Magufuli: Nakerwa na vigezo vya uzoefu kuomba ajira

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,239
9,527
Wadau hebu someni hii habari halafu tujadili kama hii ni nini zaidi ya siasa za mfamaji!

Tatizo la ajira ni kigezo cha uzoefu au ukuaji wa polepole wa sekta ya umma na sekta binafsi?

Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira.

Dk Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi hizo lakini wana uwezo wa kuongoza.

Katika kampeni zake mjini Iringa leo, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Amesema kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo.

''Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa? Tena wanataka uzoefu wa miaka mitano huo uzoefu wataupata wapi, nataka kama kuna uwezekano haya mambo ya uzoefu yafutwe kabisa," Dk magufuli.

Ameeleza kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda ili kumaliza tatizo hilo sugu kwa wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla. Amewataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.

Poleni CCM
 
Aache kuwatapeli wapiga kura. Kwenye ajira lazima kuwe na nafasi za watu wenye uzoefu na za wasio na uzoefu. Hawezi kuondoa hilo. Na hukuna sheria inapinga hilo kwani hiyo ndio hali halisi ya ajira popote duniani.

Cha kufanya ni kutengeneza ajira mpya tu.Hizo nyingine ni blabla tu za kuomba kura.

Basi awachukuwe wanafunzi waliomaliza chuo wakafanye kazi za kujenga barabara na nyumba aone kama wataweza. Wenye uzoefu lazima wawepo.

Wakati wenzake wanasema mapema miaka iliopita kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni bomu mbona hatukumsikia akisema chochote?
 
Magufuli yupo sahihi

Kwahiyo wewe unaimani kigezo cha uzoefu kikiondolewa basi watu wote wasio na kazi watapata kazi?

Hivi umeshawahi kutafuta hela kwa shida ukapata mtaji ukaanza biashara halafu uajiri mtu aje ajifunzie hapo kwenye huo mtaji?

Kama huu ndio ufikiri wako na Magufuli basi Tanzania kuna shida
 
Huwa inawekwa tu, lkn wanachukuag watu wote Mara nyng lbda uogope we mwnyw ku apply
 
Magufuli yupo sahihi

Hata mwenzie JK mwaka 2005 alilisema hilo katika kampeni zake za chama hichohicho cha CCM wakati anaomba kura. Kwa hiyo hizo ni hadithi zao zinajirudia tuu. Nawaomba vijana wengi wapiga kura ambao mwaka 2005 hawakuwa wapiga kura kutokana na umri waelewe hiyo ni nyimbo kama zile za taarabu tuu, CCM NI ILE ILE NA MAMBO NI YALEYALE.
Wasidanganyike hata kidogo.
 
Magufuli yupo sahihi

Yupo sawa kwa asilimia chache, maana anachotaka kutuaminisha ni kuwa vijana wanakosa ajira kwa sbb hawana uzoefu, inamaanisha hzo nafac zinaendaga wap baada ya kukosa watu wenye uzoefu!??
 
Aache unafiki wake bhana. Anakerwa saa hizi akiomba kura
 
Wadau hebu someni hii habari halafu tujadili kama hii ni nini zaidi ya siasa za mfamaji!
Tatizo la ajira ni kigezo cha uzoefu au ukuaji wa polepole wa sekta ya umma na secta binafsi?

Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira.
Dk Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi hizo lakini wana uwezo wa kuongoza.
Katika kampeni zake mjini Iringa leo, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Amesema kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo.
‘’Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa?.. tena wanataka uzoefu wa miaka mitano huo uzoefu wataupata wapi, nataka kama kuna uwezekano haya mambo ya uzoefu yafutwe kabisa,” Dk magufuli.
Ameeleza kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda ili kumaliza tatizo hilo sugu kwa wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla. Amewataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.

Poleni CCM
Mtu anayeweza kuhoji kuhusu kipengele cha uzoefu katika ajira ni yule tu aliyeko nje ya ajira, yaani ambaye bado hajaajiriwa. Ukweli ni kwamba kuna nafasi ambazo zinahitaji uzoefu kulingana na ngazi ya utendaji. Kuna ngazi au daraja ambalo mfanyakazi analipata baada ya mwaka mmoaj, miwili, mitano, miaka 10 au zaidi. Katika ngazi ya awali yaani ile ya kuingilia kawaiada haihitaji uzoefu bali kiwango cha elimu husika, lakini ikitokea nafasi ikajitokeza inayohusu mtu aliyekuwa anaishikilia ameacha kazi, amfarikia au amefukzwa kazi, na huyo mtu alikuwa katika daraja la juu, ni kawaiada kwamba mtu akayaepaswa kuajiriwa kushika nafasi hyo ni yule ambaye ana uzoefu na nafasi iliyopo, vinginevyo, akijiariwa mtu ambaye hana huo uzoefu lazima atapwaya na kazi zitamshinda. Aidha, zingatia kwamba kazi nyingi hazihitaji kiwango cha elimu tu, hata uzoefu wa kukabiliana na changamoto za kazi hiyo nao ni muhimu, vile vile uzoefu wa kuhudumia wateaja wa aina tofauti tofauti, Ni ni ukweli usiopingaka kuwa ukiingia kwenye eneo la kazi ambapo mtu aliyepo uzoefu wake kuhusu hiyo kazi ni mdogo utauona tu. Mfano mzuri ilikuwa wakati wa zoezi la kuandikissha wapiga kura, kuna baadhi ya watu waliingiia katika kazi ile bila kuwa na uzoefu na matumizi ya komyuta, nathani tulishuhudia kilichokuwa kinatokea kwa baadhi ya vituo. Hata hivyo, tatizo la ajira nchini Tanzania tatizo sio hivyo vigezo bali ni kutokuwepo hizo nafasi, ndo maana ikitokea nafasi ya watu wawili, waombaji wanakuwa 5000. Kama nafasi zingekuwepo, waajiri wangeisha legeza hivyo vigezo vya uzoefu maana wangejikuta bila kuwa na wafanyakazi kwa sababu ya Labour Moility.
 
54832942.jpg
 
Watu kama akina Tido, wanavyoiendesha vzr azamtv. Unafikiri ni sawa na kumchukua mtu aliyemaliza chuo, na ikawa ni ndiyo kazi yake ya kwanza? Kama vp tuanze na wizara yake kwanza, atuajiri bila uzoefu.
 
Mwambie anzishe ajira zake zisizohitaji experience. .kisha atoe ajira..
 
Ameajiri wangapi katika wizara alizopitia bila kuzingatia uzoefu wao?
akijibu hili ntamuelewa.

I am a politicians" by Dr. magufuli
 
Mwambie anzishe ajira zake zisizohitaji experience. .kisha atoe ajira..
Ameishawahakikishia wana-ccm wote ambao kura za maoni hazikutosha waendelee kumuunga mkono na kazi zipo tele akiishaingia ikulu. hizo ndio ajira zisizohitaji experience lakini sharti ni moja tu -uwe mkereketwa wa kijani. huyo ndio makomeo.
Haya ya kukerwa na vigezo vya uzoefu anawalaghai tu vijana. Atoe mfano alikemea hiyo tabia katika kikao gani cha wizara gani ambazo amezisimamia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15. Akitoa ushahidi huo, ninabadilisha kura yangu kutoka kwa el na kuielekeza kwake.
 
Akiwa waziri magufuli alihonga nyumba za serikali. Sasa akiwa rais atahonga nn?
Kumbuka rais wa awamu ya tatu alihonga wizara ya fedha kwa ajili ya dili la mwanamke.
Rais wa awamu ya nne alikuwa anahonga wilaya na mikoa.
Ccm inanuka uchafu haisafishiki. Magufuli ni dodoki chafu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom