Magufuli mwambie Nyerere Wakoloni weusi wamerudi kwa kasi

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
134
500
Wakoloni weusi wanasema ule mradi wa Rufiji hauna tija , Profesa Assad amesahau mwaka 2018 alikushauri kuwa ndio mradi wenye gharama nafuu

Wakoloni weusi wamesahau uliwaagiza ATCL wakamchukue Zitto Kabwe Kigoma alivyopata ajali, walidhani pesa zinatoka Mbinguni

Wakoloni weusi wamesahau ulivyojenga hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya, hata kule Nkasi wamesahau tangu ukoloni hawakua na hospitali ya Wilaya na Wilaya ilianzishwa mwaka 1978.

Magufuli hata wale vijana wa mitano tena wapo kimya wamekuwa mabubu wanawaogopa Wakoloni weusi.

Wakoloni weusi waliokubeza wakati unamteua Kichere leo wanaomba msamaha, wanasema yale maagizo uliyompa siku ile Kichere asingesema mbele yako?

Wamesahau ulimuambia unataka ukafanye kazi na wamesahu ulifariki tayari ripoti imeshaandikwa

Wakoloni weusi siku hizi watoto wao wanasoma Ubelgiji na wengine wanaenda kufanya biashara nje ya nchi.

Wakoloni weusi wanataka stendi ya Mbezi ibomolewe ili waendelee kuiba mapato Ubungo na mvua ikinyesha liwe bwawa.

Magufuli muambie Nyerere mama Samia ameapa kuendeĺeza miradi yote mikubwa uliyoacha.

Wakoloni weusi hawataki kulipa kodi wanajificha kwenye siasa ,ukiwadai wanasema ni mambo ya kisiasa .

Magufuli mwambie Nyerere wale niliokuwa nawaalika Ikulu nao wananisema nilikuwa sishauriki. Wakoloni weusi wanataka mikataba ya kinyonyaji isainiwe ili nchi itaifishwe mbeleni

Magufuli mwaambie Nyerere ile kazi uliyomtuma Kichere kubaini wizi unaofanyika kwenye Halmashauri tayari Ummy Mwalimu ameshaanza kuufanyia kazi.

Magufuli mwaambie Nyerere, Clouds wameshaonesha risiti za Electronic walizozopewa pesa zao kwaajili ya malipo.

Wakoloni weusi siku hizi wanapishana kwenye vyombo vya habari lakini habari njema ni kwamba Mama Samia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanapishana kutekeleza miradi uliyoianzisha.

Magufuli mwambie Nyerere kazi kule inaendelea japo Wakoloni weusi wanarudi kwa kasi
 

Kijogoodi

Senior Member
Mar 29, 2021
181
500
Wenye makontena wakilalamika kwa kucheleweshewa mizigo yao , hapo roho kwatu kwa Chadema kwa sababu Magufuli amenyooka kwa kupata hasara.


Screenshot_20210412-113821.jpg
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,068
2,000
Mradi wa Nyerere sijui kwanini unaongelewa... Kama ni ndoa ishafungwa kumjadili mchumba hakusaidii. SGR nao hivyo hivyo, tujadili mengine
 

mume wa mtu

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
652
500
Mradi wa Nyerere sijui kwanini unaongelewa... Kama ni ndoa ishafungwa kumjadili mchumba hakusaidii. SGR nao hivyo hivyo, tujadili mengine
Huwa nashangaa sana hii miradi inavyotajwa wakati hata robo haijafika,tuna safari ndefu kuimaliza hii miradi kwasababu kama kukopa tumeshakopa sana,ndio maana sasa tukaingia kwenye mambo ya taskforce kukwapua pesa za wafanyabiashara kwa kuwabambikia makodi yasiyolipika ili kutaifisha mali zao,mambo ya kesi za uhujumu uchumi halafu mnakubaliana na watuhumiwa wanalipa pesa wanaachiwa huru ndio tulipokuwa tumefikia ili hii miradi iwezekane kufanyika vinginevyo haiwezekani!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom