Magufuli na maamuzi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli na maamuzi yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundamilia07, Dec 10, 2009.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa mara nyingine tena tunaona jinsi Bwana John Pombe Magufuli anavyoiingiza serikali katika madeni ambyo yangeweza kuepukika. Kama mtakumbuka wakati akiwa Waziri wa Ardhi aliidhinisha na kukaidi mamlaka zilizozuia uvunjaji wa kituo cha mafuta pale Mwanza ambapo matokeo yake serikali ilijikuta ikitemeshwa Shilingi Bilioni 5 kama fidia ya kuvunja kituo kile.

  Leo hii SAMAKI, ambapo tunaelezwa kuwa gharama ya kuwahifadhi sasa ni kubwa na inazidi kuongezeka. Na huenda hiyo kesi itakuja kuzaa madai makubwa zaidi ya yale ya kituo cha mafuta cha Mwanza.
  Haya tusubiri!!!

  Seized fish storage cost now 1.2bn/-

  FAUSTINE KAPAMA,
  9th December 2009


  THE storage costs of fish seized from of MV Tawariq 1 whose 37 crew members are charged with illegal fishing in the country’s deep sea waters of the Indian Ocean has now reached 1,169,399,702/-, the 'Daily News' learnt yesterday.

  The value of the fish is estimated at 2,074,240,000/-. Director of Fisheries in the Ministry of Livestock Development and Fisheries Godfrey Nanyaro said the consignment was now a burden to the government, hence the need to dispose of the same urgently.

  Mr Nanyaro said this in his affidavit filed at the High Court on Monday to support the new application by the prosecution, seeking orders to allow the government to distribute the fish freely.

  He stated in the affidavit that since October this year when the court ordered the government to dispose of the fish by way of international tender, the ministry had received no bidders for the consignment.

  According to him, the cost kept on rising as fish was stored at a cost of 3,511,992/- per day and that continued storage of the consignment affected the status, quality and value of the fish.

  In the application filed under certificate of urgency, the prosecution is asking the court to vary the conditions embodied in its orders given on October 1 and 20, this year regarding the disposal and sale of the fish.

  The consignment weighing 296.32 tonnes valued at 2,074,240,000/- is the subject of criminal case against the crew members charged with illegal fishing within Exclusive Economic Zone of United Republic of Tanzania.

  The prosecution is further seeking orders to distribute the fish free to institutions and interested persons and vary conditions relating to the making and filing reports of the mode and proceeds of sale.

  Apart from Mr Nanyaro, the Permanent Secretary of the Ministry, Dr Charles Nyamrunda, has also sworn an affidavit indicating that once the fish is distributed freely, the government would reimburse the accused the money equal to value of the fish if acquitted.

  The decision by the prosecution to file the new application comes few days after Judge Razia Sheikh rejected the first application because it was supported by an incurably defective affidavit sworn by Mr Nanyaro.

  She upheld an objection raised by Capt. Ibrahim Bendera, advocate for the accused, that the affidavit by Mr Nanyaro was incurably defective because it contained objections, analysis, prayers, legal arguments and conclusions, which was illegal. Judge Sheikh is expecting to hear the new application today.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Magufuli anafanya kazi kama vile Tanzania ni ka nchi kako ndani ya bara la Ulaya au America. as a result akisimamia sheria na ukweli kwa jinsi anayojua taratibu , kila kitu kina mrudia yeye kwa sababu systems au idara zingine hazifanyi kazi kwa level, standard na kasi yake. He is not a leader of this age kwa Tanzania yetu hii! If he is then president is his best position!

  Ukimuuliza yeye akupe majibu na kale kalafudhi kake ka huko kaskazini with evidence na sheria gani anasimamia utaona, ukipima matokeo ya kazi yake, they Guy alitakiwa Kuwa rais wa zama hizi ili atupeleke kwenye standard yake.

  Maskini sie huruma zetu hizi za kutosimamia sheria kwa gharama yeyote ndio imetufikisha hapa!

