Hess
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 593
- 675
Wadau,
Baada ya Rais wetu kuapishwa, alijipa kazi ya kutumbua majipu. Hadi sasa kazi hiyo anaifanya vizuri. Nampongeza.
Wakati anatangaza baraza lake la mawaziri, JPM alimteua Nape kuwa waziri wake wa habari, michezo na utamaduni. Uteuzi huu iliibua hofu miongoni mwa wamilki wa vyombo vya habari.
Imekuja kubainika kuwa uteuzi huu haukufanywa kwa bahati mbaya ila kimkakati. Mkakati ulikuwa ni kumfanya mtawala ajitenge na vyombo vya habari. Na hii imedhirika ndani ya siku chache tu Magufuli kaondoka na MAWIO na leo kaondoa TBC bungeni kama chombo cha kuwajuza watanzania yanayojiri bungeni.
Maswali ni haya, Magufuli nisaidie;
1. Kwanini unaviogopa vyombo vya habari?
2. Kwanini umefuta MAWIO gazeti lililokuwa likusaidie kuanika majipu ili iyatumbue vizuri?
3. Kwanini unawanyima watu haki ya kupata habari? Kwanini TBC unaitoa bungeni?
4. Unatumbua majipu, kwanini majipu mengine hutaki yaanikwe na media?
Nilianza kukuamini nilipoona kasi yako kwa mafisadi, lakini naingiwa hofu sasa TZ tunaanza kuandaa Rais sultani na Dikteta. Madikteta wote duniani hawapendi media.