Magufuli, Mwakyembe hatarini

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
250
MIKAKATI ya kuwakwamisha kiutendaji Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwekyembe, inadaiwa kuanza kuandaliwa na vigogo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kushirikiana na baadhi ya makandarasi, Tanzania Daima Jumapili imedokezwa.

Mawaziri hao wameanza kuonekana tishio kwa baadhi ya vigogo wa TANROADS ambao inadaiwa walikuwa wakijinufaisha kupitia zabuni mbalimbali zilizokuwa zikitangazwa na serikali.

Vigogo hao wa TANROADS inadaiwa walikuwa wakivuna fedha kutoka kwa wamiliki wa kampuni za ujenzi ambao walikuwa wakitoa fedha ili kujenga ushawishi wa kampuni zao kupewa ushindi wa zabuni husika.
Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa hivi sasa baadhi ya vigogo hao wamekuwa na wasiwasi wa kuendelea na mchezo huo wa kuvuna fedha hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Magufuli kuwa Waziri na Dk. Mwakyembe kuwa Naibu Waziri.

Magufuli alipoanza kazi katika wizara hiyo alibatilisha tangazo la ajira lililotolewa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Ephraim Mrema, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akishtumiwa kwa kuiendesha ofisi hiyo kwa masilahi ya kundi fulani la watu.

Kinachochangia wasiwasi wa watendaji hao ni hatua ya wizara hiyo kutoa taarifa kuwa imempa barua ya kuondoka kazini Mkurugenzi wa TANROADS, Ephraim Mrema, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kuitumia ofisi hiyo kwa masilahi binafsi.

Mrema, pia alikuwa akidaiwa kufanya marekebisho kwa baadhi ya watendaji mikoani na makao makuu kwa lengo kuweka safu mpya itakayokuwa na utii kwa yale atakayokuwa anawaagiza.
Marekebisho hayo yalizusha mzozo mkubwa ambao ulitikisa TANROADS na Wizara ya Miundombinu iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Shukuru Kawambwa ambaye kila mabadiliko yanayofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika baraza la mawaziri humkumba.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa baadhi ya makandarasi ambao walikuwa wakinufaika na kuwapo kwa Mrema hivi sasa wanafanya mikakati ya chini kwa chini ikiwamo kuhujumu baadhi ya miradi ili uongozi wa Mafuguli uonekane haufai, hasa katika sekta ya ujenzi wa barabara.
Habari hizo zilidokeza pia kuwa Mrema, alikuwa akiungwa mkono na baadhi ya vigogo waliopo serikalini ambao wana kampuni za ujenzi lakini wamekuwa wakiwatumia ndugu au jamaa zao kuziendesha.

Tanzania Daima Jumapili, ilidokezwa pia kuwa Mrema alikuwa na uhusiano na baadhi ya vigogo wa ikulu au familia zao jambo lililokuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzake.
Taarifa hizo zilidai Waziri Magufuli, anaonekana kuwa tishio kwa makandarasi wa barabara ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinufaika na fedha za ujenzi wa barabara, ambapo walikuwa wakizidisha gharama zake.

Wakati wa utawala wa Magufuli katika wizara hiyo, ujenzi wa kilometa moja ya lami ilikuwa sh milioni 300-400 lakini hivi sasa kilometa moja ni sh bilioni moja.
Wataalamu wa masuala ya ujenzi wanabainisha kuwa pamoja na kupanda kwa gharama za vifaa, lakini gharama za ujenzi wa kilometa moja ya lami kwa sh bilioni moja ni mkubwa na kuna uwezekano baadhi ya watendaji na makandarasi wananufaika na ongezeko hilo.
Wataalamu hao wanadokeza kuwa Magufuli atakabiliwa na wakati mgumu wa kurekebisha jambo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linawanufaisha makandarasi na wale wanaofanikisha mipango ya kuwapatia zabuni.