  Kinachonipa homa tu ni hili li chama lake Arhuuuuuuuuuuuhhh! 'because my concept ni kuwa wote ndani ya CCM mafisadi' I can defend this concept kwa kila namna!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hapana Magufuli hakukamata ile Meli ila ilikamatwa na Maafisa uvuvi wa kikosi cha doria kanda ya Dar es salaam, nikiwa Dar nilifatilia kiasi hili sakata, kinachoonekana ni kua wale maafisa uvuvi waliishika ile meli kama sheria ya nchi kupitia fisheries act nafikiri ya mwaka 2007 inavyoagiza, sasa Magufuli yeye ni msimamizi mkuu wa shughuli za Wizara hiyo,......rejea majukumu ya waziri kwa wizara.
  baada ya maafisa Uvuvi kukamata meli hiyo wakishirikiana na police na NAVY NA KIKOSI CHA Askari wa doria cha SADC sasa baada ya kukatwa wale waharifu swala linabaki kua la wizara ya sheria na Ofisi ya DPP.
  Tatizo ni lilelile Je DPP anatimiza wajibu wake, je wizara ya Sheria na katiba imetimiza wajibu wake.?
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii imekalia vibaya! ila huyu bwana ni mdunda kazi kwelikweli
   
 5. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona unataka kuleta mambo ya kuuza ng'ombe ili utatue kesi ya kuku.kwa mtazamo finyu unaweza ukaona gharama za kuhifadhi hao samaki ni kubwa saaana lakini huangalii thamani ya samaki wetu wanaovuliwa kinyume cha sheria na maharamia-bahari kwa miaka mingi sasa.hao samaki ni kidhibiti katika kesi inayoendelea dhidi ya maharamia waliokamatwa na meli ile ya uvuvi.
  unapotaka wauzwe au wagawanywe kwa watu bure unamaanisha ni kuondoa kidhibiti ambacho ndio kigezo cha kutoa hukumu.
  acha wahifadhiwe ili mwisho wa siku haki itendeke kwani kwa mujibu wa mahufuli,kiwango cha wizi wa rasilimali zetu, ni kikubwa kiasi cha kutisha kiasi kwamba kama tungekuwa tunalipwa na hawa maharamia-bahari basi sector ya uvuvi pekee ingetosha kutukwamua kiuchumi
   
 6. a

  alles JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvumali, umetoa darasa tosha kwa watu wasiojua mgawanyo wa madaraka/kazi wa serikali. Kuna wakati inabidi tuweke ushabiki pembeni,tutanue mawazo yetu na tuangalie vitu kwa mapana yake.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  What price do we want to pay to put in place proper working systems?
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,123
  Trophy Points: 280
  tumechoka jamani eehh......................
   
 9. M

  Mchili JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35


  Kama magufuli alivyowaambia, hiyo sio hasara ni gharama ya kesi itakayoweza kutatua tatizo la muda mrefu. Ukitizama figure kwa haraka haraka unaweza fikiri ni hasara kubwa lakini kwa serikali ni matumizi ya kawaida ya utendaji.
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wimbo wetu uliobora mtamu masikioni mchungu moyoni
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi yule Dr. Tezaghe (sina hakika kama nimelitaja jina lake sawasawa) alirudishwa kazini?.......

  Mkuu unaweza kutupa background kwa nini kile kituo kilivunjwa?
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Yafaa kumpongeza Magufuli na siyo kumbeza au kumlaumu. Matatizo yapo sehemu nyingine... DPP et al
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  labda sisi kama taifa lazima tujue kua ofisi ya DPP Inamapungufu ya wazi sana na ndio maana siku moja mtu mmoja anaitwa Tundu Lissu alisema hajawahi kushindwa kesi yoyote aliosimamia dhidi ya maofisa toka ofisi ya DPP, akiwa na maana hii ofisi imejaa uzembe na ubabaishaji.
  kwemye hizi wizara zina Wanasheria ambao wanamuwakilisha Mwanasheria mkuu wa serikali na wizara ya Sheria na katiba, hawa mara nyingi hudaiwa wanashirikiana na washitakiwa wa serikali ili serikali ishindwe kesi na wahalifu kama hawa washinde kisha wao hupewa mlungula kama shukrani.
  hii imetokea mara kadhaa amini nawaambia sasa tunaweza kukaa na kumlaumu Magufuli na baadhi ya Watendaji wake pale wizarani bila kuwatazama hawa watu wenye taaluma zao za kisheria, ila nijuacho mimi ofisi y DPP Inakosa wanasheria makini au wanafanya kazi za hovyohovyo wakitarajia manufaa toka kwa watuhumiwa.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,737
  Likes Received: 4,959
  Trophy Points: 280
  ..nadhani Magufuli ni very intelligent and hard working.

  ..lakini amefanya maamuzi mawili ambayo kwa mtizamo yamemtia doa kubwa.

  ..uamuzi wa kwanza ni kuuza nyumba za serikali. ile ni hasara kubwa kwelikweli.

  ..suala la pili ni pale alipopuuza ushauri wa wataalamu na kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. Mahakama Kuu imeamua serikali ilipe Tshs 14.7 billion.

   
 15. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi si muoni Magufuli kama ni mtu ambaye anaweza kufanyakazi as a team, he is very selfish and arrogant.
  Ninaweka maelezo haya katika kiwango cha kawaida kueleweka. Katika muda ambao nimepata kumfahamu, the guy is not real. He's a politician kama walivyo wengine, right now he is maintaining low profile kwa sababu za kisiasa.
  Kama ulivyosema juu ya nyumba za serikali, yeye na kundi lake walibuni uuzaji wa nyumba za serikali ili kutimiza matakwa ya ubinafsi (selfishness)
  Na pale wananchi walipokuwa wanalalamika aliwaeleza kuwa nyumba za serikali zitaendelea kuuzwa na hatositisha zoezi hilo (arrogancy). Matokeo yake serikali kuingia gharama zisizo za lazima kuwapatia watendaji wengine makazi
  Kitendo cha kudharau mamlaka zingine na kuamuru kituo cha mafuta kivunjwe (arrogancy).
   
 16. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Keep it up Dr. Magufuli!
   
 17. GP

  GP JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mtoa mada hapo juu(Pundamilia07):, Dr Magufuli kweli ni BIG SELFISH.
  huyu jamaa akiwa waziri wa miundombinu alijichepushia barabara ipite nyumbani kwao Chato, so selfish.
  mi najiuliza sana kwa wale wananchi ambao wabunge wao sio mawaziri watasema nini sasa????, inamaana kwao hakutakua na maendeleo??.
   
 18. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Blood of Fisadis
   
 19. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mgawanyo wa madaraka wa kazi za Serikali tunaujua. Magufuli ndiye kiongozi mkuu wa Wizara hiyo na msimamo na mtazamo wake katika suala zima la uvuvi haramu ndio uliosababisha meli ile ikamatwe. Kaisari apewe yanayomstahili!

  Wakitoka maafisa uvuvi ama hao watendaji mnaowasema ndani ya Wizara yake wakaboronga je atakayewajibika na kelele kupigwa ajiuzulu si Magufuli?

  Magufuli anastahili kuwa Waziri Mkuu wa nchi hii na ataiendesha vyema na kwa mafanikio makubwa na Rais wake ataweza kubembea atakavyo akijua nchi ina anayeishikilia na kuiendesha kishupavu. Kwa kifupi Magufuli ni Mwanasiasa na Mtendaji anayethubutu.
   
 20. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280

  Ndiye Mgombea ambaye CCM wanaona eti Jembe- Kama ni jembe ujue Jembe ya kulimia kwenye Mchanga na si shamba Bora lenye rutuba na ardhi nzuri.

  Kiongozi anayetumia hisia katika kutekeleza majukumu yake hafai na Magufuli hana tofauti na EDO.


  UKAWA leteni Mgombea bora na Makamu wake ambaye si Mzigo kwa Umma.
  Wakati Mnafanya hivyo itapendeza hata makatupatia ahadi ya Watu wawili Kama PM mtarajiwa. Tuna hitaji timu tukayo iamini jambo hili wakati huu ni lamuhimu sana-kuakaa na wateule kwenye Mfuko ya wateuzi si muda wake hasa kipindi hiki cha Ukombozi wakombolewa wantaka kuwajua wapiganaji wao mapema iliwaze kuwaamini na kuwa na matumaini.


  Ikiwezekana tupeni Full list ya Baraza la Mawaziri watarajiwa. Kama ni ya watu 15 Wekeni wateuliwa 30 kwamba ndani yake ndiyo watateuliwa watu 15.

   
Loading...