July 31, 2020
Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni wamekubaliana kurejesha kwenye Ikulu zao mchakato wa kutandaza bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.
Bomba hilo linaloanzia Hoima, Uganda na kuishia Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, limekwama baada ya kuwepo kwa “vizingiti” ndani ya serikali zao na hata wawekezaji katika mradi huo.
Wawekezaji katika mradi huo mkubwa wa kusafirisha mafuta, ni Total, Tullow na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya China.
Chanzo: Magufuli, Museveni wakubaliana kuufufua mradi wa Bomba la Mafuta