Magufuli na Wanaomshauri Hawajui Kanuni za Uchumi wa Nchi.

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kwa watu wanaoelewa Uchumi, Kuna Tofauti Kubwa kati ya Macro Economy na Micro Economy. Na Kanuni za Kuendesha Nyanja Hizi Mbili za Uchumi Zinatofautiana. Nitasema Kwa Kifupi sana. Nianze na Dhana ya Kubana Matumizi, Dhana ya Kubana Matumizi ni Dhana ambayo Kila wakati inasaidia Katika Micro Economy yaani Uchumi wa watu Binafsi na Mashirika Madogo.

Lakini Dhana ya Kubana Matumizi ni kwa Asilimia Ndogo sana Unaleta Manufaa kwa Macro Economy hasa Uchumi wa Nchi (Kwa Maana ya Serikali) Namaanisha Nini, Ninapokuwa Mtu Binafsi Sina ajira na Bank Nikiwa na Tsh. 500,000 Kwa Kuwa sijui Kazi Nitapata Lini. Inanibidi Nianze Kutumia Laki tano yangu kwa Kuibana sana (Hiyo Ni Kanuni ya Micro Economy) Sasa tofauti, Nikiwa Rais, Uchumi wa Nchi Umedorora, Watu hawana Kazi na Hazina kuna Tsh, 200,000,000,000 tu, Sitasema Oh my Ngoja Tubane matumizi. Hiyo Itaharibu Zaidi. Mwisho hata Kodi Zitakauka. Nitakachofanya, Nitaanzisha Miradi ya Barabara, au Miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Polisi au Waalimu, Na katika Miradi hiyo, Nitahakikisha Inabuniwa kwa namna ambayo Vifaa na Malighafi vitakuwa Vinatoka Nchini, Hivyo Wajenzi wanapata ajira, Mchana Wakienda Kula lunch, Mama nitilie anapata ajira, Na kama nilibuni Barabara ya Zege badala ya Lami, Kiwanda cha Cement Kinauza zaidi, Kinaajiri zaidi. Kodi Nazo Zinapatikana Zaidi. Na Mwisho wa Siku Mzunguko wa Uchumi Unaaza Kupiga Kasi.

Kadhalika Iwapo Uchumi Unadorora Serikali Kuu Inatakiwa Kupunguzia watu Kodi Kidogo sio Kuongeza, Pia hazina Inatakiwa Kusaidia Kushusha Viwango Vya Riba Sio Kuongeza. Hata Kama Itabidi Kuchapisha Pesa Zaidi (Now, Huwezi Kuchapisha Pesa na Kuzigawa, Zitaleta inflation ) Unachapisha Pesa zaidi (Kwa Nchi ambazo Pesa za Karatasi bado ni Principle means of transaction) Kisha baada ya Kuwa Na Fedha Zaidi Kwenye Mzunguko, hakikisha Zinakwenda Katika Miradi Itakayochochea Ajira za haraka na Kudumu.

Ndio Maana, Kuna Msemo wa Zamani sana Wa Pharaoh mmoja wa Misri alisema, Ukiwa na Watu Wengi sana wenye nguvu Katika himaya na wakafa njaa. Ni Kwa Kuwa hawakumla mfalme. Umasikini Ndio sababu ya Maendeleo, Kwa Kuwa Kwenye Umasikini, Mahitaji ni Mengi na Mahitaji yakiwa Mengi Fursa Ni Nyingi. Shida Ni Uongozi!
 
Textbook staff, hao wenye wachumi tunaowasoma vyuoni kila siku wanaingia kwenye recession kwa hiyo haya mambo ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia
 
Nyie hata Magufuli Awabebe kwa mbeleko mgongoni..hamtabebeka
. mtasema anawaumiza. . Hambebeki kamwe .

Kumbuka nchi haindeshwi kwa Mawazo ya mtu mmoja wala kwa theory zako hizo za definition.

So unataka kuniambia Huo ndio Ushauri wako rasmi wa kuwafanya watanzania waishi maisha mazuri .

Tujifunzeni kuapriciate pia .,tuache kububujikwa -ve tu.

Tumeshaamua kumpa nchi mtu Basi sasa Tumuache afanye Kazi . .hii ni nchi na si Familia yako .

ViVa JPM.

HAPA KAZI TU.
 
Kwa uelewa wangu definition ya kubana matumizi ni kuwa na surplus budget(may be naweza kuwa wrong) na nlikuwa najiuliza mfano kipindi kile rais alipositisha sherehe za uhuru na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara watu wakasema serikali inabana matumizi ila mm nlifikiri serikali ili reallocate fedha na sio kubana matumizi. Cuz km alibyoandika mtoa mada kaongelea ishu za kujenga barabara km sehemu ya spending ya Serikali lkn ilipofika kwenye hiyo reallocation watu wakasema serikali imebana matumizi nafikiri km kuna vitu havijaeleweka vzr kati ya kubana matumizi na kureallocate resources
 
Wewe unadhani Kubana.Matumizi serikali inapaswa kufanyaje ? Ila kuleta Hiyo logic yaako@cdc
 
Kwa watu wanaoelewa Uchumi, Kuna Tofauti Kubwa kati ya Macro Economy na Micro Economy. Na Kanuni za Kuendesha Nyanja Hizi Mbili za Uchumi Zinatofautiana. Nitasema Kwa Kifupi sana. Nianze na Dhana ya Kubana Matumizi, Dhana ya Kubana Matumizi ni Dhana ambayo Kila wakati inasaidia Katika Micro Economy yaani Uchumi wa watu Binafsi na Mashirika Madogo.

Lakini Dhana ya Kubana Matumizi ni kwa Asilimia Ndogo sana Unaleta Manufaa kwa Macro Economy hasa Uchumi wa Nchi (Kwa Maana ya Serikali) Namaanisha Nini, Ninapokuwa Mtu Binafsi Sina ajira na Bank Nikiwa na Tsh. 500,000 Kwa Kuwa sijui Kazi Nitapata Lini. Inanibidi Nianze Kutumia Laki tano yangu kwa Kuibana sana (Hiyo Ni Kanuni ya Micro Economy) Sasa tofauti, Nikiwa Rais, Uchumi wa Nchi Umedorora, Watu hawana Kazi na Hazina kuna Tsh, 200,000,000,000 tu, Sitasema Oh my Ngoja Tubane matumizi. Hiyo Itaharibu Zaidi. Mwisho hata Kodi Zitakauka. Nitakachofanya, Nitaanzisha Miradi ya Barabara, au Miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Polisi au Waalimu, Na katika Miradi hiyo, Nitahakikisha Inabuniwa kwa namna ambayo Vifaa na Malighafi vitakuwa Vinatoka Nchini, Hivyo Wajenzi wanapata ajira, Mchana Wakienda Kula lunch, Mama nitilie anapata ajira, Na kama nilibuni Barabara ya Zege badala ya Lami, Kiwanda cha Cement Kinauza zaidi, Kinaajiri zaidi. Kodi Nazo Zinapatikana Zaidi. Na Mwisho wa Siku Mzunguko wa Uchumi Unaaza Kupiga Kasi.

Kadhalika Iwapo Uchumi Unadorora Serikali Kuu Inatakiwa Kupunguzia watu Kodi Kidogo sio Kuongeza, Pia hazina Inatakiwa Kusaidia Kushusha Viwango Vya Riba Sio Kuongeza. Hata Kama Itabidi Kuchapisha Pesa Zaidi (Now, Huwezi Kuchapisha Pesa na Kuzigawa, Zitaleta inflation ) Unachapisha Pesa zaidi (Kwa Nchi ambazo Pesa za Karatasi bado ni Principle means of transaction) Kisha baada ya Kuwa Na Fedha Zaidi Kwenye Mzunguko, hakikisha Zinakwenda Katika Miradi Itakayochochea Ajira za haraka na Kudumu.

Ndio Maana, Kuna Msemo wa Zamani sana Wa Pharaoh mmoja wa Misri alisema, Ukiwa na Watu Wengi sana wenye nguvu Katika himaya na wakafa njaa. Ni Kwa Kuwa hawakumla mfalme. Umasikini Ndio sababu ya Maendeleo, Kwa Kuwa Kwenye Umasikini, Mahitaji ni Mengi na Mahitaji yakiwa Mengi Fursa Ni Nyingi. Shida Ni Uongozi!
Unafahanu nishati na madini wametengewa kiasia gani?

Je unafahanu miundombinu wametengewa kiasi gani?

Maana ya kubana kwa serikali ya JPM ni kubana kwenye matumizi ya Chai bungeni ili fedha iende kukamilisha miradi...hamuelewi ila tutaendelea kuwaelewesha tu.
 
Wewe unadhani Kubana.Matumizi serikali inapaswa kufanyaje ? Ila kuleta Hiyo logic yaako@cdc
Mm ninavyofikiri ni kuwa na surplus budget yaani kukusanya pesa nyingi na kuwa na matumizi machache kuliko pesa iliyokusanywa au ikitokea gvt inalipa madeni kwa kuponguza spending za ndani. Ila kutoa pesa say, kutoka kwenye sherehe kupeleka kwenye ujenzi wa barabara kwa mm ninavyoona sio kubana matumizi kwa sababu gvt expenditure hapo haijaponguzwa. Km una uelewa zaid nielezee concept ya kubana matumizi
 
Back
Top Bottom