Magufuli na Ndulu, Kikwete na Idrissa...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,063
115,462
Sifa moja ya 'watalaam wanaoujua na wanajua kwamba wanajua' ni kuwa hawapendi kujipendekeza na hawaogopi kufukuzwa.

Wao hupenda kushauri kwa sauti ndogo tu ukiamua kuwasikiliza haya ukiwadharau hasara ni kwako.

Kikwete alipokuwa Rais alifanya kosa moja lillilogharibu Taifa mabilioni baadae

Kikwete aliamua kuwasikiliza Ngeleja na Adam Malima ambao walikuwa waziri na naibu waziri na kuacha kumsikiliza Mtaalam Idrissa Rashid aliekuwa CEO wa Tanesco.

Idrissa Rashid alipoteuliwa CEO wa Tanesco alikuta nchi ina mgao wa umeme na hali ya shirika hoi na wanasiasa wanaingilia maamuzi ya kitaalam.

Akapiga marufuku wanasiasa kuingilia maamuzi kwa miaka minne ya Uongozi wa Idrissa Tanesco hakuna mwanasiasa aliezungumza kitu na mgao ukaisha na shirika likaanza kusimama Idrisa alikuwa anawajua vizuri kina Ngeleja na Malima

Malima alianza kazi BOT Idrissa akiwa gavana..

Ngeleja alipokuwa Vodacom Idrissa alikuwa kwenye Management, wangemueleza nini? aliamua tu 'kutowasikiliza.

Idrissa alivyoondolewa tu Tanesco kilichofuata ni ziara za Waziri Ngeleja Tanesco na 'mgao wa dharura ukaanza' the rest is history. Zaidi ya bilioni 500 zilikwenda. Kikwete alikosea kuwasikiliza kina Ngeleja na Malima asimsikilize Idrissa.

Magufuli anaelekea kurudia kosa hilo hilo anapaswa kumsikiliza Benno Ndulu mtaalam aliemfundisha uchumi Philipo Mpango na naamini Ndulu akisema leo ataje his best students Mpango sidhani atakuwemo.

But Magufuli anaonekana kumsikiliza zaidi Dk. Mpango ambae hata VAT tu haoeneshi kuijua vizuri hadi Ndulu alipojitokeza 'kutoa ufafanuzi.

Siku Ndulu akiondoka hapo ndo tutajua hasara kiasi gani kama taifa tutaingia.

Time will tell.
 
Tuna wachache sana walioamua kusimamia taaluma na kile wanachokiamini as long as ni academically and professional concluded.
 
Mkuu Umenena Kweli..

Shida moja Magufuli huwa hataki chembe ya challenge kutoka kwa walio chini yake na kama umemsoma vema, lolote analotaka yeye liwe ndio anataka ivyo ivyo.

Sasa ameshindwa kabisa kum drive Gavana Ndullu sababu Ndullu sio msomi wa bla bla na ndio hapo Magufuli anapogonga mwamba kwa pale BOT.

Lakini kwa Waziri Dr Mpango, Magufuli anam drive anavyotaka na worse Mpango amekubali kuwa driven hata kwenye masuala ambayo yeye ana ufahamu nayo mfano kwenye suala la VAT kwenye Utalii, Mizigo ya Transit na Vocha za simu.

Kwa ufahamu wangu Chief Economic Advisor wa Uchumi wa Nchi ni Gavana wa Central Bank ya nchi yoyote ile lakini kwa hapa kwetu inaonyesha kabisa Ndullu hasikilizwi lakini kizuri hakubali KUENDESHWA.

Na ndio mana baada ya Magufuli kuivunja Bodi ya TRA ambayo yeye Ndullu ni member na kutoa sababu za kwamba TRA waliweka pesa kwenye fixed deposit kwenye bank, Ndullu amejitokeza hadharani na kusema "sio dhambi kwa institutions za serikali kuweka pesa kwenye fixed deposit kwenye banks na kwamba kuna Uwezekano mdogo sana wa pesa hizo kupigwa kama tulivyoaminishwa ".

Hii ni statement ya mtu aliejiamini kwenye taaluma yake ila ndio ivyo tena hatumiki.

Nimesikia sikia kuwa Ndullu anatarajia kustaafu utumishi wake pale BOT muda sio mrefu sana kutoka sasa.

Hapo ndio tutarajie kuwekewa Gavana ambae atakuwa anaendeshwa kama gari ambalo halina usukani.
 
na kuna watu bado hawatakuelewa
 
Sina mashaka na elimu ya Prof. Ndulu (I respect his school-NU-Evanston Chicago- where he wrote his PhD).

Lakini hebu Mkuu tufafanulie tangu Huyu bwana ashike usukani pale BoT (2008?) what have we achieved as a nation in monetary perspective?? Maana in my memory colossal sum of money has been stolen from BoT under his watch. (countless number of scandals-hata yeye mwenyewe kutumia billions za walipa kodi kujijengea nyumba ya Gavana!)

Prof. Ndullu ameingia BoT...... 1USD=1250Tshs.

Leo after almost a decade while still at the top of the BoT the shilling is at 2185 kwa 1USD.

Please enlighten us. Labda kuna vitu sisi hatujui Kuhusu hawa wasomi wetu waliotukuka.

Masanja
 
Mimi siamini kama Ndulu ni Gavana Bora...Chukulia kipindi cha Kikwete kila siku shilingi yetu ilikuwa inaporomoka, mimi natamani yule waliyesema kafia marekani angerudishwa apewe hicho cheo cha Ndulu yule jamaa kwangu ndo gavana bora kupita wote ambao wamesimamia BOT, uchumi kipindi cha Mkapa ulitengemaa kwelikweli, au wizara ya Fedha apewe Basil Pesambili Mramba.
 
Sijasema Ndulu ni malaika
ninachosema ni mtaalam wa uchumi wa kumsikiliza kuliko Mpango na kuliko Magufuli

kuhusu wizi BOT usisahau wizi ukiwa umepangwa kitaalam
hakuna gavana wa kuuzuia...hasa kama hadi wizara zimeshiriki
Escrow ilipangwa wizarani hadi kwa mwanasheria mkuu
kumbuka BOT wao waliomba tu barua ya mwanasheria mkuu kama ushahidi ndo wakaruhusu hela zitoke

kuhusu kushuka kwa shilingi....ni mambo tele yanahusika sio tu BOT..
Ndulu naweza kusema amesaidia 'hali isiwe mbaya zaidi'
angalau inflation iko single digit miaka yote yupo hapo
mambo yangeweza kuwa mabaya kuliko hapo....

amepunguza damages za maamuzi mabaya ya wajuu wake
yeye hana mamlaka kamili ya kila kitu
 
Sina mashaka na elimu ya Prof. Ndulu (I respect his school-NU-Evanston Chicago- where he wrote his PhD).

Lakini hebu Mkuu tufafanulie tangu Huyu bwana ashike usukani pale BoT (2008?) what have we achieved as a nation in monetary perspective?? Maana in my memory colossal sum of money has been stolen from BoT under his watch. (countless number of scandals-hata yeye mwenyewe kutumia billions za walipa kodi kujijengea nyumba ya Gavana!)

Prof. Ndullu ameingia BoT...... 1USD=1250Tshs.

Leo after almost a decade while still at the top of the BoT the shilling is at 2185 kwa 1USD.

Please enlighten us. Labda kuna vitu sisi hatujui Kuhusu hawa wasomi wetu waliotukuka.

Masanja

Swali zuri sana... binafsi huwa naona yeye mara nyingi hujitokeza kujibu pale tu anapokuwa kaguswa, lakini sidhani kama kuna la maana amefanya.
 
Sifa moja ya 'watalaam wanaoujua na wanajua kwamba wanajua' ni kuwa hawapendi kujipendekeza na hawaogopi kufukuzwa.

Wao hupenda kushauri kwa sauti ndogo tu ukiamua kuwasikiliza haya ukiwadharau hasara ni kwako.

Kikwete alipokuwa Rais alifanya kosa moja lillilogharibu Taifa mabilioni baadae

Kikwete aliamua kuwasikiliza Ngeleja na Adam Malima ambao walikuwa waziri na naibu waziri na kuacha kumsikiliza Mtaalam Idrissa Rashid aliekuwa CEO wa Tanesco.

Idrissa Rashid alipoteuliwa CEO wa Tanesco alikuta nchi ina mgao wa umeme na hali ya shirika hoi na wanasiasa wanaingilia maamuzi ya kitaalam.

Akapiga marufuku wanasiasa kuingilia maamuzi kwa miaka minne ya Uongozi wa Idrissa Tanesco hakuna mwanasiasa aliezungumza kitu na mgao ukaisha na shirika likaanza kusimama Idrisa alikuwa anawajua vizuri kina Ngeleja na Malima

Malima alianza kazi BOT Idrissa akiwa gavana..

Ngeleja alipokuwa Vodacom Idrissa alikuwa kwenye Management, wangemueleza nini? aliamua tu 'kutowasikiliza.

Idrissa alivyoondolewa tu Tanesco kilichofuata ni ziara za Waziri Ngeleja Tanesco na 'mgao wa dharura ukaanza' the rest is history. Zaidi ya bilioni 500 zilikwenda. Kikwete alikosea kuwasikiliza kina Ngeleja na Malima asimsikilize Idrissa.

Magufuli anaelekea kurudia kosa hilo hilo anapaswa kumsikiliza Benno Ndulu mtaalam aliemfundisha uchumi Philipo Mpango na naamini Ndulu akisema leo ataje his best students Mpango sidhani atakuwemo.

But Magufuli anaonekana kumsikiliza zaidi Dk. Mpango ambae hata VAT tu haoeneshi kuijua vizuri hadi Ndulu alipojitokeza 'kutoa ufafanuzi.

Siku Ndulu akiondoka hapo ndo tutajua hasara kiasi gani kama taifa tutaingia.

Time will tell.

Nilifikiri ndo furaha yenu Raisi Magufuli na Serikali yake kushindwa sasa kelele za nini tena kama mna uhakika kwamba anashindwa? Kwa nini mnahangaika kumpa mtu ushauri ambaye lengo na furaha yenu ni kuona anashindwa? Mbona mnakuwa kama Wanawake ambao wana sifa ya kutokujua wanataka nini?
 
Kuna vichwa vya kukaa pale uyu Ndullu apumzike tuu ikibidi aende na JK tuu
We need new ideas and thinking kwa kweli.Zama za JK uyu uyu ndo alikuwa BOT
 
Mimi siamini kama Ndulu ni Gavana Bora...Chukulia kipindi cha Kikwete kila siku shilingi yetu ilikuwa inaporomoka, mimi natamani yule waliyesema kafia marekani angerudishwa apewe hicho cheo cha Ndulu yule jamaa kwangu ndo gavana bora kupita wote ambao wamesimamia BOT, uchumi kipindi cha Mkapa ulitengemaa kwelikweli, au wizara ya Fedha apewe Basil Pesambili Mramba.

Mkuu sasa hivi Mramba anapatikana hospitali ya Sinza Palestina anakosaidia kufanya usafi wa mazingira!
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom