Magufuli na Mnyika: Ondoeni foleni ya kujitakia Mbezi mwisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli na Mnyika: Ondoeni foleni ya kujitakia Mbezi mwisho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Dec 6, 2011.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  WADAU WENZANGU,
  nawasilisha kwenu kero ya kujitakia hapa mbezi mwisho , foleni ya magari inaanza kuanzania saa tisa hadi saa nne usiku. katika kujitaidi kupunguza foleni seriakali kupitia tanroads walijenga stendi mpya kwa mabilioni ya shilingi za walipa kodi, tangu stendiikamilike ni zaidi ya miezi sita, lakni haifunguliwi ili itumike. tuaambiwa kuwa hakuna choo, mbaya zaidi hakuna jtihada zozote zinzzo fanyika. masaa yanayopotea kwa zaidi ya magari 12,000 yanayoingia dsm toka mikoani na nchi jirani ni hasara ya mabilioni kwa siku, hasara hii inaweza kuzuililka kwa kujenga choo ambacho gharama yake haizidi 12m. waziri magufuli na mnyika tusaidieni kuondoa kero hii.
   
 2. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  [​IMG]

  Inakera sana, nasikia wanasubiri rais akipata muda kwenda kuzindua hy stendi. Tatizo lingine linalosababisha foleni ni:
  1. Matuta- Tangu shekilango rd imewekwa matatu imekuwa foleni mtindo mmoja
  2. Askari kung'ang'ania kuongoza magari muda ambao hata hakuna magari mengi hivyo kufanya foleni ijikusanye. Taa ina mgawanyo mzuri wa magari hata kama unakaa kwa foleni lakini una uhakika baada ya muda fulani utavuka. Kama pale Ubungo jamaa huweza kuvuta upande mmoja hata kwa dk 20, hasa akipigiwa simu na mshkaji wake
   
 3. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  magufuli ndo kashindwa kazi!!!we unadhani Mnyika akilishughulika kwa dhat watampa hiyo nafasi!!apate sifa za bure kwa jimbo la wajanja wa Tanzania!!mlaumu magufuli sio mnyika kaka!!!
   
 4. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa Magufuli na Mnyika wanahusika nini hapo?Kero za barabarani wahusika ni kikosi cha usalama barabarani.Mtafute Mohamed Mpinga.
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Aisee kweli kabisa. Kuna mambo mawili zaidi yanaongeza foleni hapo. Kuna askari ambaye huwa anazuia magari ili kuruhusu watembea kwa miguu wapite. Jambo lingine kubwa ni kuwa. Stand ya daladald ipo upande wa kulia kama unatokea mjini, kwa maana hiyo daladala zinazotoka mjini zikitaka kuingia stand ni lazima zisimame kwanza ili kupisha magari yatokoyo moro kupita. Kwa maana hiyo husababisha foleni nyuma yake. Kituo kipya kilikuwa sawa kabisa.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwanini sio mkuu wa Mkoa, Wilaya, Mayor wa Kinondoni au Mayor wa Jiji? Hawa watu wanafanya nini hasa? Tukumbuke kila Halmashauri huwa wanapata fungu kwa ajili ya kukarabati barabara zake. Pia Halmashauri zina vyanzo vingi tu mapato i.e mango etc. Hakuna taa barabarani, mitaro imejaa maji machafu, mji unanuka. Wanafanya nini hawa watu? Matatizo mengi tunayatupa kwenye serikali kuu i.e Wizara wakati huku chini wajanja wanakula posho na kupiga mnada mali za umma (UDA).
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Kwa Kweli Ukifuatilia foleni Katika barabara ya morogoro utakuta ni ya Kujitakia Kabisa!! Kuanzia Mbezi Mwisho!! Kimara Suka, Kimara Mwisho, Ubungo Maji, Ubungo Junction na Ubungo stand ya Mkoa!! Kwa kweli ukifuatilia utakuta Utagundua Chanzo Cha foleni Yote ni Kupuuzia na kutokuwepo utaratibu wowote katika Matumizi ya barabara!!