Ufuatiliaji wa karibu wa Magufuli pamoja na uwezo wake wa kuhifadhi takwimu ndio unaowatia hofu wale wote waliokuwa wakinufaika na fedha za serikali kwa kutumia njia za mkato.
Historia ya Magufuli kufuatilia ubora wa barabara au jengo linalojengwa ndio unaozidisha hofu kwa makandarasi ambao wamekuwa wakijenga chini ya viwango kwa lengo la kujinufaisha zaidi.
Mara kadhaa wakati akiwa Waziri wa Ujenzi, Magufuli alikuwa akiyakataa majengo, barabara au kuvunja mikataba pale anapoona havikujengwa kwa kiwango kinachotakiwa.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kuhusu kuwapo kwa taarifa hizo za kuhujumiwa, Mwakyembe alisema ni mapema mno kulizungumzia jambo hilo, kwa sababu ndiyo kwanza ameingia ofisini na anahitaji muda zaidi kujua nini kinafanyika ndani na nje ya ofisi hiyo.

Alisema kuwa muda ndio utakaoamua kuhusu njama hizo, lakini katika mazingira ya kawaida hakuna mkandarasi au mtendaji wa serikali ambaye anaweza kufanikisha hujuma kubwa kama hiyo.
"Ndugu yangu, sina jibu la kukupa kuhusu njama hizo, lakini ni vema tukapeana muda ili tuweze kufanya kazi," alisema Mwakyembe.

Source : Tanzania Daima
 

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,203
1,195
Watanzania tuna imani na Magufuli katika wizara hiyo. Inasikitisha kuona ni jinsi gani peas zetu watanzania zinavyoliwa bila utaratibu, gharama ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tsh. 300 - 400 millioni mpaka Tsh. 1,000 Millioni kwa kilomita ndani ya miaka mitano tu? Hakuna ujambazi kama huu jamani! CCM haitufai hata kidogo.
 

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,424
0
Tanzania Daima, do investigative journalism. Msituletee conspirancy theories na wishful thinking zenu.

Shoddy juornalist(s/m).
 

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,285
1,500
sijaona hatari yoyote kwa waziri magufuli na naibu wake mwakyembe. watakaooneka na kudhibitishwa wanakwamisha sheria itawabana na waziri atapigilia msumari wa moto. ngoja uone barabara zitakavyojengwa sasa
 

Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Tanzania Daima, do investigative journalism. Msituletee conspirancy theories na wishful thinking zenu.

Shoddy juornalist(s/m).

Are these not facts? do you know what you are saying or you are also counted in the same boat? Hujui unachokanusha fisadi mkubwa
 

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
250
Tanzania Daima, do investigative journalism. Msituletee conspirancy theories na wishful thinking zenu.

Shoddy juornalist(s/m).

Mimi nakushangaa Ama kichwa yako imejaa siasa,mimi toka nimelifahamu Tanzania Daima sijawahi kusikia limefungiwa au kupewa onyo lolote.Ni gazeti linaloandika habari bila upendeleo wowote.Mmiliki wa kampuni ya free media huwa haingilii utendaji wa wahariri wa Tanzania Daima.Hata Msajili wa vyama vya siasa alilisifu gazeti la Tanzania Daima kuwa liliandika habari za uchaguzi bila hata ya kupendelea chama cha mmiliki

Wewe fikiria Tanzania Daima ilikuwa inaandika mwenendo wa kesi ya Dr.Slaa kama ilivyo.Sasa nakushangaa Ama una maana gani ,hii siyo makala ,hii ni habari lazima utofautishe.
 

Rodcones

JF-Expert Member
Oct 16, 2007
401
225
Wakianza majingu watakwisha maguli anafanya kazi na anajiamini so nina imani nae kabisa.


Ningependa agombee uraisi 2015 kama.
 

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,407
2,000
Tanzania Daima, do investigative journalism. Msituletee conspirancy theories na wishful thinking zenu.

