Magufuli na wimbo wa "kada wa chama... Mpeni kura za ndiyoooo" - jumamosi jangwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli na wimbo wa "kada wa chama... Mpeni kura za ndiyoooo" - jumamosi jangwani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masantula2012, Jun 11, 2012.

 1. M

  Masantula2012 Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu Wadau - JF.

  Hebu naomba kwa aliyeelewa au kutafakari na kutafakuri juu ya wimbo uliopigwa wakati Dr. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Magamba alipokuwa akihutubia wenzake waliojumuika katika viwanja vya CHADEMA Square (Zamani Jangwani) siku ya Jumamosi.

  Baadhi ya maneno yalikuwa " Kada wa CCM .... Mpeni kura za Ndioooo..." Pili yeye ndiye aliyekuwa amepangwa na kuongea mwishoni kati ya mawaziri wote!!

  Aidha, ndiye aliyekusanya kadi na bendera za vyama vinginevyo especially CHADEMA (Za Wana wa M4C). Alivyoongea kwa maana ya sauti na "style", aliongea kama mtu mwenye "Authority" sana na mwenye matumaini fulani. Wakati akikusanya kadi na bendera, wimbo huo ukapigwa tena kwa muda mrefu lakini kana kwamba TOT walidokezwa kiaina fulani, wakamalizia na Jakaya Kikweteee ... Apewe kura za Ndiyoooo...

  MY TAKE: Pamoja na kuwa hainitishi wala kunizuga akili, nilitafsiri kuwa hiyo ilikuwa "dalili na harakati/ mwanzo" wa Kampeni za kuingia Magogoni 2015. Je, Wadau mwalionaje hili?? Kama tafsiri yangu ni sahihi, Dr. Magufuli (Wa makufuli na mafunguo yake) atafua dafu kwa Dr. Wilbroad Peter Slaa au yeyote yule toka CHADEMA 2015???? Je tusome alama za Nyakati wana M4C na kujiandaa vilivyo? Tafakari………. Chukua hatua.
   
 2. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama ngome ya nyumbani kwake tu inabomoka, je Tanzania nzima, sidhani kama ndani ya CCM kuna mtu atauweza mziki mwa Dr Slaa, Mbowe au hata Zitti Kabwe!
   
 3. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hana lolote huyo! Magufuli ni taalam wa kukariri tu
   
 4. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mtu anaitwa POMBE,...Mi nilidhani angeomba radhi kwa kauli yake ya kuwataka wananchi masikini wapige mbizi ili wavuke BAHARI yeye aliendelea na pombe zake eti anajifanya anakusanya kadi za CHADEMA.Huyu mzee anazima moto kwa jirani huku kwake kunaungua:kweli huyu ni pombe.Naamini taarifa za CHASO-SAUT amezipata...
   
 5. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni vema POMBE, ashauriwe akapige brash ya kiswahili sanifu, kwani aksent ya speech yake kwenye kiswahi ni very affliated by his mother tongue. Is very poor in swahili language indeed.
   
Loading...