  Mchanganuo

  Suluhisho la Hizi Foleni Kulingana na Eneo

  1. Mbezi Mwisho: Tatizo kubwa la Hapa ni Muingiliano Mkubwa wa Shughuli za Kibinadamu! Kando kando Sana ya Barabara, Hii inafanya Madereva kupita eneo Lile kwa tahadhari Kubwa Kuogopa Kusababisha ajali au Hata Kugonga Bidhaa za Watu!!
  Pia katika eneo lille Limetokea Ghafla Kuwa na wingi wa Watu Huku Kukiwa Hakuna Utaratibu wowote Umefanywa Kuwawezesha Watu Kupita kwa Ustaarabu!! Tunaomba Halmashauri Ya Kinondoni Itangaze Rasmi je lile ni Eneo la soka au Eneo la barabara??

  2. Eneo la Kimara suka: Chanzo Kikubwa cha foleni pale ni Uwepo wa Tuta Kubwa ambalo ni Chanzo Kikubwa cha Uharibifu wa Barabara!! Pia kituo kilichopo Kimewekwa Kabisa Sambamba na Tuta Hivyo Kufanya daladala Nyingi Kusimama Kwenye Tuta kwa Kisingizio cha Kupisha waenda Kwa Miguu na kupakia abiria na Hii Husababisha Foleni Kubwa Isiyokuwa na Ulazima!!

  3: Kimara Mwisho: Sehemu hii inamuingiliano wa Matumizi ya Barabara (Kama magari Kugeuzia Pale na Kituo cha Basi Kuwa Karibu Kabisa na Barabara!! ) Ushauri wangu ni Kuwaomba Wahusika Kujenga Kituo Kingine Kwa Ajili ya daladala maeneo ya Bondeni Kule ili Kuwe na Bus Stand Kama Magomeni Mapipa!! na stend ya barabarani ibaki kwa ajili ya Mabasi Yanayotoka Mikoani!!

  4: Ubungo Maji: Eneo Hili lina Usumbufu Mkubwa wa Daladala!! Stendi imekaa Karibu sana na Barabara na Hii Husababisha Mwiingiliano Mkubwa wa Daladala na Malori Makubwa!! Pia Uwepo wa Tuta Kubwa Pale Umesababisha Barabara Kuharibika ambapo Umuhimu wa lile Tuta Hata Haonekani!! Kwa Muda mrefu Magari yanakuwa Kwenye Foleni Kusubiri Kuitwa na Trafic Police kwenye Junction!! Na Hivyo sioni sababu ya Tuta Kwani Watu Wanaweza Kuvuka Wakati Magari yanasubiri Kuitwa!! Hivyo Basi Uwepo wa Tuta Pale ni Kuharibu Barabara na kuongeza msongamano wa Magari pindi Yanapoitwa na sio Msaada Wowote kwa Wavukaji.

  5; Ubungo Junction: Mimi nawaomba wahusika Wazibe Mashimo Yaliyopo Katikati ya Maungio ya barabara na hivyo kusaidia watu Kupita kwa Kasi Kidogo!! Pia Waenda kwa Miguu waweze Kuwezeshwa Kidogo katika eneo Lile la Kuvukia!! Kwani pale Hali ni Mbaya ukizingatia na lile soka lisilo Rasmi ambalo Limeingia hadi barabarani!!

  6: Ubungo Stand ya Mkoa (Central Bus Terminal)!! Kwa Kipindi Hiki cha Karibia na sikukuu za Mwisho wa Mwaka Huwa Tatizo la Pale Linazidi Kabisa!! Hadi Kero Kupindukia!!
  Chanzo cha Tatizo!
  Kwa Kipindi hiki cha Mwisho wa Mwaka kuna kuwa na Mwingiliano Mkubwa wa Wasafiri, ambao wengi wanakuja na magari Binafsi ya Ndugu zao na Wengine na Magari ya Kukodi!! Sasa Muingiliano unaanza pale Kila Mtu anapokuwa Hataki Kuingia Ndani Ya Stendi KUU!! Hivyo watu wote wanataka Wapaki pale Nje na Kuwashusha Wasafiri wao na Kuondoka!! Tatizo Kubwa Lipo kwa Taxii ambao pia wanaogopa Kuingia Ndani kwa Hofu ya Kulipishwa Ushuru wa Kuingia ndani!!
  Suluhisho
  Tunawaomba Mamlaka zinazohusika Kuongeza eneo la Maegesho Nje ya Stendi Kuu!! Eneo lote linalopakana na barabara Kuu lijengwa vizuri kwa ajili ya maeneo ya Kuegesha magari ya watu ambao Hawana ulazima wa Kuingia Ndani!! Tungeomba iwepo parking ya angalau Magari 500, Hii ingesaidia sana Kupunguza Msongamano na Barabara Kuachwa Wazi kwa Watu wanaokwenda Mjini Moja kwa moja.
  Pia Stendi ya daladala kwa mabasi Yanayotumia babara hiyo kwenda sehemu Mbali mbali haitoshelezi Mahitaji kabisa!! Inaonekana ni Muhimu sana Kuongezwa kwa eneo la parking ya daladala na Kuwatoa nje kabisa ya Barabara!! Mfano wa Kuigwa na pale Buguruni Rozana
  Nawasilisha
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu hapo kwenye green; kwa kweli sijakuelewa - kwamba wananchi watembea kwa miguu hawana haki ya kupata wasaa wa kuvuka kwa usalama au? India na China (nchi zenye watu wengu zaidi duniani) kwa maeneo yenye taa za barabarani zimesetiwa kuruhusu sio magari tu bali watembea kwa miguu na wakati huo magari yote yanakuwa yamesimama yote. Ni bongo tu mlalahoi huonekana hana umuhimu.

  Kwenye
  red; hata kama stendi ikiwa upande wa kushoto, still ita-create foleni wakati daladala zinatoka kituoni kuingia barabara kuu au zinazotoka upande wa Kibaha kuingia kituoni (U-turn). Kumbuka siku hizi kuna magari kutoka nje ya mji yanaishia Mbezi.

  The only solution ni kuwa na madaraja ya juu kwa magari na watembea kwa miguu. Yote yanawezekana kinachokosekana ni utashi na utayari wa kisiasa.
   
 9. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  nimeipenda analysis yako nami naunga mkono mapendekezo uliyotoa hasa Mbezi mwisho. kwanza wafanyabiashara barabarani watoke na ikiwezekana wanaokatisha barabara wawekewe utaratibu maalumu kama wa daraja au underground way.
  namimi naongezea pale Manzese - wafanyabiashara wanapanga vitu barabarani ni kama Ubungo Junction

  Mbunge Mnyika anaweza kuhamasisha wananchi wasifanye biashara jirani kabisa na barabara
   
 10. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Trafic light fire, zinacount muda at least madereva wanapata muda wa kujiandaa kufanya maamuzi stahili. Ijapokuwa inaonekana mchina sana bora technologia hii ikapelekwa sehemu mbalimbali
  ili kutoa nafasi ya kisaokolijia kwa watumiaji wa barabara kusubiri.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Kama ni choo si wampe private investor tu ajenge? By the way, mbona stand nyingi hazina vyoo!!
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  thread hii imesheheni mawazo mazuri, tanroads na kinomndono mmc msiache kuyafanyia kazi
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nyie mmeona foleni ya mbezi tu. Ya mandela road je? Si bora kimara huko? Tena natamani kuhamia huko niepukane na foleni ya mandela
   
Loading...