadilisha sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyopo sasa
   
 8. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #27
  Sep 12, 2017
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,242
  Likes Received: 6,008
  Trophy Points: 280
  Zee nafiki sana hili
   
 9. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #28
  Sep 12, 2017
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,242
  Likes Received: 6,008
  Trophy Points: 280
  Ni unafiki tu ulikuwa
   
 10. k

  kiumbempole Senior Member

  #29
  Sep 12, 2017
  Joined: Jan 15, 2016
  Messages: 151
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #30
  Sep 17, 2017
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,309
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Huko mimi sipo. Sina jeuri ya kukataa kupimwa mkojo aise
   
 12. PAZIA 3

  PAZIA 3 JF-Expert Member

  #31
  May 1, 2018
  Joined: Jan 30, 2018
  Messages: 636
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 180
  Siku hizi amesahau kabisa aliyoyasema
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...