Magufuli na wanyonge vs UKAWA na wazungu!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Hatimaye UKAWA wamejipambanua katika rangi yao halisi ya kutaka kuuza uhuru kamili wa nchi...kwa kuwalilia na kuwashabikia wazungu!!

Reference iko humu humu jamvini.

Ni ukweli usio na shaka kwamba UKAWA walipambana sana hata kabla ya matokeo ya uchaguzi wa Rais Nov 2015...

Ukawa walipambana vilivyo kuwaonesha wazungu kuwa Tanzania hakuna amani...

Ukawa kwa mara ya kwanza Tanzania walihakikisha kuwa vyombo vya habari vya kimagharibi vinaonesha Tanzania kuna tension kiasi cha amani kutoweka....

Ila kwa weledi mkubwa na uzalendo uliokithiri vyombo vyetu vya kiuongozi na kiusalama vikashinda jaribio hilo ovu la UKAWA na wananchi wa Tanzania wakamaliza uchaguzi kwa amani na ustaarabu kama ikivyo desturi yetu.

UKAWA waliandaa maandamano UK na USA na sio Manzese,Magomeni au Tandahimba ili kuonesha kuwa nchi hii haina demokrasia kisa CCM ilikuwa imeshinda na inaendelea kushinda...huku wakisahau kuwa ndani ya vyama vyao wanacheza tikitaka na kugeuza gia za angani ili tu viongozi wao wawe wa kudumu yaani wanahubiri demokrasia ambayo ndani ya vyama vyao haipo.

UKAWA wako tayari kuomba majeshi nje ili tukupambana na CCM(REFERENCE: Vijana wa IT na mabodyguard kutoka nje ya nchi)

UKAWA inaendelea kujidhihirisha kwa sera zake za utegemezi kwa mataifa ya nje...yaani UKAWA inaachana na dhana ya kutumia resource nyingi tulizonazo kukwamua wananchi kutoka kwenye matatizo na badala yake inajikita kwenye kuamini kuwa maendeleo yatakuja kwa msaada na hisani ya watu wa marekani.

UKAWA inatukumbusha vikundi vya miaka ile ya kudai uhuru ...vikundi tulivyoviita vibaraka wa wakoloni.

HII NI HULKA CHAFU YA UKAWA iliyotubadilishia gia angani!!

UKAWA hii ya sasa ni UKAWA inayonukia kinyesi cha UFISADI PAPA baada ya kukiokota na kujipaka yenyewe karibia na uchaguzi wa 2015.

Hii ni UKAWA iliyopoteza agenda muhimu za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi,ukosefu wa ajira,ukosefu wa uadilifu,elimu duni na afya isiyoridhisha....UKAWA inahaha kutafuta Agenda ya kubakia kwenye ulingo wa siasa kwa gharama yoyote baada ya kuvurunda ...!

UKAWA inajitenga rasmi na hoja za wananchi na badala yake inachukua mrengo wa kunyenyekea wakoloni!

UKAWA inaanzisha mapambano upya ya sisi wazalendo dhidi ya Ukoloni wa kisasa na kwa nguvu zetu,adabu,uvumilivu na msimamo tutashinda tu...!

UKAWA haisikiki kwebye vita dhidi ya mauaji ya albino lakini inataka isikike kwenye msaada wa MCC...HUU NI UNAFIKI WA KUTUPWA!!

SHAME UPON UKAWA ILIYOAMINIWA NA KUJIGEUZIA GIA ANGANI...!

KWA MAGUFULI HAKIKA MTAISOMA NAMBA....KWANI AGENDA YETU NI KAZI TU KAZI TU KAZI TU!


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
kweli wewe jinga lao kweli
yaani unaleta habari ya mwaka jana wakati leo tuna habari mpya kabisa ya MCC!!!

Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).

MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.

"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.
 
Back
Top Bottom