Shoddy juornalist(s/m).
Mkuu Ama, amakweli wewe una uelewa mdogo katika sekta hii.
Tz Daima wamesema kweli bila kutaja majina. Mkandarasi anayehusika hapa ni mhindi na ni mbia wa subash patel. Alipewa kazi ya kumalizia km 16 za barabara ya Dodoma Manyoni kwa bilioni 32!!!(20 b zilitafunwa).
Sasa kapewa Bagamoyo Msata kwa bilioni 105,wakati tenda ya chini ilikuwa bilioni 80.(bilioni 20 kutafunwa tena)
Kipande cha kumaliza Dodoma Manyoni ujenzi wa barabara ulikuwa bilioni 2 kwa kilpmeta!!!!!
Msata Bagamoyo bil 1.6 kwa km!!!!
This is common knowledge hata humu Jf ipo hii info.
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,299
2,000
Mkuu Ama, amakweli wewe una uelewa mdogo katika sekta hii.
Tz Daima wamesema kweli bila kutaja majina. Mkandarasi anayehusika hapa ni mhindi na ni mbia wa subash patel. Alipewa kazi ya kumalizia km 16 za barabara ya Dodoma Manyoni kwa bilioni 32!!!(20 b zilitafunwa).
Sasa kapewa Bagamoyo Msata kwa bilioni 105,wakati tenda ya chini ilikuwa bilioni 80.(bilioni 20 kutafunwa tena)
Kipande cha kumaliza Dodoma Manyoni ujenzi wa barabara ulikuwa bilioni 2 kwa kilpmeta!!!!!
Msata Bagamoyo bil 1.6 kwa km!!!!
This is common knowledge hata humu Jf ipo hii info.

Jamani wananchi wote wanajua uhusiano aliokuwa nao Subash Patel na watawala wetu kwahiyo kama kampuni yao imepewa kujenga Msata- Bagamoyo kwa bilioni 105 basi mjue zingine zinapelekwa kwa wazee wa nchi !! Hata hivyo si mnakumbuka kampuni ya kikorea iliyopewa kujenga barabara hiyo hiyo wakishirikiana na Suma JKT ilivyokwapua mabilioni ya fedha na kutoweka lakini hakuna hata mtu aliyewajibishwa; baada ya hapo ndio amepewa partner wake Subash!! Gharama za ujenzi wa hii barabara ni sawa na kujenga huko AHERA; muungwana anaiua nchi jamani.
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
bn105 bmoyo-msata wakati tabora,kigoma na rukwa hawana hata 1km ya lami ya uhuru wa tanganyika huo si uhuni jamani?
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,531
2,000
Tanzania Daima, do investigative journalism. Msituletee conspirancy theories na wishful thinking zenu.

Shoddy juornalist(s/m).

. Ama, hawa ndo zao, hutunga habari ya kuuza gazeti, huwa hawana habari ya maana kwa mtu yeyote anayejua habari.
 

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
250
Kwa nini mliwachagua viongozi mafisadi,viongozi wetu wanaonekana watakatifu machoni pa watu lakini nyuma ya pazia ni wezi wakubwa.Kwa nini km 1 ni sh bilion 1.6?? .Eee Mungu uinusuru nchi yeu
 

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
0
Kama ni wezi siku za mwizi ni arobaini tu. Hivyo wasubiri zikifika nao wataisha tu.
 

Juaangavu

JF-Expert Member
Nov 3, 2009
935
250
Kwa nini mliwachagua viongozi mafisadi,viongozi wetu wanaonekana watakatifu machoni pa watu lakini nyuma ya pazia ni wezi wakubwa.Kwa nini km 1 ni sh bilion 1.6?? .Eee Mungu uinusuru nchi yeu
<br />
<br />
Mungu awashughulikie hao majambazi, na ikiwezekana awauwe wote. Haingii akilini kabisa, kwa huu ukamuzi unaoendelea ndani ya hii nchi. Sijui ni lini wananchi wote wataelewa kinachofanywa na waliokabidhiwa madaraka ya kuwaongoza, hakika patapendeza sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom